Speedaf ni wapuuzi sana, niliagiza kioo cha redmi note 10 5g ndani ya siku 4 kilikuwa tz. Kesho yake tracking ikasoma Dodoma, baada ya siku 3 agent akawa amesign kuderivery mzigo. Kama siku 4 mbele mzigo ukawa signed na agent na namba yake ya simu ikaonekana. AliExpress wakanitumia delivery note ya mzigo kuwa nimeupokea wakati sijauona, nikaenda posta kuangalia kama ulifikia kwao nao hawakuuona.
Ile namba niliipigia zaidi ya wiki na haipatikani, nikawasiliana na muuzaji akanitumia namba ya makao makuu Tanzania ile namba hata haipokelewi.
Wakati nimekata tamaa nikaijaribu kuipigia ikapokelewa nikamuuliza kuhusu kupokea mzigo wangu akanielekeza niufuate nyumbani kwake na ni nje kidogo ya mji. Kiukweli alinikera huyo jamaa na hapo nyumbani kwake alikuwa na mizigo mingi ya watu wengine.