Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Eenh! Microphone check [emoji441]
Screenshot_2021-11-09-17-43-34-08.jpg
 
Mode, mimi ni Tomaso, this letter doesn't look real! is this bonafide genuine?. Headed paper gani hii haina address?.
Hiyo barua ya kujiuzulu ikowapi?.
please do the needful.
P
Kwamba pengine Jobo kagoma wazee wakaamua kuandika na kutuma twitter?
 
On his way to CHADEMA.
Ndugai for presidency 2025 watu weweeeeeee
Sidhani kama hiyo subwoofer itafika 2025 bila kupasuka, hata sasaiv unawezakuta yuko hoi kitandani.
 
Kosa la ndugai liko wapi kwa mjibu wa sheria? Je, ndugai kavunja katiba katika kutoa maoni yake...!

Kosa la ndugai, linapaswa liwe la kichama na si kama anavyosakamwa aachie ngazi!

Kwa katiba ipi na sheria ipi inayodai sipika akitoa maoni yake kuhusu jambo la kiserikali atawajibika/wajibishwa?

Chama ndicho chaweza kumwajibisha ikiwa ziko taratibu za aina hiyo ila si kwa kumvua madaraka ya usipika!

Ngoja litokee hili, Tutajiona mapanzi mbele ya dunia kwa jinsi itavyoonyesha katiba yetu isivyiheshimiwa na kujitoshereza!

Sasa nimeelewa kwamba, Tz katiba yetu ni mbovu kuliko chochote!

Kwa nchi zenye watu wenye kupima ukweli wa jambo kupitia katiba walizonazo, Kusingeeleweka ikiwa sipika anashinikizwa kuachia ngazi kwa jambo ambalo halipo kikatiba

Mh Sipika ni mkuu wa mhimili unaojitegemea, lkn pia ni RAIA wa Tz mwenye Uhuru wa kutoa maoni yake katika jambo lolote lile huku akizingatia sheria za nchi

Niko na Ndugai na hana kosa kisheria na kikatiba
Watanzania tuwaze nje yabox anayo msururu was yanayomzonga na tusishadadie Moja pekee, iwapo amekubali kuwajibika Kwa hiari ni jambo jema na funzo Kwa wenye manlaka.
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni

Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama

#JamiiForums

Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai tarehe 10 Novemba 2020, alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 baada ya kupata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7. Kura moja ilimkataa. Ndugai alikuwa spika katika Bunge la 11 la 2015 - 2020.

Hapo awali akizungumza Desemba 28 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa kwani ipo Siku Nchi itapigwa Mnada

“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.

Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni.


View attachment 2070821
Hatakosa Uwaziri huyu. Hongera Mheshimiwa
 
Sheria inasema spika anapaswa kujiuzulu mbele ya bunge sasa imekuaje hapa? Afu mbona barua ni kavu
... hatujaletewa barua humu; kilicholetwa humu ni taarifa kwa umma kwamba Ndugai kaandika barua ya kujiuzulu. Kuhusu kujiuzulu mbele ya Bunge, kama ndivyo sheria inavyosema, hatua ya kwanza ni kuandika barua then "ikikubaliwa" mengine yanafuata ikiwemo kujiuzulu mbele ya Bunge.
 
Alikuwa anadhani upinzani ni jambo rahisi, amekuwa mpinzani ndani ya wiki tu na uspika ameukosa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Alijua kuwa mpinzani ni kitu rahisi rahisi,
Namfananisha na chama cha CCJ, kilikufa haraka sana.
 
Back
Top Bottom