Assessment niliyofanya mpaka sasa kwa Russian landing forces, their military gears, troops, tectics nakuhakikishia Russia hana uwezo wa kuvamia Marekani. Labda hiyo Marekani uwe unaisema iliyochorwa kwenye kikaratasi chumbani kwako umeiweka uvunguni mwa kitanda. Poland tu the way walivyo wanaweza mount resistance kwa invading Russian forces. Uturuki hii pekee inaweza zuia landing kama iliyofanyika leo.
Silaha kubwa zilizotumika leo: ukituma Mi-8s na Ka-52s unakutana na MANPADS na short range air defence systems, ukituma tanks ardhini unakutana na Uturuki au Poland wanazo German made Leopard 2 na ATM za kutosha. Ukija na Sukhoi na MiG haziko stealth hata bila ground radar Poland wakinyanyua AWACS mbili tu angani zinatoa mwongozo wa fighters zao kushambulia adui akiingia anga lao. Russia ikitumia artillery, self propelled howitzers na MRLS kama Smerch, Uragan hao members wa NATO karibia wote huwa wana counter battery radars. Kitu pekee ambacho Russia ana edge ni missiles hizo Kalibr zilizotumwa kama 160 hivi. Russian navy ilikuwa na meli zaidi ya 12 baharini na imeteka mji wa Maliupol na navy base ya Ukraine. Meli zinaleta shida kiasi, hakuna ASM za range kubwa ila landing crafts zitazuilika. Kuna nchi kibao hapo zinaweza hold more than a month zikivamiwa na Russia.
Ukraine sio level za Urusi na haina silaha za kutosha, wala sioni kama ina mobilization ya maana, kwanza jeshi ni 160,000 hivi ukiongeza na reserve wasiofika milioni moja. Hata hivyo Ukraine imefanya counter attack mida ya jioni, imepeleka mashambulizi kujaribu kuzuia airports za karibia na mji mkuu kutekwa. Naamini wakishindwa wataweka craters kwenye runways ili ndege za Urusi zisitue hapo.
Siwezi ilinganisha Russian na Marekani, ikitokea vita kati yao doctrine zao zinaonesha kabisa kwamba Russia atakuwa na defensive position na US atakuwa na offensive position. Hatotokea mwanajeshi yeyote wa Urusi aingie ardhi ya Marekani. Kwa mfano atapita wapi na kwa kutumia nini?
Kuhusu nuclear capabilities achana na idadi ya warheads sema nuclear delivery systems, preemptive strike capability na response. Hawazidiani sana idadi ya makombora na hawahitaji kutumia hata robo yake kumaliza vita.
Vita ya Russia vs USA haipo. NATO vs Russia haipo zitakuwepo operations za kuunga mkono au kumpinga third party