Spika Ndugai awashukia wasomi nchini, asema anajua watamshambulia katika mitandao

Cha ajabu nayeye amesoma Sheria, japo alifeli, lakini hajui maana ya "learned colleague"
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema anakerwa na kada nne ambazo zinatukuza usomi wao mbele ya Watanzania wasiopenda kujikweza.

Wahandisi wamefanya nn tena?
Anataka wapunguziwe salary. Yeye anajua kuwa kuisoma fizikia and advanced maths ni sawasawa na kusimama kwa wananchi na kuomba KurA na baadaye kujipendekeza kwa amiri jeshi mkuu. Anatuma polisi na wengine wanaiba KurA unaingia bungeni.
Hizi fani sio Sawa na kuwa chawa kwa mtu ndipo unazipata unahaso kweli.
Hata kuku inaweza inasimama ikapewa KurA kwa kulazimisha chaguzi za wizi.
Kuna mbunge mmoja alifungiwaga mbwa uwanjani zimsikilize Mana alisema msiponipa KurA mbwa zenu zitanipa so wananchi wakapeleka mbwa uwanjani yeye alikuja akazikuta.

Yaani jamaa anadharau sawa. Baadaye ataaanza kuhoji why mjeda aitwe Brigedia yaani kigogo huwa anaongea Nini sijui kumhusu inaonekana Kama ni kweli
 
Wivu...wivu
Sisi kuitwa wahandisi mtu anaumia wakati yeye anaitwa Mheshimiwa
 
Ni kweli ila hii ni Africa wengi hujitukuza na kutaka kutukuzwa mimi hawanipi shida maana hawana cha kuniambia.

Hizo Kada hapo juu ni Kada za watoto wa maskini walio wengi, mtoto wa tajiri anasomea biashara, uchumi nk na hana mda wa kutafuta law school au cpa Ili aajiriwe.

Technically huwa nawapuuza ni watu wasio na pesa,mchukue Dr mpe vihela akuuguze uone anavyopaparika.Hao wahandisi ndio kabisaa njaa tupu.
 
Tukiweka ujinga pembeni, hakuna umuhimu wowote wa mtu kujitambulisha kwa cheo au kiwango cha elimu awapo nje ya eneo lake la kazi.

Swala la kwamba wewe ni engineer, CPA, dokta, profesa, wakili nk hayo ni mambo yahusuyo profession yako na unatakiwa uyaache huko ofisini na kwenye makaratasi / wasifu wako. Swala la kwamba eti umesotea icho cheti halina mashiko hayo ni matatizo yako, hayatuhusu. Kwani sisi ndio tulikutuma ukasotee si ulienda kwa shida zako? Kuna wajasiriamali wanasotea biashara zao miaka 10+, wameanza na viosk mpaka wanamiliki supermarket wamenyamaza, we umefanya ka CPA miaka miwili unaleta ngebe eti ooh nimesotea. Nonesense!
 


Yeye alisomea nini? Uspika? Basi hatumuonei wivu. Kama bwana mifugo pia hatumuonei wivu.
In fact anaweza kujiita anavyotaka na wala sio issue
 
Wivu...wivu
Sisi kuitwa wahandisi mtu anaumia wakati yeye anaitwa Mheshimiwa
Na bado huwa wanajisahau wanataka kutoa maelekezo katika kazi zinazosimamiwa na wataalamu.
 
Mi nakubaliana nae, ni suala la mentality tu, kwani hata wagunduzi wengi katika fani mbalimbali waliopo nchi za ughaibuni tunawaona kila siku wakofanya mambo makubwa bila kujitwisha vilemba vya ukoko. Hivyo tuzo za udaktari ndizo pekee huwa nazikubali, kwani kila Mtu amesoma kwa nafasi yake mpaka tupo wengi mitaani wenye madigirii ya kila fani hadi bodi ya mikopo inadhindwa kutuhudumia waliopo vyuoni.
 
mbona wabunge wanjiita waheshimiwa inamaana binadamu wengine kama wakulima siyo waheshimiwa. Hao wajiitao waheshimiwa pekee yao wakati binadamu wote ni sawa haoni kama unashangaa zaidi. anajua PhD inapatikanaje? japo siyo lazima mtu aitwe injinia fulani lakini ni mbaya zaidi mtu kubagua watu fulani na kuwaita waheshimiwa. wote tuwe tunaitwa waheshimiwa.
 
HII NCHI NGUMU SANA, MNATUHAMISHA MIJADALA YA MAANA KWA MIJADALA ISIYO NA TIJA KABISA...

MNATAKA TUSAHAU MACHUNGU YA TOZO, KODI LUKU AU?
 
Kuna msemo wa vijana siku hizi wa HUSINIPANGIE. Hivi tumefika mahali tunaingilia uhuru wa mtu ajitambulishe kwa namna gani. Hii sio fair hata kidogo. Huko vijijini watu huitwa majina ambayo wenyewe walipenda kuitwa tangu wakiwa vijana. Huitwa hivyo. Kama aliuwa kiboko anapewa jina na wananchi ambao walisumbuliwa ni huyo kiboko na utambuliwa hivyo. Pengine ni mtu wa majigambo anaweza kujiita jina na wanakijiji umuita hivyo n.k.

Shida ni nini. Mhandisi akijiita mhandisi kuna shida gani?. Mtu akiwa anajisikia vizuri akiitwa mhandisi /eng kuna shida gani. Mbona tunaanza kuingilia maswala binafsi ya watu. Hii si sawa.
 
Wacha we,mTheolojia ktk ubora wake
 
Kwani supika mwenyewe kabobea wapi?

Yale ya mheshimiwa supika, mheshimiwa mbunge, mheshimiwa Waziri nk anayakumbuka?
Na wenzi wao pia hupenda kuitwa Waheshimiwa. Enzi zile tukimuita mke wa Mwalimu, Mama Maria Nyerere.
 
hizo Ni pumba tu, Kwani hizo taito zinawaongezea nn, huo Ni ulimbukeni na ushamba wa elimu.
 
Kutaka kutambuliwa kama "wakili msomi", halina tofauti na wabunge waliposhinikiza watambuliwe kama "Waheshimiwa" lengo likiwa ni kutafuta utukufu. Kujitofautisha na wananchi wengine ili waweze kuwatweza. Na ndiyo maana baada ya hapo walianza kujipandishia na kujilipa 12m/= kwa mwezi. Shame.
Lakini, ... Yana mwisho. Kitaibuka kizazi ambacho hakitakubali ufisadi wa aina hii. "Keki ya Taifa" lazima igawanywe kwa watu wote kwa usawa.
 
kweli upo sahihi kabisa.
 
kuitwa mheshimiwa na hizo taito za darasani yote Ni ulimbukeni hakuna la maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…