SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

Speedaf wanazingua kwenye delivery..yani Ukisema usubiri wakuletee lazima ukutane na usumbufu...mimi huwa nikiona mzigo umefika mfano leo....kesho nawaibukia ofisini kwao nakamata mzigo wangu nasepa

Nimekuwa nikifanya hivyo hadi nishazoeleka pale ofisini kwao
 
nitafatilia upande wa courier , nikiona mizunguko ni mingi na inakula mda, nakausha nahesabia hasara, siwezi msumbua seller kudai refund najua hahusiki hapa
Kwahiyo seller waendelee kutuma mizigo huku ili kuneemesha watu wengine?

Out of Topic, umewahi kutapeliwa kitu ambacho ni cha thamani na cha muhimu kwako?
 
Habari wakuu. Na mimi napenda kuungana na nyie katika kutoa mtazamo wangu kwa hawa speedaf.
Ninachowapongeza na kuwasifu ni kitu kimoja ambacho ni kwamba wapo faster sana katika kusafirisha mizigo. Niliagiza percel flani hivi ambayo ni memory card 1T aliexpress na nilchagua aliexpress standard shipping kama kawaida. Baada ya kupata tracking number niliunganishwa moja kwa moja katika web page ya speedaf ili nitrack parcel.
Baada ya siku kumi tu mzigo ulikuwa umeshafika Tanzania. Ilikuwa haraka mno kulingana na matarajio yangu ambapo nilitegemea baada ya wiki mbili.
Baada ya mzigo kufika nilitumiwa meseji ambayo ni;
" Habari fika Picha ya ndege karibu na river road bar kuchukua mzgo wako wa Ali Express Muda kuanzia sasa mwisho ni Saa 10 jioni asante!"
Mimi nilizoea kupata mizigo yangu posta ya Chalinze Pwani kwa hiyo kwenda picha ya ndege kwangu ilikuwa ni mpya sana hiyo.
Nikaamua niende jana tarehe 20/04/2023 nikaone ni wapi hasa pa kupokelea mizigo yetu.
Nilishangaa sana, maana nilijikuta nipo nyumbani kwa mtu, yaani hata hapaonyeshi kuwa kuna ofisi, ila majirani wanajua kuwa hapo ndipo watu wanapochukulia mizigo yao ya kikuu au aliexpress.
Nilipo muuliza kwa nini sipokei mizigo yangu kupitia posta,alinijibu hata yeye hajui kwa nini.
Hitimisho langu ni kwamba,hawa jamaa hawapo serious kuhusu usalama wa bidhaa kutokana na kwamba hawana ofisi maalumu kwa mawakala wao. Kitendo cha kupokea mzigo katika nyumba ya mtu hakileti afya maana lolote linaweza kutokea na kuhatarisha usalama wa bidhaa. Just imagine ni mzigo wa pesa ndefu alafu sehemu ya kupokelea haileweki. Utaishia kupoteza mali yako na ukapata taabu ya kudai refund. Mapungufu yao ni hapo tu. HAWA JAMAA HAWANA OFISI MAALUMU.
 
Upo sahihi sana,delivery wanafanya kienyeji sana,siku nikienda ofisini kwao nitawaonesha huu uzi


Kila siku nawaambia msisubiri kuletewa,kama upo dar ukiona mzigo umefika tu wewe wahi chap ofisini kwao beba mzigo wako sepa
 
Posta hawana shida mbona

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
Nakiri mwanzo nilikua na waswas na posta ila mzigo ulifika.tena iikua mingi na wamenitumia sms watu wa posta na nimepewa huduma nzuri.kweli shirika la posta limebadilika pale nilikuata mizigo ya watu ipo mingi kweli posta ya kidigtali .hongera shirika la posta
 
Yeah posta wame improve sema ndo sasa hivi wanapata competition from private companies

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Mimi toka mwaka jana sina hamu ya kuagiza
 
Sasa tumuelewe nani mbona wengine wanasema hawana ofisi
 
Uzoefu wa utumiaji speedaf Tanzania kwangu uko tofauti sana na watumiaji wengine...maana mimi kwao nimeshapokea parcel zangu zaidi ya 50 bila tatizo lolote..mizigo yote huwa huwa natrack kupitia app yao na ikifika siku 2 sijaona dalili ya kuletewa nafuata mwenyewe..lakini mingi yule distributor wao bonge anafikisha kwangu bila shida...zaidi ya mizigo 50 sijawahi pata challenge...mzigo wangu ukija kupitia speedaf najisikia raha lakini ukienda posta kwanza charges zinaongezeka wakati speedaf sitoi hata kumi na mzigo naletewa kwenye address.. halafu posta inachelewa sana maana mizigo yao mingi kuna nchi inapitia na kukaa siku kadhaa..hapa navoandika hii text mizigo nimenunua last week kabla ya idd now ipo airport inafanyiwa clearance ....mimi sijaona ubaya wa speedaf hata kidogo...ila posta ndio sitaki hata wasikia.....
 
Safi
 
Ninavyoipenda serikali yetu huwa inasajili hata makampuni ya kitapeli cha msingi walipe kodi ya serikali
 
Wale OCEAN sijui nini lazima wana mkono wao hapo.

Unafhani wanafurahia maendeleo basi?
 
Wakuu mwenye namba ya wakala wa speedaf Bukoba anisaidie, Jamaa keshapokea parcel yangu na amesign kuonesha kwamba tyr nimechukua

Namba aliyoweka haipatikani leo siku ya tatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…