Mpendwa, kwa bahati mbaya huna habari, unajadili jambo ambalo hulielewi.
Tangu miaka ya 1950 majeshi ya Marekani na Urusi walipanga wanfanye nini wakipata taarifa kwamba upande mwingine unarush makombora mengi yanayoelekea kwao. Yote yameandaliwa (na kila upande unaijua na hapa sababu kuu kwamba hadi sasa hatujaona vita ya moja kwa moja kati ya Marekani na Urusi - hali hii ina inatwa "mutually assured destruction").
Mipango ni hii: wakati kituo kikuu upande moja inaona kupitia satelaiti zake kwamba makombora mengi yanarushwa katika vituo vya nchi nyingine (vituo vinajulikana, vinatazamiwa mfululizo kila siku kwa satelaiti) amri inapelekwa kwa vituo vya wenyewe kuandaa kila kitu kwa kurusha.
Kuna kipindi kifupi cha dakika chache (maana roketi itakuwa hewani takriban dakika 20-30) kupiga simu na kuuliza: je tunaona roketi zenu, mnatushambulia kweli?).
Baadaye mpango ni hata kama roketi za adui ziko njiani na zitaharibu upande wetu, sisi bado tunaweza kurusha roketi zetu zitakazofika upande mwingine kidogo baadaye.
na hata kama vituo vingi vya roketi upande mmoja vinaharibika tayari, bado kuna nyambizi baharini zitakazorusha roketi tzake kidogo baadaye. Silaha za nyambizi za marekani zinatisha kuangamiza miji yote ya Urusi, hata kama Marekani imekufa tayari.
Hivyi ndivyo ilivyoandaliwa tangu miaka zaidi ya 50 kila upande, na mara kwa mara wanafanya mazoezi wawe tayari.