beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai leo amehoji kwanini Fedha zinakwama Wizara ya Fedha akimtaka Waziri kujiandaa akisema, "Siku ya Wizara yake nitakamata Shilingi mimi mwenyewe"
Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni Dodoma wakati Bunge likijadili Hotuba ya Wizara ya Nchi - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Ameeleza, "Bunge tunaweza kuweka 'pressure' lakini sio vizuri tuiweke mahali ambapo hakuna sababu. Waziri nataka majibu, Fedha zinazokuja kwa ajili ya mazingira zinakwama Wizara ya Fedha kwa sababu gani? Mpaka inafika mahali zinataka kurudishwa"
Ameongeza, "Kwanini Fedha inaombwa inakuja katika Nchi yetu Wizara ya Fedha mnakalia eti kisa Kamati haijakaa. Katika jambo hilo tunataka badiliko"