Spika Ndugai 2025 sio mbali, ni kweli kuongeza tozo za miamala kutapeleka zahanati, maji, madawati, madarasa na barabara kila kijiji kabla ya 2025?

Spika Ndugai 2025 sio mbali, ni kweli kuongeza tozo za miamala kutapeleka zahanati, maji, madawati, madarasa na barabara kila kijiji kabla ya 2025?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, hivi ni kweli sababu ya Bunge lako kuongeza tozo kwenye miamala ya simu ni kumalizia upatikaji wa barabara, maji, madawati, madarasa, na zahanati katika kila kijiji kabla ya 2025?

Naungana na wewe 100% kuwa hakuna mfadhili atakuja kutujengea nchi yetu, hivyo ni jukumu letu kujikamua wenyewe kwa hali na mali kulijenga taifa letu kwa nguvu zetu.

Hata hivyo, Tanzania hakuna mtu asiyelipa Kodi. Kila huduma na kila bidhaa ina kodi ndani yake ambayo mtumiaji lazima ailipe. Lakini kuna Kodi za mapato, tozo, biashara na huduma pia. Mtu anayelipa PAYE atalipa tena kodi mbalimbali kwa kutumia hela yake iliyobaki baada ya kulipa PAYE.

Tatizo letu kubwa sio mapato, ni matumizi, vipaumbele, usimamizi mbaya na wizi wa fedha za umma, hata wewe unafahamu hili, ripoti za CAG zinaonyesha kila mwaka.

Kama taifa tuliamua kutumia fedha zetu kuboresha umajumuni wa Afrika badala ya kusambaza maji kwa watu wetu.

Kama taifa tunagharamia kuendesha siasa zetu kwa gharama kubwa sana bila sababu za msingi badala ya kupeleka pembejeo za kilimo na masoko kwa watu wetu ili walime kwa tija.

Kama taifa tunaanzisha miradi ambayo haisaidii kuongeza uchumi wa taifa.

Kama taifa tuna rasilimali nyingi sana, maji, ardhi, madini, wanyama pori, mifugo, na misitu ambazo hatujafanya vyakutosha kwenye rasilimali hizi kupata fedha ili kuepuka aibu ya kama Bunge kufikiria kuongeza gharama kwa machinga anaetembeza mashati 3 mkononi anayetaka kumtumia hela bibi yake aliyeko kijijini ili anunue chumvi na mafuta yaa taa. Nijuavyo mimi hela nyingi kwa kutumia simu huwa zinatumwa kutoka mijini kwenda vijijini waliko wategemezi wao ambao wana njaa, misiba, wagonjwa na shida nyingine huko vijijini.

Inatia Mashaka makubwa kuwa na Bunge lenye wabunge ambao hawawezi kufikiria namna tutakavyoweza kuchima chuma, dhahabu, kuboresha kilimo na mifugo, kuvua samaki baharini, kutumia misitu yetu na mbuga ili kupata hela kubwa ya kulihudumia taifa na watu wake badala yake wanawaza kuvitoza pesa vibabu vilivyotumiwa vijisenti vya kujikimu na wajukuu zao.

Kama ni lazima tozo hiyo iwepo, basi ingeazia kwa watu watakaotuma sh. 300,000 na kuendelea lakini sio sh. 5000, 10,000 au 50,000.

Dawa kubwa ni kuchagua kipi kijengwe Leo na kipi kinaweza kusubiri kesho.
 
Yani utadhani kodi unayokusanywa na Serikali inapelekwa kwenye matumizi mengine yasiyojulikana na hii ya simu ndio inapelekwa kwenye mtaji,umeme,Barbara,madarasa na mambo mengine.
Sasa kazi ya hii Serikali ni nini hasa??
 
Muulize kwanini ndugu zake hawakumchangia matibabu India.
Anataka tena vijisenti vya masikini vimlipie yeye.
Ndugai ovyo,Rais amesema wapitie upya,yeye anasema imeshapita ni sheria.Dharau na kiburi
 
Kibanda changu cha uwakala wa NMB na CRDB kimongeza wateja Mara NNE ya ilivyokuwa mwanzo tuendelee.

Naona kabisa ile kodi ikikwama labda hapa katikati waongeze na ya bank
 
Muulize kwanini ndugu zake hawakumchangia matibabu India.
Anataka tena vijisenti vya masikini vimlipie yeye.
Ndugai ovyo,Rais amesema wapitie upya,yeye anasema imeshapita ni sheria.Dharau na kiburi
Lazima apaze sauti kuitetea, maana imepita bungeni kwake. Ndiyo maana Prof. Asad alisema bunge lake ni dha
 
Kibanda changu cha uwakala wa NMB na CRDB kimongeza wateja Mara NNE ya ilivyokuwa mwanzo tuendelee.

Naona kabisa ile kodi ikikwama labda hapa katikati waongeze na ya bank
Mpaka iende bungeni tena
 
Watawasingizia wapinzaniHii

Watawasingizia wapinzani

Watawasingizia wapinzani
Hii inaweza kuwa ni hujuma kwa mama ili hata vijijini wamuone hafai hasa pale 2025 ahadi hizi za maji, zahanati, madawati, nk zisipotimia. awe macho kwa kila kitu kutoka kwa kila mtu. Mimi nilidhani Bunge lingejikita kwenye giant projects kama upanuzi na usimamiaji wa Bandari zetu, namna gani ndege zetu zitazalisha, uchimbaji wa madini ya chumba ili kujenga viwanda mama nchini. Hee, small minded wanafikiri small projects kama kuongeza mafuta na miamala kwa walalahoi na kushusha bei ya pombe.
 
Back
Top Bottom