With all due respect you are dodging the qn!
Hakuna mtu amesema USA hatoi misaada, matter of fact hata hii net nalalia hapa ni kwa hisani ya USAID. Kuhusu donation na misaada haikuwa hoja, hoja ilikuwa urusi wanajeshi wake wanakufa njaa vitani huko ukraine. Nikakuambia haiwezekani wanajeshi wa urusi wafe njaa wakati huohuo urusi anatoa msaada wa chakula na afya kwa raia wa ukraine mpaka kwa wanajeshi wa ukraine waliojisalimisha! Rationally speaking, Priority ya kwanza ya Urusi ni wapiganaji wake hivyo hawawezi kutoa chakula kwa watu wengine (tena wanaopigana nao) wakaacha kuwapa wanajeshi wao ambao wanawategemea zaidi kwenye kushinda hii vita. Ukiona wametoa msaada kwa wapinzani wao ujue wao tayari wametosheka. Au we unafikiri Putin na kremlin yake wanaweza kutoa chakula kwa ukraine akaacha wanajeshi wake wanakufa njaa alafu hapohapo akawa na mategemeo watapigana kishujaa washinde vita!??
Nikakuuliza ni wapi US pamoja na kuvamia nchi lukuki umeshawahi kusikia anatoa msaada wakati vita vikiendelea!?
Kutoa misaada anatoa sana lkn baada ya kumalizika vita. Ashapata kufikia malengo yake kama ni serikali ashaiweka anayoitaka ndipo sasa anakuja kutoa misaada. Lkn atoe misaada wakati wa mapambano tena hata hajafikia malengo sidhani, kama amewahi kufanya hivyo utuoneshe hapa kama ambavyo sisi Pro russia tumeweka picha na video za misaada ya urusi huko ukr!
Badala ya kujibu hoja ulizoadressiwa umekuja na tantarira nyingiii mara Ooh Russia hayupo kwenye kutoa misaada, Mara chanjo mara sijui nini hoja haikuwa huko wacha kujitoa ufahamu!
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app