Spika amzuia Mbunge wa Iringa kujadili hoja ya kufutiwa leseni mawakala wa mbolea

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
SPIKA wa Bunge, Tulia Ackson amemzuia Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu aliyeomba mwongozo wa Spika bungeni leo Aprili 18 2023 kutokana na mgogoro mkubwa wa mbolea unaotishia mazao ya wakulima kuungua kwa kukosa mbolea baada ya uamuzi wa Serikali kuwafutia leseni mawakala 721 kutokana na uhuni wanaofanya kwenye mbolea.

Kwanini Spika anazuia wabunge wasijadili matatizo ya wananchi ana manufaa gani na Serikali? amezuia hoja ya CAG watu wamenyamaza, leo anazuia hoja ya matatizo ya mbolea yasijadiliwe ili wakulima mazao yao yafe kwa kukosa mbolea na nchi kuingia kwenye njaa kubwa ili baadae wanufaike watu wachache kwa kuagiza chakula nje ya nchi kutuletea tanzania.

Watanzania wataendelea kuchezewa na Spika hadi lini?
 
Kwani umesahau alipataje nafasi ya kuwa hapo alipo?

Si ni baada ya watu flani kuona matangulizi wake katika nafasi hiyo anaanza kuzua mjadala wa deni la taifa?
Unategemea mtu kama huyo ataruhusu mijadala yenye kuwaweka matatani wasiopenda kukosolewa hata kama mjadala una manufaa kwa taifa.
 
SPIKA wa Bunge, Daktari Tulia kila anapoongoza Bunge anapenda kuwazima wabunge wanaotaka hoja za dharura za matatizo ya wananchi zijadiliwe lakini anakataa mifano michache hii

1. Majuzi Mbunge Ole Sendeka aliomba Bunge liahirishe ratiba zake lijadili kwa dharura suala la ufisadi mkubwa uliotajwa ripoti ya CAG, Spika akakataa

2. Leo Mbunge Bahati wa Mbeya akaomba Bunge lisimame wajadili matukio ya wananchi kuvamiwa na kuuwawa na tembo maeneo mbalimbali nchini, Spika akakataa

3. Leo Mbunge wa Iringa Msambatavangu ameomba Bunge lijadili tatizo la mbolea kwa wakulima ambao mazao yao yanaanza kuharibika kwa kukosa mbolea na mgogoro wa mawakala kufutiwa leseni, Spika amekataa..

Sasa tunajiuiliza hoja za kujadili ushoga na usagaji ziliruhusiwa kujadiliwa bungeni lakini matatizo ya wananchi Spika anawazuia wabunge.​
 
SPIKA wa Bunge, Tulia Ackson amemzuia Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu aliyeomba mwongozo wa Spika bungeni leo Aprili 18 2023 kutokana na mgogoro mkubwa wa mbolea unaotishia mazao ya wakulima kuungua kwa kukosa mbolea baada ya uamuzi wa Serikali kuwafutia leseni mawakala 721 kutokana na uhuni wanaofanya kwenye mbolea.

Kwanini Spika anazuia wabunge wasijadili matatizo ya wananchi ana manufaa gani na Serikali? amezuia hoja ya CAG watu wamenyamaza, leo anazuia hoja ya matatizo ya mbolea yasijadiliwe ili wakulima mazao yao yafe kwa kukosa mbolea na nchi kuingia kwenye njaa kubwa ili baadae wanufaike watu wachache kwa kuagiza chakula nje ya nchi kutuletea tanzania.

Watanzania wataendelea kuchezewa na Spika hadi lini?
Huyo mumewe kashahongwa Cheo cha Ukurugenzi EWURA,anadhani ataongea nini?Mara kadhaa namuona anachekacheka na Born town wa Msoga,unafikiri atafanya uamuzi gani!
Huyo ni Spika wa Mchongo watu wapitishe mambo yao!
 
Kwani umesahau alipataje nafasi ya kuwa hapo alipo?
Si ni baada ya watu flani kuona matangulizi wake katika nafasi hiyo anaanza kuzua mjadala wa deni la taifa?
Unategemea mtu kama huyo ataruhusu mijadala yenye kuwaweka matatani wasiopenda kukosolewa hata kama mjadala una manufaa kwa taifa.
Hizi hadisi za deni la taifa mnazitoa wapi? Kwa nini imwangushika supika?
 
Kwani umesahau alipataje nafasi ya kuwa hapo alipo?
Si ni baada ya watu flani kuona matangulizi wake katika nafasi hiyo anaanza kuzua mjadala wa deni la taifa?
Unategemea mtu kama huyo ataruhusu mijadala yenye kuwaweka matatani wasiopenda kukosolewa hata kama mjadala una manufaa kwa taifa.
Ndugai alikuwa nae anazuia mijadala mingi pia mbona, pamoja na kuzuia bunge kurushwa live
Na wala hakuwa hata na nia ya kui challenge Serikali kuhusu mikopo, aliropoka tu bahati mbaya clip ikasambaa ndio maana akaomba msamaha ambao ulikataliwa
 
Ni kweli lakini hii haiondoi ukweli kuwa Mh.Tulia anaweza kuwa anazuia mijadala muhimu na ya faida kwa taifa.
Two wrongs don't make a right, kwamba Ndugai akikosea na Tulia akosee.
 
Sababu ni moja tuu, bunge lingekuwa liko imara kama alivyowahi kusema Prof Assad lingeweza kumuazimia hata yeye spika kama alivyokuwa anasema mbunge Shabiby (ingawa najua he was joking). Inatakiwa ifike mahala mbunge likiamua linamkomalia kisawa sawa. Tutaendelea sana kumkumbuka spika wa viwango na speed...
 
Ni kweli lakini hii haiondoi ukweli kuwa Mh.Tulia naweza kuwa anazuia mijadala muhimu na ya faida kwa taifa.
Two wrongs don't make a right, kwamba Ndugai akikosea na Tulia akosee.
Nimekujibu hivyo kukumbusha Ndugai alikuwa mbovu, Wewe ulikuwa una imply Ndugai alikuwa Spika bora, wala pointi yangu sio kumtetea Tulia
 
Anatambua fika kilichompata Spika Ndugai, hivyo anatambua nguvu ya chama chake, na nguvu ya mhimili uliojichimbia. Kabla ya kupelekeshwa na mihemuko, na hatimaye kufanya uamuzi wowote ule wa kukurupuka, ni lazima kwanza apate ushauri kwa bosi wake.
 
Mtu uuze vitumbua halafu uje kuwa mtu smart wa kuongoza mhimili. Nonono
Tatizo mnataka drama hata kwenye vitu vyenye taratibu

Issue ya tembo si kuna mamlaka husika?

CAG si wahusika wananyooshwa?

Mbolea ndio mtihani
 
Back
Top Bottom