LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Chanzo ni Ukraine kukubali kujiunga na NATO lakini sio hilo tu kingine ni kukubali marekani na NATO kuingiza silaha zao ndani ya nchi ya Ukraine

Kama unavyojua Russia na Ukraine ni majirani na hawezi kukubali kuona silaha za maadui zake NATO na marekani zinakuja karibu
Huko ni kuhatarisha usalama wake
So anajilinda ndio maana anamwambia Ukraine ajiondoe NATO na asiruhusu silaha kuingia Ukraine.

Kingine ni watu wenye asili ya urusi wa majimbo ya Donetsk na luhanski waliopo ndani ya Ukraine wanaotaka kujitenga na Ukraine na kujiunga na Russia
 
Jamani shule mnaenda kusoma nini?,hata ukuze uchumi ufikia mahala kila raia anatembelea VXR mwisho wa siku utautumia Uchumi wako katika ugunduzi wa mambo mablimbali na mwisho kabisa ni ugunduzi wa silaa za kujilinda au utanunua hii ni vicious cycle brother.
Utajenga uchumi utajengeka but at the maendeleo hayo hayo yatakupelekea kwenye destruction na IPO siku utaanza mmoja.
Kwa hiyo huyo russia keshakuza uchumi wake kiasi ambacho ilichobakia ni ugunduzi wa silaa tu 😱 za kujilinda? tu hana tena haja ya kuendelea kukuza uchumi kwa kuwa huko alishamaliza 🤣😂😆 halafu wewe ndo unajiona umeenda shule mwenyewe tena unajiita Econometrician
 
Russia hadi sasa siku ya 3 hajawa na clear dominance over Ukraine airspace.Kuna Ukranian pilot warusi wanamuita "The Ghost of Kyiv"hadi sasa ameshadungua jets 4 za Russia kwenye dogfight..
Unaweza ku google "the ghost of Kyiv"utaona habari zake.
Na ndege ziliongaangushwa ni Su-35 planes, two Su-25 planes, a Su-27 plane and a МіG-29.

Urusi ndio maana anajitahidi sana asikutane na NATO, maana hadi sasa kashatumia 1/3 ya Jeshi lake
 
Wakati dunia imetulia lile lifedhuli libaba la kina KABUDi,ndugai,Polepole,gwajima Boya,msukuma,Sabaya,bashiru ,makonda Nk lilitutesa na vita ya kusadikika ya kiuchumi kumbe yanatuibia tu yenyewe
 
Kwa mtu yeyote anaeweza kunisaidia nn chanzo cha vita inayoendelea kati ya Ukraine na Russia, chimbuko lake hasa limeanzia wapi?

Tuseme chanzo ni Marekani na washirika wake kutaka kuweka silaha zao za Nuke Ukraine kwa kupitia mgongo wa Ukraine kujiunga na NATO.

Mkataba wa Minsk uliosainiwa sijui miaka mingapi iliweka wazi kwamba NATO haitaendelea kujitanua kuelekea upande wa Urusi hivyo kitendo cha NATO kutaka kupokea Ukraine ni kuvunja mkataba huo.

Hii ndiyo maana Putin amezionya Finland na Sweden nao wakijifanya kutaka kujiunga na NATO watapigwa vibaya.
 
Marekani wajanja hawata weka combat troops, urusi ata pata madhara ya kiuchumi makubw sana

Mrussi kajipanga na hakuna anaemtisha unafikiri hajui hivyo??? Zama za marekani soon zinapotea coz hata kiuchumi marekani kashaachwa na china muda sana sema data hazitoki sahihi.

Ukija kiuchumi russia anamilikia 75% ya mafuta na gas kwa Europe na nchi ya 2 kwa uzalishaji mafuta duniani akizuia na yeye unategemea nini?? Bei ya mafuta tayari imeshapanda. Lazima warudi mezani na mrussi ametengeneza uchumi wa kujitegemea hakuna wa kumtisha kwa sasa anajua nini anafanya sisi tusubir mwisho
 
Kwahiyo kwasasa Nchi ndogo ya Ukraine inapambana na nchi 3;

1.Urusi
2.Belarus
3.Chechnya.

Hii ni Aibu kubwa Sana. Ukraine kumbe Wanajeshi imara kweli kweli.
Unashangaa hayo, mbona hushangai Israel akisaidiwa na mmarekani wamegonga mwamba kwa palestrina
 
Back
Top Bottom