Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Chernobyl hakuwa mlipuko , ilikuwa moto tu. Wakati wa milipuko vumbi hurushwa juu zaidi hadi kimo ambako upepo unazunguka dunia yetu. Hivyo viwango vya mnururisho vitaongezeka sehemu nyingi za Dunia, hata maeneo ya mbali kabisa. (hii tunajuakwa hakika maana kuna maarifa jinsi gani vumbi inasambaa kote duniani baada ya milipuko ya volkeno).
Maana yake magonjwa ya kansa yangeongezeka hata kilomita elfu kadhaa kutoka mahali pa milipuko.

Kwanza hongera kwa kujitahidi kuelezea vyema ktk kujenga hoja yako.

Pili, natamani siku moja Nyamizi aweze kuandika vitu vya maana mfano wa hivyo (watu wakapata walau kitu cha kujifunza kwake).

Tatu, natofautiana na 'sehemu' ya maelezo yako ktk ukubwa na kuenea kwa viwango vya mnururisho kwenye tabaka la hewa (atmosphere) ktk mifano uliyotoa. Suala la kusema kwa kujumuisha (generalization) kuwa bomb la nyuklia likilipuliwa huko Marekani/Poland basi athari za mionzi ktk tabakahewa zitakuwa kubwa kuliko zile zilizosababishwa na mlipuko wa Chernobyl wa mwaka 1986, sikubaliani na hoja hiyo.

Athari za mionzi zilizosababishwa na mlipuko wa Chernobyl 1986, zinaelezwa kuwa zilikuwa ni zaidi ya mara 400 ya bomb la nyuklia lililolipuliwa Hiroshima. Kwa hiyo hiyo hoja ya kujumisha kwa kukata inakosa mashiko.

Bali inakadiriwa kuwa kiwango cha mionzi kilichosababishwa na mlipuko wa Chernobyl 1986, ni sawa na kulipua dazeni ya mabomu ya nyuklia (12 atomic bombs).

Bado sijaona sababu ya kusema tutaathirika 'moja kwa moja' na minururisho ya mabomu kadhaa ya nyuklia kama Russia akiamua kuichapa nyuklia Marekani au Poland.

Btw: Athari za mionzi ktk tabaka hewa zilizosababishwa na mlipuko wa Chernobyl wala hazikufika Afrika ya mashariki.

Screenshot_20220324-183901_Chrome.jpg

Screenshot_20220324-190521_Chrome.jpg
 
Poland wametuma vifaa vya vita Ukraine
USA wametuma vifaa vya vita Ukraine
NATO kwa ujumla wao.

Hapo bado na Missionaries na Jeshi na vifaa alivyonavyo Ukraine, lakini moto ameupata na watu wamesogea vizuri.

Hili ni Pigo la Pacific, Russia kapiga na kuchakaza Wote na bado wanaangaika kuanza kuongeza budget za Military na Security zao.

Russia hapo kapigana na USA,Ukraine, British, Germany, Poland afu unakuja kusema Russia sio kitu, Hata kama Asipo shinda, Ila amewatoa jasho kweli kweli, Vikao haviishi, sanctions haziishi.
 
marekani na nato walipigana vita na talban zaid ya miaka na wakapigika kingese

Nayo marekani tuiweke wapi kwenye medani za kivita ?
Mimi nazungumzia Russia na uwezo mdogo iliyoonyesha kwenye hii vita,Marekani itafutie nafasi yoyote unayoona inafaa
 
Sorry kwa sababu unataka kujifunza.
1. Kuweza kabisa unatakiwa ujue missile maana yake.
2. Unatakiwa ujue maana ya warhead.

Baada ya kujifunza hayo utakuja uelewe kwamba missile huwa inabeba warhead. Warheads zinaweza kuwa ni za mlipuko wa kawaida au nuclear.
Sasa avangard ni missile speed yake ni hypersonic. Yaani zaid mara 10 ya speed ya sauti. Au unaweza ukasema 10 mach.

Sasa avangard haiwezi kuwa treced na radar yoyote kutokana na speed yake.
Vilevile avangard inaweza kubeba nuclear warhead.
Kwa kifupi tu ni hivyo.
Mpendwa, unachanganya mambo tena. Rada inapima kwa kasi ya nuru hivyo kasi ya 10 mach si changamoto kwa rada.
Changamoto iko kwa mitambo ya kuzuia roketi (inayoongozwa na rada). Maana muda hautoshi kwa mitambo iliyopo siku hizi kutambua roketi ya aina hii na kulenga na kurusha roketi ya kinga inayoiharibu hewani.

Bila shaka wataendelea kubuni kitu cha kuizuia. Labda leza? Tuone.
Hadi sasa kila silaha iliyotangazwa ni ya mwisho imepata dawa lake.
 
Endapo urusi atafanikiwa kuuza gesi yake ulaya kwa ruble na saudia akafanikiwa kuuza mafuta yake kwa yuan ni hatari sana kwa usd na kwa america kwa ujumla.

Tuone muda utasemaje. Hizi mambo naona km wakubwa wanacheza chess vile. Kila move naiona kama 'Kete' zinazosukumwa kwa ustadi mkubwa na uangalifu. Putin akifanya move moja anasubiria kuona watareact vipi wakati huo kichwani anazo option kadhaa kama wakimove hivi atareact hivi taabu ni pale wanapomove vile asivyotarajia. US&Co Pia. Wakati wowote game inabadilika aliyekuwa anashinda anapoteza au vice versa. Kosa kidogo unaadhibiwa.

US/NATO vs RUSSIA mwisho wa siku lazima mmoja asande. Haina droo hii game

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Asante...nami nawazia hivyo
 
Endelea ku kopi mkuu....google ipo.
Ila siku si nyingi tutarudia hii page.
Pia ukisoma mtu anamtaja mwinginge kuwa mjinga, kwenye majadilianao kama haya,..mtu huyo ni hovyo sanaaaaa.
Bado wadhihirisha ujinga wako, ulivamia mazungumzo ya mie na Mwanamkiwi kwa kukurupuka, sie tunajua tunachokijadili na twaendelea kujadili nae...siku nyingine ukiona watu wanajadiliana, soma kwanza na uelewe points wanazojadili, kisha ndio uchangie.

Btw: Ujinga ni hali ya kutojua kitu fulani. Hukujua point ya msingi tuliyokuwa twajadili na huyo jamaa yangu.
 
kama ikitokea vita vya nuclear marekani itageuzwa majivu ndani dakika tano nusu kuna mnyama anaitwa sarmata hili ni kombora hatari

urusi wanayo tech ya kuzuia mashambuliz ya nyuklia marekani ya kwao ili feli hata thaad air defense system zilifeli kuyatungu makombora ya north korea pale japan
R-36 Sarmat hizi ambazo zilitengenezwa Ukraine na alishagoma muda sana kuzipa spare parts ndio Russia anaringia. Si ajabu ziko kwenye silos uko na maintenance inasuasua
 
Mother of All Bombs (MOAB) the biggest non-nuclear bomb ever dropped in the world View attachment 2163155
Sijui watu wengi wanaoamini vita ya kinyuklia inaweza kuwa ndogo. Najua wanajadiliana namna yake, ila naona wengi wanakubali hatari ni kubwa mno haiwezi kubanwa mara imeanza.
Kwa hiyo jambo la kuangalia ni vita kubwa, si mabomu 10-20 bali mamia , mabomu yaliyoandaliwa na maelfu.

Tofauti na Chernobyl ni ukali wa moto na milipuko; Kwa hiyo matumizi ya silaha nyingi za nyuklia zitafikisha vumbi na mnururisho hadi tabakastrato na hivyo kuzunguka dunia yote. Hali hii tumeshaona kila baada ya miaka kadhaa baada ya milipuko ya volkeno kubwa, mara vumbi imerushwa zaidi ya km 20 iananza kuzunguka dunia yote.

(Hiroshima haifai tena kama kipimo cha kulinganisha; maana nguvu yake ilikuwa kama 13,000 tani za baruti ya TNT =13 KT. Huu nu ukali wa kombora moja linaloweza kufyatuliwa leo kwa mzinga mmoja - artillery si roketi;
 
❗️🇧🇪 Belgium is not supporting full rejection of Russian oil and gas in the EU, Prime Minister Alexander De Croo says.

🔎 Regarding Moscow’s demand to pay for gas in rubles, the prime minister claims that this means prices can also "be reviewed."
 
Back
Top Bottom