Spika Ndugai aomba radhi Wakristo kwa kauli yake kuhusu Yesu

Spika Ndugai aomba radhi Wakristo kwa kauli yake kuhusu Yesu

Nimeona taarifa ya Bunge kuwa Ndugai anatuomba radhi Wakristo. Kusema Yesu ana mke hayo ni maneno ya Mpinga Kristo kwa mujibu wa imani yangu.

Kwanini Ndugai atume mtu aniombe radhi wakati amemdhalilisha Bwana wangu Yesu Kristo na kumnenea uongo?

Ndugai ameshindwa nini kuja kwenye vyombo vya habari yeye mwenyewe au kutumia njia ilele aliyonikwaza kuniomba radhi?

Mimi naona amenidharau na dini yangu na Bwana wangu. Sijamsamehe
Wewe na Ndugai wote mpo kwenye kundi moja.
 
Spika alimtaka Jerry Silaa kukanusha kaulivyake kwa njia ileile aliyoitolea, yaani aite wananchi na kwenye mkutano huo abadili maneno yake kuhusu wabunge kutolipa kodi.
Kwanini naye asutumie njia ileile aliyotolea kauli yake kuwa Yesu alikwenda Yerusalemu akiwa na mkewe, akanushe na kuwaomba radhi wakristu na kuliomba bunge msamaha kwa kulidanganya, huku akijua kuwa anasema uongo na kuwakera watu na Yesu mwenyewe?
 
Ni sawa kwa spika kulidanganya bunge na kulivunjia heshima mbele ya jamii kwa kusema Yesu alikuwa na mke?
Nami ataiambia kamati imhoji na alete ushahidi wa kauli yake?
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaomba radhi wakristu kwa kauli aliyotoa leo bungeni alipokuwa akielezea alivyotembelea Israel

Katika maelezo yake alisema "Yesu alitembea na mke wake kutoka Nazareti kwenda Yerusalemu kuhesabiwa" ambapo amesema alimaanisha Yusufu alitembea na mke wake sio Yesu kama alivyotamka

Amesema kilichotokea ni kosa la kibinadamu. Alivyokuwa anaeleza kuwa anaufahamu ukristo vizuri na kuwa amewahi kuhiji maeneo matakatifu

View attachment 1918431
View attachment 1918433
Huyu Ndugai vipi?
 
Hahaha Hiyo Inaitwa Mfupa Hauna Ulimi,,,ulimi Hauna...Hayo Ni Makosa Ya Kimatamshi Tu. Najiuliza Tu Hivi Angekuwa Ananisimulia Mimi Binafsi Tupo Wawili Kama Mkristo Angeniomba Msamaha?
 
Acheni kutafuta ujiko kirahisi rahisi. Akuombe msamaha kwani amekukosea nini? Kukosea ni jambo la kawaida. Isitoshe, kisheria, anaypaswa kuomba msamaha ni Yesu kama atakuwa ameudhika. Pia, fahamu. Yesu alipoondoka alicha wanafunzi na si wakristo jina ambalo liliundwa na maadui zake kwa kejeli wakimaanisha wale walioanza kufuata mafundisho yake sawa na walutheran na luther au wahutterite na Jacob Hutter wamennonite na Menno Simmons etc.
Hahahaha Na Ndio Maana Hata Wewe Huwezi Kutuomba Msamaha Kwa Kwa Kujiita Father Of All.
sijui Ulimaanisha Baba Wa Vyote Au Wa Wote, Lakini Je Sisi Wote Wewe Ni Baba Yetu? Tuombe Radhi Tafadhali
 
Simsamehi katu. Huyu ndiye mwakilishi wa "666" hapa Tanzania.
Uko sahihi mkuu kwa maneno kutoka kinywani mwake yanayoashiria uwakilishi wa mpinga kristo (blasphemy) is just an iceberg the worst is still to come when the citizens will gnash due to the torment endorsed by the authority of this type
 
Back
Top Bottom