SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

Sure, mzigo unatoka China kwa spidi ya ajabu, siku 7 tu upo Dar, halafu sasa hao speedaf wa bongo ndio wanauchukua na kukaa nao zaidi ya siku 7 hauoni movement yoyote ya mzigo, siku wakikutaarifu kwenda kuchukua wanatuma text tu hawataki kupokea simu, wanaweka location za ajabu ajabu..yaani miyeyusho. Kama wameanza na hili la kusign mizigo ya wateja basi wanazidi kuharibu.
Kwa mara ya kwanza nashangaa mzigo wangu umekuja na speedaf afu nimepokea ofisi za kikuu AliExpress ziko sehemu Moja

Kikweli sijapenda taratibu zao mizigo ipo ovyo ovyo Ni rahisi mzigo potea Sana ,,

Imagine watu tofauti wanaingia ofisini kupiga stori

Bora posta mizigo inakaa ofisini unatumiwa no ya mzigo unaenda na ID yako unapewa control number unalipa Yani Ni safe Sana
 
samahani mkuu naomba nikuulize kama hutojali, mara ya mwisho natumia AliExpress ilikua mwaka septemba nafikiri, hebu nisaidie hao Speedaf wana replace posta au vipi na je AliExpress standard Shipping imekuga au.
AliExpress Mara ya mwsho November nilinunua ka kitu Cha tzs 4500 nikalipa au kuchagua yanwen economic air mail ..nikachukua posta



But mwezi huu nimenunua kitu nikachagua yanwen nakuja kuta unaletwa na cainiao super economy nikamwambia sikuchagua hio akasema yanwen is not available sijui ,, nikauliza Tena akasema yanwen can't ship nikamuuliza inakuja na meli au ndege akajibu ndege nikajibu sawa,


Siku 11 badae mzigo umefika


Nililipa 962tzs usafiri mzigo mdogo tu wa 3000tzs ...nashangaa nimepigiwa simu kienyeji nakuta Ni speedaf
 
Wangu aliship na cainiao super economy ..nimepigiwa umepelekwa office za kikuu AliExpress ..mzigo nimekuta una nembo ya speedaf
soma comment #66 hapo juu
ni vyema ku-chat na seller na kumuuliza juu ya courier atayemtumia, kama ni speedaf, posta, etc
 
Habari wakuu. Na mimi napenda kuungana na nyie katika kutoa mtazamo wangu kwa hawa speedaf.
Ninachowapongeza na kuwasifu ni kitu kimoja ambacho ni kwamba wapo faster sana katika kusafirisha mizigo. Niliagiza percel flani hivi ambayo ni memory card 1T aliexpress na nilchagua aliexpress standard shipping kama kawaida. Baada ya kupata tracking number niliunganishwa moja kwa moja katika web page ya speedaf ili nitrack parcel.
Baada ya siku kumi tu mzigo ulikuwa umeshafika Tanzania. Ilikuwa haraka mno kulingana na matarajio yangu ambapo nilitegemea baada ya wiki mbili.
Baada ya mzigo kufika nilitumiwa meseji ambayo ni;
" Habari fika Picha ya ndege karibu na river road bar kuchukua mzgo wako wa Ali Express Muda kuanzia sasa mwisho ni Saa 10 jioni asante!"
Mimi nilizoea kupata mizigo yangu posta ya Chalinze Pwani kwa hiyo kwenda picha ya ndege kwangu ilikuwa ni mpya sana hiyo.
Nikaamua niende jana tarehe 20/04/2023 nikaone ni wapi hasa pa kupokelea mizigo yetu.
Nilishangaa sana, maana nilijikuta nipo nyumbani kwa mtu, yaani hata hapaonyeshi kuwa kuna ofisi, ila majirani wanajua kuwa hapo ndipo watu wanapochukulia mizigo yao ya kikuu au aliexpress.
Nilipo muuliza kwa nini sipokei mizigo yangu kupitia posta,alinijibu hata yeye hajui kwa nini.
Hitimisho langu ni kwamba,hawa jamaa hawapo serious kuhusu usalama wa bidhaa kutokana na kwamba hawana ofisi maalumu kwa mawakala wao. Kitendo cha kupokea mzigo katika nyumba ya mtu hakileti afya maana lolote linaweza kutokea na kuhatarisha usalama wa bidhaa. Just imagine ni mzigo wa pesa ndefu alafu sehemu ya kupokelea haileweki. Utaishia kupoteza mali yako na ukapata taabu ya kudai refund. Mapungufu yao ni hapo tu. HAWA JAMAA HAWANA OFISI MAALUMU.
Mrejesho kuhusu hio memory card

Me nataka nunua 32Gb kwa 5.5K
 
Wakuu mwenye namba ya wakala wa speedaf Bukoba anisaidie, Jamaa keshapokea parcel yangu na amesign kuonesha kwamba tyr nimechukua

Namba aliyoweka haipatikani leo siku ya tatu
Waki sign inaonesha nn huko AliExpress

Me nimechukua pale inaonesha mzigo tayari upo mkoani kwangu ngoja nione itakuaje
 
Msaada mwenye namba za speedaf hapo dar! Kuna mzigo wangu wanaupiga danadana tu, ulitakiwa kuja mbeya, ukaenda dodoma, umerudi dar... Ni zaidi ya mwezi sasa sijaupata huo mzigo
 
Hello habari wadau wa jukwaa la teknolojia na wanajamiiforum kwa ujumla.
Kutoka na kasi ya maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia si ajabu tena kwa mtu kufanya manunuzi mitandaoni .

Vivyo hivo hata Tanzania kwa sasa idadi ya watu wanaofanya manunuzi hayo imeongezeka maradufu, hasa masoko ya kutoka Uchina(nduguzetu wa damu).

Zimekuepo njia nyingi zitumikazo kusafirisha mizigo kutoka mataifa hayo (Uchina ikiwemo) kwa mda mrefu sasa .Hivi karibu kampuni ya speedaf ilifungua branch Kenya na kua mkombozi huko kwa huduma yao ya door to door delivery lakini uharaka wa mchakato mzima wa kupata mzigo wako toka siku ya manunuzi ulikua ni wa haraka na kuridhisha
Baada ya ujio wao Tanzania tulifurahi sana na kuamini kua nasi sasa tutaendana na kasi ya wenzetu kwani kampuni ile ile imeingia nchini kwetu kutoa huduma zile zile.

La hasha ,vilio vimeanza kusikika kila kona ya nchi yetu .Mizigo inatoka China vizuri, inafika mpka mkoa mhusika ulipo , maagent wanawakabidhi watu wafanye delivery kwa mteja husika ila kimbembe kinaanzia hapa .

1.Mteja hapokei simu ya wito kwa ajili ya kupokea mzigo wake .

2.Ukifuatilia ofisini speedaf unakuta sometimes mzigo ushasaini kua uliiuchukua ilhali haujauchukua wewe mhusika .Meanz agent wa kuleta anajisainia mwenyewe kua kafanya delivery( Kum make zenu tamaa mbaya). Sasa unapoingia kwa seller kudai refund unakuta seller anaevidence inayoonesha kua mzigo umepokelewa na mhusika alieununua.

Sasa kwa hali hii kweli tutafika .Mnafanya huduma nzuri au makampuni mazuri yasije nchini kwa tamaa ndogo ndogo kabisa .

WADAU KAMA SPEEDAF HAWALETI MAREKEBISHO HARAKA,tuanzeni napema kampeni ya kufosi seller kutokutumia hawa speedaf kwani ni hasara kubwa mno tuipatayo wote mnunuzi na muuzaji. Hapa chini naweka ushahidi wa item nisioipokea ila agent uchawara kasign kua umefika na kapita nao kaenda kuhonga kwa demu wake manina
View attachment 2434527View attachment 2434883
What's the speedaf phone number. I need it please.
 
Ni kwel mzigo nimepata.sema nimejifunza kitu.siku nyingine nikiona sio ali express standard shipping ambao ndio hao spedaf siagiz.mambo ya kupitia posta siyaamin. Sisi tunajijua.kule kupotea /kuibiwani rahis sana
kwani hao aliexpress standard shipping wakikutumia mzigo wewe huwa unapokelea office zipi??
 
Speedaf wanazingua kwenye delivery..yani Ukisema usubiri wakuletee lazima ukutane na usumbufu...mimi huwa nikiona mzigo umefika mfano leo....kesho nawaibukia ofisini kwao nakamata mzigo wangu nasepa

Nimekuwa nikifanya hivyo hadi nishazoeleka pale ofisini kwao
upo mkoa gani??


mimi nipo moshi na huwa napigiwa Simu kwa wakati.
 
Back
Top Bottom