Spika Ndugai amesema kuna upotoshaji mwingi unaendelea nchini, adai kuna wakati sheria za hovyo zinapitishwa bungeni

Spika Ndugai amesema kuna upotoshaji mwingi unaendelea nchini, adai kuna wakati sheria za hovyo zinapitishwa bungeni

Kwamba ndug, jobu ndugai speeker wa bunge anajitetea mbele watetezi wake au hanafanya kitu gani hii.... Rubish kabisa
Hizi ni tatizo la akili ndogo kutwala akili kubwa...
Final say bungeni ni spika, so nani anapitisha izo sheria hanazo ziita miscellaneous ammendiment.... Kama yeye ajausiswa .huyo ni mzigo kwa taifa hovyo kabisa... na kwa nn?? .. hame- base sana kwenye ukabila..
 
speerker
FB_IMG_1640927930932.jpg
 
Hao vijana wasomi wanaokushambulia mitandaoni wako sahihi, na sababu ni hizo ulizotaja, Bunge kupitisha miswada kwa kuvizia nawe unajuwa hali hiyo uchukui hatua, wacha wakutukane!
 
Akiwa kwenye kongamano lililokuwa limeandaliwa na vijana wenyeji wa dodoma ambapo alialikwa kama mgeni rasmi katika kongamano hilo, spika Ndugai amedai kuwa kuna upotoshaji mwingi sana unaendelea nchini.

Akitolea mfano suala la yeye kupingwa, Ndugai amesema anapingwa si kwa sababu ana pungufu lolote isipokuwa ni kwa sababu anatoka kwenye kabila la wagogo.

"Kuna baadhi wananiandika kila kukicha siyo kwa sababu nina pungufu lolote ila ni kwakuwa mimi ni mgogo" alisema.

Pia, alisema wengi wanaomchafua na kupotosha ni vijana wenye elimu ya juu 'digrii' kwamba badala ya wao kufanya kazi wanatumia simu zao za mkononi kumtukana mitandaoni.

" Darasa la saba ndiye mtoto mwenye maana kwa mzazi kwa sababu ukimwambia lima ana lima ila huyu wa digrii yeye ana simu ya mkononi, yupo kwenye makundi ya kutukana utasikia wanasema huyu spika bure kabisa huyu kisa wana digrii" alisema Spika Ndugai na kuongeza.

Katika hatua nyingine spika Ndugai amesema kuna upotoshaji unafanyika wakati wa upitishwaji wa sheria bungeni. Amesema kuna muda bungeni zinapitishwa sheria za hovyo kabisa.

Akitolea mfano wa marekebisho ya sheria mbali mbali 'miscellaneous amendments' amedai kuwa zinawasilishwa bungeni zikiwa vipande vipande tena kipindi ambacho wabunge wamesambaratika sehemu mbali mbali hivyo sheria hizo zinapata mwanya wa kupita kutokana na kutokuwepo kwa organization ya wabunge na pale mambo yanapoharibika linalaumiwa bunge kumbe kanuni zinakuwa zimetungwa na kupitishwa na wakurugenzi, taasisi na mawaziri wa wizara husika
View attachment 2061917
Ondoa " vijana wenyeji wa Dodoma" weka "wagogo"
 
Ameona atumie ukabila kama turufu!? Anataka vijana wasihoji wao wanapoharibu vijana walime tuu?
Anakosolewa mambo haya atuambie ugogo unakujaje
-kuhusu wabunge wa covid 19.
-kuhusu kugombana na Assad.
-kutotaka yeyote amkosoe spika au alikosoe bunge
-kuadhibu vikali wabunge wa upinzani kiss hojazao
- kupitisha haraka sheria mbovu za aibu mpaka yeye kujishangaa
-chuki na ubabe usio na maana
-kushindwa kumtendea haki mbunge alopigwa risasi akiwa kazini
-kutangaza bungeni kuwa kunawabunge hawatorudi kisa yeye hawapendi
-kumkosoa rais samia hadharani
-kutumia bunge kushambulia watu hata wa mitandaoni
Niaibu kubwa mhimili kuongozwa na MTU dhaifu hivi anayejiita eti mzee wa kanisa...
 
Akitolea mfano suala la yeye kupingwa, Ndugai amesema anapingwa si kwa sababu ana pungufu lolote isipokuwa ni kwa sababu anatoka kwenye kabila la wagogo.
Huyo ndio bingwa wa kukomoa upinzani na wapinzani.
Wa chama chake na hata waandishi nguli wanamtukuza na kumshangilia sana kwa ujinga huu unaoendelea kuua taifa letu kwa kasi. Eti ndio ushindi kwa chama chao kufanikiwa kuondoa 'kupingwapingwa', sijui ili iweje.
Bunge limekuwa ni la vigodoro, haiko tena kusimamia maslahi ya n chi na taifa. Linafanya vituko vya aibu mpaka kuruhusu hata wasio na chama kuwa nao humo. Kwa sasa hakuna tofauti ya mapofesa, wanasheria, wasomi na wale ambao hawakujaaliwa kupata elimu. Ndugai anaendelea kufaidi mapambio ya kishetani. Uzuri keshaanza kulia mwenyewe.
 
Tumeshuhudia ndugai akifukuza wabunge wenye uwezo wa kujadili, akiwazuia kuongea kwa Uhuru wao, ....... Ndugai ni mpumbavu maandalizi. Ukirejea jinsi bunge la 2015-2020 alivyo liendesha utakubaliana na mimi, huyu jamaa hafai.
Huko sahihi kabsaa, kwan ukisikia mtu anaendeshwa na tumbo unaelewaje, mfno mzuri umeona baada ya kuondoka jpm
 
Tusipo kuwa makini itachukua miaka 500 Tanzania kuendelea kiuchumi.
Kama tukiendelea kupata viongozi wenye kuzungusha tako kwa mabeberu na kusujudia mabeberu hata hiyo miaka mia5 itakuwa bado atujaendelea
 
basi alitakiwa kwa mamlaka yake kama spika azuie majadiliano ya jambo hilo mpaka wakati
Siyo kwa nchi hii. Hiyo unaongelea kinadharia mkuu. Kivitendo haiwezekani. Rais atake jambo lake lipitishwe bungeni halafu spika azuie? Jioni yake atavuliwa uanwchama na uspika na ubunge ataondolewa na kwenda kuwa mkulima wa kawaida
 
Huyu jamaa ni dhaifu sana

Alivyoambiwa kuwa yeye ni spika dhaifu, akaanza kuwatoa wabunge wa upinzani ndani ya bunge ili kudhibitisha kuwa yeye sio dhaifu! Bila kujua uimara haukuwa unapimwa kwa ubabe wa kijinga, bali hizo sheria mbovu zinazopitishwa. Leo huu anakiri kuwa kuna sheria mbovu zinapitishwa, ila anataka asitukanwe na kuonekana sio dhaifu.
 
Anachotaka kusema hapa ni kuwa serikali inapitisha miswada kwa kuvizia attendance ya wabunge??

Kama ameliona hilo anapaswa kuwakatalia kwa kuhakikisha kuwa miswada inajadiliwa kukiwa na mahudhurio ya kutosha ya wabunge.

Hapo tunaanza kuulizana National Interest ni ipi??
Kutowesha upinzani nchini.
 
MH SIAMINI HAYA KABISA KWELI KABISA SUPIKA WETU WA BUNGE ANAWEZA KUSEMA SHERIA MBOVU ZINAPITISHWA KWENYE BUNGE LAKE?!?!!? HALAFU YEYE MWENYEWE AZILALAMIKIE?!? HIVI TUULIZANE NI NANI ANYEPELEKA SHERIA ZILIZOPITISHWA NA BUNGE KWA RAIS?!?. NAANZA KUAMINI SUPIKA KUNA KITU KICHWANI MWAKE KIMELEGEA SUKURUBU IMEACHIA MEDULA OBLANGATA, ANAHITAJI KURUDI INDIA!!. HIVI KWELI SUPIKA NAKIMBILIA KWENYE UGOGO,UKABILA?!?!, USOMI, DARASA LA SABA?!?! HIZO NI HOJA KWELI ZA KUTULETEA HAPA KAMA VILE SISI WATZ WOOOTE NI MBUMBUMBU!!??!, NO HATUKO MAZEZETA KIASI HICHO. NAANZA KUKUMBUKA ISSUE YA PROF. ASSAD KUANZIA REPORT YAKE YA UKAGUZI MPAKA HOJA YA BUNGE NI DHAIFU. SUPIKA KATUHAHAKISHIA ASILIMIA MIAMOJA BILA KUBAKIZA KWAMBA KWELI BUNGE NI DHAIFU HASWAA!! KWA KUSEMA SHERIA MBOVU ZILIPITISHWA BUNGENI
Ujinga au wehu wa Spika ni kupayuka ovyo. Lakini ukweli ni kuwa Bunge linapokea na kutekeleza maagizo ya serikali (Ikulu) - mihimili uliojichimbia chini zaidi.

Bunge lenyewe la CCM na waunga mkono wa juhudi. What good can come outa such trash. Assad alilita kwa usahihi kabisa, bunge la mazuzu.
 
Ndo maana ya BUNGE DHAIFU. CAG alipotamka kauli hii, Spika alikua mkali kama Mbogo aliyejeruhiwa. Leo anakiri mwenyewe. Wewe Ndugai ulieaminiwa ukapewa usupuka, Ni nani aliyekuloga?
 
Back
Top Bottom