SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

Hata mimi nimepokea mizigo karibu 8 kuanzia November 2022 hadi tar 1 Jan mwaka huu.Niliweka address ya Dar ila baada ya kunipigia nikawaelekeza wailete mkoani na yote nimeipokelea huku.Kuna mingine nimeagiza tar 12 Dec nikaipata tar 1 Jan tena huku mkoani.Ki ujumla wako vizur sana.
 
Umejaza nchi gani? Kama umejaza Tanzania ni sawa

Kuna njia mbili ambazo wanaweza watakutumia either watumie posta au speedaf

Kwahyo wewe track mzigo wako ukifika bongo utaenda kuuchukua kwenye ofisi moja wapo kati ya posta au speedaf
Nimeambiwa speedaf.je ni wap niende mana sitak kuanza kupigiwa
 
2.Ukifuatilia ofisini speedaf unakuta sometimes mzigo ushasaini kua uliiuchukua ilhali haujauchukua wewe mhusika .Meanz agent wa kuleta anajisainia mwenyewe kua kafanya delivery.
Open Disputes kama Mzigo haujakufikia.....
 
Kiuhalisia hawa SPEEDAF kwa suala la speed delivery wapo vizuri, ikiwa wao ndo carrier wanakutumia na email wanakua wanakupa updates...

Tatizo linaanza mzigo ukifika Bongo

1. Hawana Ofisi just incase mwenye mzigo hayupo basi atajua mahali la kuupata (may be wanakwepa kodi).

2. Wanatumia watu wahuni wahuni

3. wanasaini Pacel za wateja (inapunguza usalama wa mizigo), mimi pacel yangu ya kwanza ndo nilisaini, the rest nakuta washasaini wenyewe..sasa wana haraka gani?

4. Unachukua pacel just kwa kutaja jina tu [emoji15] which means ni rahisi kuibiwa mtu akijua umeagiza mzigo.

5. Nimegundua wanawatumia watu walewale wa KIKUU

Nakumbuka pacel yangu ya kwanza kuja na SPEEDAF ilipofika kumbe wakaipaki ofisi za KIKUU, mtu wa kikuu akanitunia txt "kuna mzigo wako ofisi za kikuu fika uuchukue" wala hakufafanua kuwa nfo ule niliagizia aliexpress. Mimi nikapuuzia nikahisi wamejichanganya, halafu huku inaonesha pacel delivered, kwenda posta hamna, ndipo nikapata wazo la kumrudia yule mtu wa KIKUU ndo nikaupata.

Niseme tu kwamba, SPEEDAF boresheni namna ya kufilisha pacel kwa walengwa.
 
nimeagiza item ya $16, 31/12/2022, leo 13/01/2023 nimepokea, wako vizuri

Mkuu sorry mm nmeagiza mzigo ALIEXPRESS tarehe 28/12/2022 hadi leo bado haujafika..hv unapata wapi option ya kuchagua hao jamaa wa SPEEDAF mbona mm naona option ya njia ya ALIEXPRESS STANDARD SHIPPING tu kwangu?
 
Mkuu sorry mm nmeagiza mzigo ALIEXPRESS tarehe 28/12/2022 hadi leo bado haujafika..hv unapata wapi option ya kuchagua hao jamaa wa SPEEDAF mbona mm naona option ya njia ya ALIEXPRESS STANDARD SHIPPING tu kwangu?
speedaf huchagui, ila wao huko ndiyo huchagua,
tracking number unayo ? je ina mfumo wa TZ000XXXX ?
 
speedaf huchagui, ila wao huko ndiyo huchagua,
tracking number unayo ? je ina mfumo wa TZ000XXXX ?

Ninayo ndyo inaanza na RS,tangu January 9 imenasia hapo kwenye depart from transit country
IMG_1568.png
 
Back
Top Bottom