Kama ukiisoma saikolojia ya Zelensky utaona kabisa vita hii inamuumiza na anatamani iishe, mara nyingi ameongea kwenye vyombo vya habari kwa hisia kubwa kua anataka kukutana na Putin wayamalize. Zelensky anapita kipindi kigumu sana.
Lakini ukweli mchungu Zelensky hana sauti, kuna watu wanamwambia cha kufanya, watu wanamuamulia cha kuzungumza. Wanampa platforms kubwa ya kuzungumza na mataifa ya west, mpaka sasa kahutubia Italy, Uk, USA, Japan na Germany. Lakini nini kimebadilika?
Leo Nato wamekutana tena, na wamesisitiza hawaweki 'No fly zone ' au kuingiza 'peace keepers' mpaka hapa Zelensky alitakiwa kua macho.
Muda ni mwalimu, tuone wananchi wa Ukraine watavumilia hili mpaka lini, maana wanaona jinsi majeshi ya Russia wanavyo watreat mitaani soon or later watajua ukweli.
Propaganda za media ni kubwa, kama ukisikiliza vyombo vyao ni dhahiri kua wanashinda vita, ni dhahiri adui hana nguvu, hana chakula, wala hana vifaa vita. Propaganda hizi zimekuja hadi huku Africa, wengine wanasema mbona mpaka leo Russia hajaiteka kiev?
Malengo ya mvamizi yalikua matatu, moja 'Demilitarization' pili Kuondoa uwezekano wa Ukraine kuingia Nato, tatu kukubali kuachia majimbo matatu ambayo ni Donetsk,luhansk na cremea. Sasa tujiulize nini ambacho Russia kashindwa?