msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Akiwa kwenye kongamano lililokuwa limeandaliwa na vijana wenyeji wa dodoma ambapo alialikwa kama mgeni rasmi katika kongamano hilo, spika Ndugai amedai kuwa kuna upotoshaji mwingi sana unaendelea nchini.
Akitolea mfano suala la yeye kupingwa, Ndugai amesema anapingwa si kwa sababu ana pungufu lolote isipokuwa ni kwa sababu anatoka kwenye kabila la wagogo.
"Kuna baadhi wananiandika kila kukicha siyo kwa sababu nina pungufu lolote ila ni kwakuwa mimi ni mgogo" alisema.
Pia, alisema wengi wanaomchafua na kupotosha ni vijana wenye elimu ya juu 'digrii' kwamba badala ya wao kufanya kazi wanatumia simu zao za mkononi kumtukana mitandaoni.
" Darasa la saba ndiye mtoto mwenye maana kwa mzazi kwa sababu ukimwambia lima ana lima ila huyu wa digrii yeye ana simu ya mkononi, yupo kwenye makundi ya kutukana utasikia wanasema huyu spika bure kabisa huyu kisa wana digrii" alisema Spika Ndugai na kuongeza.
Katika hatua nyingine spika Ndugai amesema kuna upotoshaji unafanyika wakati wa upitishwaji wa sheria bungeni. Amesema kuna muda bungeni zinapitishwa sheria za hovyo kabisa.
Akitolea mfano wa marekebisho ya sheria mbali mbali 'miscellaneous amendments' amedai kuwa zinawasilishwa bungeni zikiwa vipande vipande tena kipindi ambacho wabunge wamesambaratika sehemu mbali mbali hivyo sheria hizo zinapata mwanya wa kupita kutokana na kutokuwepo kwa organization ya wabunge na pale mambo yanapoharibika linalaumiwa bunge kumbe kanuni zinakuwa zimetungwa na kupitishwa na wakurugenzi, taasisi na mawaziri wa wizara husika