Humu katika vita hii nimejifunza mengi sana
1. Vita si lelemama vita ni moyo bila moyo Ukraine ingeshasarenda toka siku ya nne au ya tatu ya hii vita. Msaada wa washirika wake lazima upewe umuhimu wake katika hili. Lakini pia niwapongeze Vijana wa Ukraine' Kwa kupigana kizalendo na moja ya jeshi kubwa na teknolojia za hali ya juu zaidi duniani!
2.Silaha za Kimagharibi ni silaha za kawaida ambazo HAZINA ubora tuliohadithiwa na BBC, madhali HIMARS, F16, TIGER TANK, ABRAMS, LEOPARD, nk zimefeli na kuteketea vibaya, Sina budi kusema kwamba Russian weapons t72, t90 , bm grad Su 34, su 25 zimefanya vyema Kwa kiasi kikubwa sana!
,3. Lazima mataifa yetu yawekeze katika teknolojia za drone, Drones zimeharibu kabisa mifumo mbalimbali ya kimapigano ya section, platoon nk.
4. Vita imeibua mataifa madogo kuonesha ufundi wao katika kutengeneza zana, aghalabu si ajabu zilizikika kelele za uwepo wa Silaha za Kiran na Korea zinazozidi kuonesha performance ya hali ya juu.
4. Russia Ina uchumi mzuri usiyoyumbishwa ovyoovyo na vikwazo, Putin vita ikiisha ni vyema akakaa na wachumi wake na kuwapongeza sana!
5. Vita imeharibu sana uhusiano wa kiuchumi na Russia, vikwazo vingi vimeifanya na kuifanya Russia kutumia muda mwingi kurecover hali hii iliyojitokeza.
Ongezea vingine ulivyojifunza Kwa mtuzamo wako