wakaliwetu
JF-Expert Member
- Jul 16, 2020
- 671
- 1,143
Dunia simama TANZANIA inakokwenda haikujui, mteremko ni mkali sana na breki zote zimefeli.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Urasi wa nchi hii mkuu?Kuna kitu anakitafuta na hiko kitu ni kua Rais...
Tatizo sio idadi, bali hata kama mswaada ni mbovu kivipi hakuna wa kusimama na kuupinga wote wataitikia ndioooooo, sasa yeye Ndugai anachotaka ni kuwepo upinzani wa kutosha ili kuzuia miswaada mibovu kama hiyo isipite, yeye pekeyake hawezi na akijaribu ataitwa kwenye vikao vya ccm kuhojiwa.
Kwa video hii tuna spika mbovuuuuu haijawahi tokeaAkiwa kwenye kongamano lililokuwa limeandaliwa na vijana wenyeji wa dodoma ambapo alialikwa kama mgeni rasmi katika kongamano hilo, spika Ndugai amedai kuwa kuna upotoshaji mwingi sana unaendelea nchini.
Akitolea mfano suala la yeye kupingwa, Ndugai amesema anapingwa si kwa sababu ana pungufu lolote isipokuwa ni kwa sababu anatoka kwenye kabila la wagogo.
"Kuna baadhi wananiandika kila kukicha siyo kwa sababu nina pungufu lolote ila ni kwakuwa mimi ni mgogo" alisema.
Pia, alisema wengi wanaomchafua na kupotosha ni vijana wenye elimu ya juu 'digrii' kwamba badala ya wao kufanya kazi wanatumia simu zao za mkononi kumtukana mitandaoni.
" Darasa la saba ndiye mtoto mwenye maana kwa mzazi kwa sababu ukimwambia lima ana lima ila huyu wa digrii yeye ana simu ya mkononi, yupo kwenye makundi ya kutukana utasikia wanasema huyu spika bure kabisa huyu kisa wana digrii" alisema Spika Ndugai na kuongeza.
Katika hatua nyingine spika Ndugai amesema kuna upotoshaji unafanyika wakati wa upitishwaji wa sheria bungeni. Amesema kuna muda bungeni zinapitishwa sheria za hovyo kabisa.
Akitolea mfano wa marekebisho ya sheria mbali mbali 'miscellaneous amendments' amedai kuwa zinawasilishwa bungeni zikiwa vipande vipande tena kipindi ambacho wabunge wamesambaratika sehemu mbali mbali hivyo sheria hizo zinapata mwanya wa kupita kutokana na kutokuwepo kwa organization ya wabunge na pale mambo yanapoharibika linalaumiwa bunge kumbe kanuni zinakuwa zimetungwa na kupitishwa na wakurugenzi, taasisi na mawaziri wa wizara husika
View attachment 2061917