Spika Ndugai: CHADEMA wajiandae kulipa gharama za kesi ya Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge

Spika Ndugai: CHADEMA wajiandae kulipa gharama za kesi ya Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge

Binamu kooona hawa ndio watu wa kuwatembelea. Ukawape dozi yako mjarabu
 
lissu-1-1.jpg


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Amesema amepewa nakala ya hukumu kutoka Mahakama Kuu iliyotupilia mbali rufaa yake namba 42 ya mwaka 2019 iliyowashitaki yeye (Spika ) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu ubunge wa Singida Mashariki.

“Nimepata nakala ya hukumu, Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikuwa wameshitakiwa na Bwana Tundu Lissu katika shauri la Mahakama Kuu namba 42 la mwaka 2019 ya kwamba Mahakama imetupilia mbali madai hayo tena kwa gharama kwa hiyo wajiandae kulipa,” amesema Ndugai.

Lissu alifungua kesi hiyo akipinga kuvuliwa ubunge wake wa Singida Mashariki ambalo kwa sasa linaongozwa na Miraji Mtaturu kutoka Chama Cha Mapinduzi.


Source: GlobalPublishers
Stupid Ndungai.

Corona ngoja ifanye mambo titakuja kuongea badae..
Every one ia exposed including me
 
Kesi afungue Lissu, gharama walipe CHADEMA. Wale wahujumu uchumi wote ni wanachama wetu wa CCM, kesi zao Chama kimewalipia?
Kama Nchi hii ingekuwa inafuata maadili ya Uongozi, Taifa lisingekuwa na Spika aliyepatikana kwa kumpiga mwenzake na gongo kichwani mpaka akazirai. Huyu alipaswa asipewe hata nafasi ya kugombea Ubunge.
Bahati mbaya Chama chetu kiliondoka na Hayati Baba wa Taifa. Waliobaki ni wapigaji tu katika hadhi tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo bila shaka ni maagizo kutoka kwenye remote control iliyojificha kule chattle.
 
Huyu jamaaa ni Maskini sana wa Roho.
Huwaga anahisi Pesa ndio kila kitu
Mara ataje Madeni ya Wabunge wa CHADEMA,mara aseme watanyimwa Posho,mara aseme warudishe Posho.
Ukiona mtu anaweka pesa mbele kwa kila kitu hata Masuala ya utu ujue ni Maskini wa Roho na ana Roho Mbaya.
Akizeeka sana usiniulize atakuwa nani___sema tu atakuwa mchawi bana😁😁

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hivyo mnaisingizia mahakama na mahakimu sema mwenyekiti wa chama Cha Ndugai katoa hukumu.
 
Back
Top Bottom