Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ni wazi bioa shaka kilichofanyika kwa Ndugai ni uvunjifu wa Katiba.

Tangu tumepata Katiba Mpya hajawahi kutokea Rais kuingilia Muhimili mwingine na Kuchochea/Kufanya mapinduzi kwenye huo Muhimili, ila Rais Huyu amefanya hivyo.

Wabunge wanaoamini walioenda Bungeni kwa ajili ya Wananchi na Jamhuri na si kwa ajili ya CCM wanatakiwa wachukue Hatua kuiondoa nchi Kwenye Shimo la Kuzimu ambalo Rais Huyu anatuvuta twende.

Kama wabunge msipolifanyia kazi jambo hili Wananchi watalifanyia kazi...

CCM imepoteza uwezo na Sifa ya kuiongoza Tanzania. Mlioko Bungeni mna Nafasi ya kujirekebisha na kuiokoa Tanzania
 
Ukisikia benefits atazopata unaweza kuzimia!
Yaani vile walijitungia Sheria ya kinga na kujilinda, kaona aondoke kabla muswada wa kutengua hayo yote hajaupitisha akiwa yeye mwenyewe ni subwoofer!

Everyday is Saturday......................................😎
 
Mama aliwaambia wanademka tu bungeni.

Sijui kwa nin hawakumuelewa, hasa huyu Job.
Ile ilikuwa ni kiashiria kuwa hawakubali viongozi wa mhimili wa bunge.

Ona sasa yanayotokea. Acheni kudemka mama atawatoa roho.
 
Ndugai hajaandika barua ya kujiuzulu uspika kwenda kwenye Ofisi ya Bunge, bali kaandika kwenda kwenye chama CCM. Bunge haliwezi kufanyia nakala ya barua hio kazi maana halina mamlaka hayo kikatiba.

Kwa msingi huo, bado ni spika kikatiba.

Ndugai aandike barua nyingine kwenda Ofisi ya Bunge ndio atakuwa amejiuzulu.
 
Japo hoja yake ilikuwa na mashiko, ila wacha tu aondoke kwa kukandamiza demokrasia na kuvunja katiba ya nchi
 
Utakaa nyuma kabisa kuleeee karibu na babu tale[emoji2][emoji2]
Screenshot_20220107-090639_WhatsApp.jpg
 
Yuko sawa, katibu mkuu wa ccm atamjulisha katibu wa bunge kuwa nafasi iko wazi
 
Unateseka ukiwa wapi sukuma gang wewe[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ndugai hajaandika barua ya kujiuzulu uspika kwenda kwenye Ofisi ya Bunge, bali kaandika kwenda kwenye chama CCM. Bunge haliwezi kufanyia nakala ya barua hio kazi maana halina mamlaka hayo kikatiba.

Kwa msingi huo, bado ni spika kikatiba.

Ndugai aandike barua nyingine kwenda Ofisi ya Bunge ndio atakuwa amejiuzulu.
 
Attachments

  • IMG_1501.MP4
    1.9 MB
Back
Top Bottom