Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Akikazia mawazo ya wabunge kama kawaida yake nimemsikia Mh Speaker ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwaongezea masomo ya kufundisha walimu kwa maana ya kuwafundisha kuyafundisha tangu wakiwa vyuoni hasa vyuo vikuu ili kupunguza uhaba wa walimu na kuongeza tija kwa wanafunzi.

Akitolea mfano wa Balozi Mbelwa Kairuki alichomsimulia kule China mwaka jana, Ndugai amesema kuwa kule China vijana wanajua mambo mengi sio kama hapa Tanzania ambapo kijana anajua kazi moja tu kama ni fundi ujenzi ni ujenzi tu na kama ni kuchomelea ni kuchomelea tu.

"Kwanini mwalimu wa high school nafundisha somo moja" eti mmesomea kufundisha somo moja tu ili iweje na uhaba huu wa walimu alihoji speaker Ndugai.

Anatakiwa afundishe masomo matatu, manne au hata kuendelea .hali iliyoibua hoja ya mkwamo wa walimu wanaongojea kazi serkalini na kujiuliza watakwenda wapi? Kama wazo la speaker litafanyiwa kazi.
Nafikili kila shule ipate walim wa kujitolea sie mazazi tuwachangie ili kupata ufanisi mzuri , kuliko kulazimisha kuongeza , masomo
 
Nafikili kila shule ipate walim wa kujitolea sie mazazi tuwachangie ili kupata ufanisi mzuri , kuliko kulazimisha kuongeza , masomo
Hata hivyo suala la kuongeza masomo haliwezekani mtu mmoja hawezi kufundisha masomo zaidi ya matatu yale aliosoma advanced level. Mostly ni masomo mawili.
 
Kuna watu wanakuwaga sehemu viwiliwili tu.

1. Masomo matano wameyasomea lini?

2. Madhara ya kuwa overwork walimu na quality ya elimu ni mauti kwa taifa.

3. Inaonyesha sasa taifa haliijui. na wala halina kipaumbele katika ubora wa elimu.

4. Uhaba huo wa walimu unatoka wapi wakati kuna walimu wengi tu wako mitaani hawana kazi?

5. Kwa nini kuboreshwa skwa elimu hakuzungumziwi? Kushuka kwa elimu na mazingira ya elimu?

Hapa kuna tatizo.


Akikazia mawazo ya wabunge kama kawaida yake nimemsikia Mh Speaker ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwaongezea masomo ya kufundisha walimu kwa maana ya kuwafundisha kuyafundisha tangu wakiwa vyuoni hasa vyuo vikuu ili kupunguza uhaba wa walimu na kuongeza tija kwa wanafunzi...
 
Tuwe making sana na elimu yetu.
Tazama video hapa.

 
Kwa mshahara upi? wewe anapigwa kiyouozi mwanzo mwisho analamba zaidi ya m 50 kwa mwezi wenzako kukomaa kote huko wanaibuka na ka laki nne nusu...kwa mwezi afu still unataka kumwongezea masomo ya kufundisha kwa siku

CCM mwogopeni Muumba nyie!!
 
Sioni uwezekano wa mtu aliyesomea masomo ya mchepuo kama PCM kuweza kufundisha masomo matano.

Physics ............1st
Chemistry ..........2nd
Mathematics......3rd

Sasa hayo masomo matano yanatoka wapi tena???

Hilo litawezekana kama tutabadilisha mitaala iwe
PCBGM
Physics
Chemistry
Biology
Geography
Mathematics

Kweli awamu hii kiboko 🙆🙌🙌
 
Back
Top Bottom