SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

upo mkoa gani??


mimi nipo moshi na huwa napigiwa Simu kwa wakati.
Nipo Dar mkuu

Ni vizuri kama huwa wanakupigia simu kwa wakati lakini mimi huwa naenda tu direct mwenyewe ofisini kwao

Huwa sipatagi amani ya moyo nijue mzigo ushafika halafu niendelee kusubiri no way

Napenda ile kitu express maana napataga mizigo in 12 days au 13 days ikizidi sana 15 days
 
Watu waongo sana...ofisi zap zipo mbona na watu tunachukua mizigo kila siku
Mkuu yawezekana ulipo kuna ofisi. Mimi Naishi Chalinze Pwani. Nilitumiwa sms na agent wa speedaf nikafuate mzigo wangu kibaha picha ya ndege karibu na bar moja inayoitwa corner bar, nilifika lakini na nilichukua mzigo nyumbani kwa ajent wala sio ofisini. Hawana ofisi huku kibaha wala Chalinze.
Alafu hebu fikiria, Mteja atoke Chalinze mpaka picha ya ndege yaani almost Dar hiyo, walishindwaje kuleta mzigo Chalinze ambapo ndipo anuani yangu ilipo? Mbona kwa njia ya posta sipati usumbufu huo wa kufuata mzigo mbali?
Kweli wapo faster kwenye usafirishaji lakini kwenye delivery hasa sisi tuliopo maeneo ya nje ya Dar wanaupungufu kubwa sana. Wajirekebishe.
 
Kwa sisi tuliopo nje ya Dar tuanaona changamoto za hawa jamaa. Huku hakuna ofisi, ama ukutane na ajent uchochoroni au nyumbani kwake. Kiofisi kwa kampuni kama hiyo haileti afya. Ipo siku watakimbia na mzigo Alafu tushindwe wa kumdai.
Kampuni ndo inakua mkuu tuwape muda wataboresha huduma zao
 
Mi angenikoma haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…