LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mrusi kachokoza nyuki kumbe Raisi wa Ukraine ni myahudi ,wayahudi wa Ukraine wasema lengo la Putin ni kufuta wayahudi walioko Ukraine na kumwondoa Raisi wao myahudi

Nimesikiliza CNN jamii ya wayahudi wa Ukraine wanasema Putin ni Hitler wa pili
Kapiga mabomu hadi.memorial yao Ukraine ambako eneo hilo la Ukraine Hitler aliua wayahudi mamilioni kwa lengo la kuwafutilia mbali

Sasa Putin kaanza kuwalenga wao na majengo yao wanayoishi
mbona asilimia kubwa ya mashmbulizi ya anga yanayofnywa na urusi nchini ukraine wanashambulia makazi ya watu
 
Kuichuku nchi nzima sio kitu rahisi kwa Strategy Anayoitumia Putin ya kubembeleza, Na ndio inampa hasara sana.

Uwepo wa watu katika battlefield Imekuwa advantage kubwa Sana kwa Ukraine, kutumia kama kinga kwao, Na kuwapa ugumu Russia kutupa mabovu kwa kunyatanyata.

Nazani wangesema raia wote wametoka, Nchi ingebaki tambalale.

Map of the progress of the special operation for March 3

View attachment 2138152
Baada ya hii ramani ni wazi Ukraine huko mbele itakuwa kama Berlin West na East ni wazi wanaigawa nchi vipande viwili hizo ndio buffer zone ndio maana kwenye hii ramani wanakuja taratibu kutoka east na kuifanya Ukraine landlock bahari wanaichukuwa Russia. Msije kushangaa hata wakubwa ni sehemu ya hii game.
 
Unadhani ni wewe peke yako una masikio ya kusikia na macho ya kuona na kusoma? Zile blah blah zilikuwa za nini za Kyiv inageuka majivu kama mlikuwa manyajua yote haya? Mlipokuwa mnaambiwa mwanzoni mwa hii vita mlikuwa mnabwata hapa kwa majigambo mengi,leo hi mmeona ugumu wake mnaanza kutuletea hizi sababu utadhani sisi hatuzisomi kwenye propaganda media za Russia.

#kyivmajivubadotu

Hivi wewe unasikiliza wabongo au russia? Kuna sehem russia imetamka kuwa ukraine itakua majivu? Unajua plan zao kwa ukraine ni nini?
 
Sio imebidi ucheke tuambie tangia mmeanzisha uvamizi wenu kule Ukrain jeshi lenu la anga limefanya maajabu yapi mpaka sasa maajabu ya maana na sio kubomoa bomoa majengo tu ya Raia apana jeshi lenu la anga limefabya nini cha maana kwenye hii vita yenu mpaka sasa
Unabisha ujinga kweli ndugu, ufahamu na uelewa wako wa mambo no mdogo sana. Russia amewaona Ukraine kama ndugu kabisa wa damu ambao wame-share historia muhimu sana hivyo wamepeleka silaha zile hafifu sana na mpaka sasa haijatumika silaha vimetumika vijisilaha vya enzi za soviet. Ungetaka kujua Russia ni nini NATO angepeleka jeshi.

Mwanzoni eti NATO wakiongozwa na Ujerumani walikuwa wanatoa kauli za vitisho Putin aliposema tu usalama wa Russia upo shakani na kuviagiza vikosi vyote vikae tayari umeona kuna harakati zozote Poland ,umeona kuna kauli imetolewa tena.
 
Yaani ana mashaka Sana Yule Raisi...huyu anampiga akapambane na makambale wenzie huyu Ni kumstress tu
Pamoja na kuwa ni mdogo lakini anatumia akili zaidi na kaonyesha upinzani mkubwa tu kuliko adui anaepambana nae,Ukraine inazidiwa kwa kila kitu na Russia ndiyo maana wengi waliamini kabisa hii vita wenyewe humu wanaiita special operatiosn ingekwisha ndani ya msaa 24 tu,Lakini kinachoendelea tumeona hadi Mkubwa alipanic akataka atumie hadi Mabomu ya Nyuklia utadhani yeye angebakia salama kama angeyatumia.
 
Hivi wewe unasikiliza wabongo au russia? Kuna sehem russia imetamka kuwa ukraine itakua majivu? Unajua plan zao kwa ukraine ni nini?
hebu tuambie plan za Russia kuvamia ukraine zaidi ya hizi
  • kutambuliwa kwa jimbo la crimea kama sehem ya urusi ili jamaa akachimbe mafuta kwa uhuru zaidi
  • ukraine kutojiunga na umoja wa NATO
kuna hoja nyingine zaidi ya hizo kutoka kwa Putin?
 
Unataka twende RT aka TBC ya Russia as if ni chombo huru, halafu unataka tukaamini propaganda zake.
Hebu nitajie chombo sasa hivi ambacho sio kama TBC? CNN zamani bwana siku hizi kama TBC wana agenda zao na leo nimeamini Trump kuwaita fake news na ni kweli wakati wa Trump walimuandamana utasema hana zuri hata moja. Vyombo vyote fake news basi tu hatuna mbadala. Hao BBC zamani unasema afadhali lakini hakuna kitu. Habari za wa africa tu kunyanyaswa mpakani CNN kama hawajaiona hiyo habari wameipotezea juu kwa juu. Aljazeera ndio mara nying walionesha ile habari
 
Uwezo wa Putin umedhihirika ni mdg sana kiakili.wacha watu wamsaidie ku think
.Kifupi ni kubwa jinga

Hivi unajua chanzo cha vita ya russia v ukraine? Hivi unafikir russia ni mwonevu kama NATO? Anasababu zake za ndomana yuko pale, kwanza yeye kasema ni millitary operation na sio vita.
 
Unabisha ujinga kweli ndugu, ufahamu na uelewa wako wa mambo no mdogo sana. Russia amewaona Ukraine kama ndugu kabisa wa damu ambao wame-share historia muhimu sana hivyo wamepeleka silaha zile hafifu sana na mpaka sasa haijatumika silaha vimetumika vijisilaha vya enzi za soviet. Ungetaka kujua Russia ni nini NATO angepeleka jeshi.

Mwanzoni eti NATO wakiongozwa na Ujerumani walikuwa wanatoa kauli za vitisho Putin aliposema tu usalama wa Russia upo shakani na kuviagiza vikosi vyote vikae tayari umeona kuna harakati zozote Poland ,umeona kuna kauli imetolewa tena.
Kwani ukraine ni sehemu ya umoja wa NATO hadi NATO apeleke jeshi?
 
Hata askari ni watu.
Kumbuka raia wamepewa silaha kuwaua Warusia.
Mtu anayetaka kukuua ni adui hata akijificha kwenye makazi ya raia.
Piga tu bila kuangalia

Go Putin Gooooooo on

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
Hao sio wanataka Kuua warusi wanajilinda kutokana na mrusi kuwavamia

Mrusi akirudi nchini kwake wao hawana shida naye sasa mtu akuvamie kwako nikibeba panga useme nakuonea

Kwa hiyo nikae nyumbani kwamgu bila silaha nikuache tu unitwange nyumbani kwangu
 
Na wewe ni zoba kabisa, huwezi ongelea vita ya Ukraine na russia bila kuitaja marekani, kaa kimya uonekane mwerevu epuka kujidhalilisha kama hujui kitu.
Unajiona na wewe umetoa hoja,ona hata huwezi kuandika majina ya Nchi kwa usahihi,kajifunze kwanza basics za kuandika ndiyo urudi hapa kubwabwaja,Mrusi wa mwendakulima usiyejua hata kuandika neno Russia kwa usahihi. Achia Warusi wa Kinondoni Moscow kina Frustration wajanja ndiyo waongee hapa 😂
 
Ila kwa haya maamuzi yake wewe kwa mtazamo wako huoni Kama keshaivuruga Russia, after war impact kiuchumi mbona Kama zinaenda kuwa mbaya Sana,au unaonaje Hapo?

Hzo ni mbwembwe tu vikwazo vitalegezwa sisi tupo suala ni muda tu. Unafikiri russia hakujua hivo? Hata kabla ya vita kuanza walimwambia watampa vikwazo lakini si kaingia ukraine? Russia anajua nini anafanya sisi wabongo tunashabikia yasiyotuhusu ila ukweli jamaa hayumbishwi na watu wa magharibi anajua nini anafanya.

Putin ndo mwamba kwa sasa
 
Pamoja na kuwa ni mdogo lakini anatumia akili zaidi na kaonyesha upinzani mkubwa tu kuliko adui anaepambana nae,Ukraine inazidiwa kwa kila kitu na Russia ndiyo maana wengi waliamini kabisa hii vita wenyewe humu wanaiita special operatiosn ingekwisha ndani ya msaa 24 tu,Lakini kinachoendelea tumeona hadi Mkubwa alipanic akataka atumie hadi Mabomu ya Nyuklia utadhani yeye angebakia salama kama angeyatumia.
Hahahaha...unajikaza kisabuni bibie huku ukijua fikra kabisa Russia katawanya kikundi haramu Ukraine kimya kimya bila bugudha kwa Raia angeamua kuchafua hali ya hewa sasa tungekua tunazungumzia vifo Vinci sana.
 
Kwani ukraine ni sehemu ya umoja wa NATO hadi NATO apeleke jeshi?
Uganda haikuwa sehemu ya Tanzania lakini tulipeleka jeshi

Nchi zote kusini mwa Afrika ,Congo Dafur ,Comoro nk sio sehemu ya Tanzania lakini tulipeleka majeshi
 
Unajiona na wewe umetoa hoja,ona hata huwezi kuandika majina ya Nchi kwa usahihi,kajifunze kwanza basics za kuandika ndiyo urudi hapa kubwabwaja,Mrusi wa mwendakulima usiyejua hata kuandika neno Russia kwa usahihi. Achia Warusi wa Kinondoni Moscow kina Frustration wajanja ndiyo waongee hapa 😂
Wewe ndio unajiona una utashi mkubwa wa kuandika? Ni wapi umewahi kuona sentensi na sentensi zinatenganishwa na koma ? Umeshindwa kwa hoja naona unataka kuleta ' personal attack'
 
Back
Top Bottom