Sijaona taarifa kwamba NATO wameweka silaha za kinyuklia Poland. Hazihitajiki.
Roketi kwenye nyambizi za Marekani na Uingereza ni aina ya Trident II zinafikia shabaha hadi umbali wa kilomita 11,000.
Zinaweza kufika Moscow hata kutoka Madagaska au karibu na Zanzibar bila matatizo. (Hakuna anayetaka kutumia silaha hizo, maana kila upande unazo na mara wanaanza kuzitumia, ni mwisho wa Urusi, mwisho wa Marekani, mwisho wa nchi nyingine - ningehisi pia mwisho wa Tanzania unawezekana maana sioni jinsi gani serikali yoyote itadumu kiasi cha uharibifu na njaa ambacho kingetokea hadi sehemu zetu za Afrika).