Spika Ndugai: CHADEMA wajiandae kulipa gharama za kesi ya Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
lissu-1-1.jpg

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Amesema amepewa nakala ya hukumu kutoka Mahakama Kuu iliyotupilia mbali rufaa yake namba 42 ya mwaka 2019 iliyowashitaki yeye (Spika ) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu ubunge wa Singida Mashariki.

“Nimepata nakala ya hukumu, Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikuwa wameshitakiwa na Bwana Tundu Lissu katika shauri la Mahakama Kuu namba 42 la mwaka 2019 ya kwamba Mahakama imetupilia mbali madai hayo tena kwa gharama kwa hiyo wajiandae kulipa,” amesema Ndugai.

Lissu alifungua kesi hiyo akipinga kuvuliwa ubunge wake wa Singida Mashariki ambalo kwa sasa linaongozwa na Miraji Mtaturu kutoka Chama Cha Mapinduzi.

Source: GlobalPublishers
 
Spika kwa siku anaitaja Chadema mara nyingi zaidi kuliko tunavyopata idadi mpya ya vifo vya Corona.
Kwani kuna takwimu baada ya mkuu kugundua mbuzi wana corona? Takwimu zimeshawachanganya kila mtu anakufa na kupona kwa huruma ya Mungu. Baada ya kuona tunaelekea kwenye mamia ya vifo na maelefu ya wagonjwa akastopisha kutoa taarifa
 
Sisi tunazipata na zitakuja kumtokea puani
 
Tunaomba copy/nakala ya hukumu na gharama husika tulipe mara moja. Mnajiona mmeshika mpini kuwa manaweza kumkata kila mtuu. Sisi tutachangia hizo mia tano tano kumaliza mchezo. Ila ukweli unajulikana kuwa ardhi tunayo kanyaga ni ya Mwenyezi Mungu na yatupasa kuikanyaga kwa adabu na kwa unyenyekevu mkubwa
 
lissu-1-1.jpg

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Amesema amepewa nakala ya hukumu kutoka Mahakama Kuu iliyotupilia mbali rufaa yake namba 42 ya mwaka 2019 iliyowashitaki yeye (Spika ) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu ubunge wa Singida Mashariki.

“Nimepata nakala ya hukumu, Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikuwa wameshitakiwa na Bwana Tundu Lissu katika shauri la Mahakama Kuu namba 42 la mwaka 2019 ya kwamba Mahakama imetupilia mbali madai hayo tena kwa gharama kwa hiyo wajiandae kulipa,” amesema Ndugai.

Lissu alifungua kesi hiyo akipinga kuvuliwa ubunge wake wa Singida Mashariki ambalo kwa sasa linaongozwa na Miraji Mtaturu kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Huyu jamaaa ni Maskini sana wa Roho.
Huwaga anahisi Pesa ndio kila kitu
Mara ataje Madeni ya Wabunge wa CHADEMA,mara aseme watanyimwa Posho,mara aseme warudishe Posho.
Ukiona mtu anaweka pesa mbele kwa kila kitu hata Masuala ya utu ujue ni Maskini wa Roho na ana Roho Mbaya.
Akizeeka sana usiniulize atakuwa nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom