Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa bunge kama chombo cha wananchi si ndio kilitakiwa kihakikishe hizo sheria mbovu hazipiti.Amesema ukweli mtupu. Hali ndio iko hivyo. Bunge linadharaulika kwa sababu hiyo tu. Sheria nyingi za Tanzania, source yake ni cabinet; Na cabinet hupokea kutoka kwa watendaji waliopo chini ya wizara yake. Na bunge linapokea bila kufanya critical analysis na changes kwa maslahi mapana ya Taifa.
😂😂wanasmimanga kisa mgogo sio
[emoji23][emoji23]wanasmimanga kisa mgogo sio
Amekiri udhaifu wa hali ya juu kwake na kwa bunge zima la jamuhuri.Ndigai ame piga nduru!
Ndiyo ukweli tupuTusipo kuwa makini itachukua miaka 500 Tanzania kuendelea kiuchumi.
Wake wana mastersProf. Assad huko ulipo, BIG UP SANA!
Mvua imenyesha tumejua panapovuja.
Je watoto wake wameishia darasa la 7?
Mishe zangu zikigoma nami niseme tunaotoka mkoa ule tunasakamwa sana.
Jamani si ndiyo huyu huyu, aliyepitisha azimio la kpongeza kushinda kiti cha MWENYEKITI wa sadcc, kawati akijua ni uongo mtupu, kiti hakishindaniwi Bali ni kwa majibu wa Kati a ya jumuia hiyo. Sasa Omani kwake itatoka wapi?Akiwa kwenye kongamano lililokuwa limeandaliwa na vijana wenyeji wa dodoma ambapo alialikwa kama mgeni rasmi katika kongamano hilo, spika Ndugai amedai kuwa kuna upotoshaji mwingi sana unaendelea nchini.
Akitolea mfano suala la yeye kupingwa, Ndugai amesema anapingwa si kwa sababu ana pungufu lolote isipokuwa ni kwa sababu anatoka kwenye kabila la wagogo.
"Kuna baadhi wananiandika kila kukicha siyo kwa sababu nina pungufu lolote ila ni kwakuwa mimi ni mgogo" alisema.
Pia, alisema wengi wanaomchafua na kupotosha ni vijana wenye elimu ya juu 'digrii' kwamba badala ya wao kufanya kazi wanatumia simu zao za mkononi kumtukana mitandaoni.
" Darasa la saba ndiye mtoto mwenye maana kwa mzazi kwa sababu ukimwambia lima ana lima ila huyu wa digrii yeye ana simu ya mkononi, yupo kwenye makundi ya kutukana utasikia wanasema huyu spika bure kabisa huyu kisa wana digrii" alisema Spika Ndugai na kuongeza.
Katika hatua nyingine spika Ndugai amesema kuna upotoshaji unafanyika wakati wa upitishwaji wa sheria bungeni. Amesema kuna muda bungeni zinapitishwa sheria za hovyo kabisa.
Akitolea mfano wa marekebisho ya sheria mbali mbali 'miscellaneous amendments' amedai kuwa zinawasilishwa bungeni zikiwa vipande vipande tena kipindi ambacho wabunge wamesambaratika sehemu mbali mbali hivyo sheria hizo zinapata mwanya wa kupita kutokana na kutokuwepo kwa organization ya wabunge na pale mambo yanapoharibika linalaumiwa bunge kumbe kanuni zinakuwa zimetungwa na kupitishwa na wakurugenzi, taasisi na mawaziri wa wizara husika
View attachment 2061917
Nchi kama ipo serious haiwezi kuwa na Spika mpuuzi kama huyu mzeeKwa 100% kuna matatizo ya uteuzi au kuwachagua viongozi wa muhimili mbalimbali, historia zao, uwezo wao na weledi wao haviangaliwi kwa makini ndio maana tunakuwa na viongozi kila kukicha wanaropoka hovyo na hawakawii kuja kukana kauli zao!
Tuchukue hatua
Alisahau kumeza vidonge vyake vya utahilaHuo mkutano wa juzi nadhani Mh.Spika hakuwa katika wakati mzuri kisaikolojia, mbona kama alipuyanga sana?
MH SIAMINI HAYA KABISA KWELI KABISA SUPIKA WETU WA BUNGE ANAWEZA KUSEMA SHERIA MBOVU ZINAPITISHWA KWENYE BUNGE LAKE?!?!!? HALAFU YEYE MWENYEWE AZILALAMIKIE?!? HIVI TUULIZANE NI NANI ANYEPELEKA SHERIA ZILIZOPITISHWA NA BUNGE KWA RAIS?!?. NAANZA KUAMINI SUPIKA KUNA KITU KICHWANI MWAKE KIMELEGEA SUKURUBU IMEACHIA MEDULA OBLANGATA, ANAHITAJI KURUDI INDIA!!. HIVI KWELI SUPIKA NAKIMBILIA KWENYE UGOGO,UKABILA?!?!, USOMI, DARASA LA SABA?!?! HIZO NI HOJA KWELI ZA KUTULETEA HAPA KAMA VILE SISI WATZ WOOOTE NI MBUMBUMBU!!??!, NO HATUKO MAZEZETA KIASI HICHOAmesema ukweli mtupu. Hali ndio iko hivyo. Bunge linadharaulika kwa sababu hiyo tu. Sheria nyingi za Tanzania, source yake ni cabinet; Na cabinet hupokea kutoka kwa watendaji waliopo chini ya wizara yake. Na bunge linapokea bila kufanya critical analysis na changes kwa maslahi mapana ya Taifa.