Spika Ndugai: Kwenye majadiliano ya mikataba ya kimataifa tusipeleke watu waliopata makarai "O" level "A" level na Chuo kikuu

Spika Ndugai: Kwenye majadiliano ya mikataba ya kimataifa tusipeleke watu waliopata makarai "O" level "A" level na Chuo kikuu

Ameongea jambo la maana sana . Ingekuwa vizuri tungeanza na sheria za bunge ingekuwa sifa hizohizo anazotaka wengine wawenazo wakati wa kufanya mikataba ndizo ziwe kigezo cha kupata speaker bora. Tusiwe tunaokoteza maspika mwisho wa siku tunapata sheria mbovu
 
Mimi nimemuelewa spika...last time I checked, RCs huwa hawaendi kufanya negotiations Kwa niaba ya Nchi...labda kwenda kushangilia kabumbu.
 
Point mkuu wapo wa vyeti siyo uelewa mdogo sana
Etii??? amesahau ya kwamba siku hizi kuna degree na first class nyingi tu za chupi, wasomi wengi huko wanajua kukariri lakni kwenye kupambanua mambo ya msingi ni weupe yaani unaona bora hata raia wa kawaida wa mtaani wanaweza jenga hoja na kutetea hoja tofouti na hao wanoitwa vipanga wa chuo kikuu.
 
Mkuu Ndugai hopeless kabisa ,Kupata karai na uwezo wa kunegotiate ni vitu viwili tofauti,tena hao waliopata ma A ya kutosha ndio mambulula linapokuja swala hilo ndio maana kina chenge pamoja na kusoma Havard lakini alituingiza MKENGE kwenye mikataba ya RADA.
 
Many successful people hawajui hata division ni nini, lakini ukiwaweka kwenye negotiations wana skills ambazo wenye division one hawana.
Akili ya kunegotiate haihitaji Division - Mbona walioiuza nchi hii ni wasomi wazuri tu!
 
Tuanze na bunge; Wajumbe wengine wa Kamati za bunge ni vilaza
 
Ndugai aanzie bungeni hivi Mbowe aliyepata division zero form six anastahili kweli kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni?

Amwondoe huo wadhifa Mbowe
 
Ndio maana amesema O level na A level wawe na division 1......uwe unaelewa!
Kupata division katika masomo sio kua huyu mtu anakua smart katika negotiations nk ingekua hivyo basi watu wenye division na first class ndo wangekua matajiri na wenye kutoa ajira Duniani!
 
Lakini pia hii sifa ya kujua kusoma na kuandika Kiswahili na Kingereza ife kabisa katika kugombea nafasi ya ubunge. Kigezo iwe ni Shahada ya Chuo Kikuu kinachotambulika
 
Mbona raisi anayewateua na ye amefelifeli tu elimu yake ya kuunga unga tu,

Hivyo vigezo vitimike na kwa wanasiasa ili tuepukanecna viobgozi vilaza
 
Kauli hii imetolewa bungeni leo na Spika Job Ndugai.
Kimsingi kuna hoja ya msingi, lakini je, ni nani anayepelekewa ujumbe huo?
Of course, sisi wananchi tumekusikia .
Mbowe uyo ziro
 
leo ndio anayaona hayo? siku zote alikuwa wapi asishauri hadi tukaingia mikataba ya kishezi kabisa.
 
Mtu anaweza kuwa na A's kibao lakini hofu ya Mungu, uadilifu na uzalendo ana sifuri. Vigezo vya kwanza viwe ni uadilifu, hofu ya Mungu na uzalendo; elimu (A's) ifuate baadaye! Mh. Ndugai anajua wazi kwamba kuna watu wenye A's kuanzia primary school hadi Havard University lakini wameliingiza taifa kwenye majanga makubwa.
 
Hivi mimacho yeye ana ngapi
Aliwapeleka Ikulu masela fulani kutoka mitaa ya Kibera akawatambulisha kama wanunuzi wa Korosho. Masela wakala pioi zetu pale ikulu then wakarudi zao kubera kuendelea kuoiga watu roba za mbao.
 
Back
Top Bottom