Spika Ndugai: CHADEMA wajiandae kulipa gharama za kesi ya Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge

Spika Ndugai: CHADEMA wajiandae kulipa gharama za kesi ya Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge

Mmeifanya Tanzania kama family yenu na jiwe munakua waamuzi wa kila kitu lakini mkumbuke madalaka yana mwisho
 
Spika wa kufuatilia na kuku
lissu-1-1.jpg


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Amesema amepewa nakala ya hukumu kutoka Mahakama Kuu iliyotupilia mbali rufaa yake namba 42 ya mwaka 2019 iliyowashitaki yeye (Spika ) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu ubunge wa Singida Mashariki.

“Nimepata nakala ya hukumu, Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikuwa wameshitakiwa na Bwana Tundu Lissu katika shauri la Mahakama Kuu namba 42 la mwaka 2019 ya kwamba Mahakama imetupilia mbali madai hayo tena kwa gharama kwa hiyo wajiandae kulipa,” amesema Ndugai.

Lissu alifungua kesi hiyo akipinga kuvuliwa ubunge wake wa Singida Mashariki ambalo kwa sasa linaongozwa na Miraji Mtaturu kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Spika ndiye mkusanya gharama za kesi zinazoamuliwa mahakamani?Je,mtu akikata rufaa shauri linakuwa na gharama kiasi gani likitupwa na mahakama?
 
Hivi chadema wakisema walipwe gharama za kesi walizoshinda serikali si hii nchi itafirisika. Huyu lisu ameishinda serikal mara ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaomba copy/nakala ya hukumu na gharama husika tulipe mara moja. Mnajiona mmeshika mpini kuwa manaweza kumkata kila mtuu. Sisi tutachangia hizo mia tano tano kumaliza mchezo. Ila ukweli unajulikana kuwa ardhi tunayo kanyaga ni ya Mwenyezi Mungu na yatupasa kuikanyaga kwa adabu na kwa unyenyekevu mkubwa
Lisu si ali appeal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom