Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,332
- 10,911
Etii??? amesahau ya kwamba siku hizi kuna degree na first class nyingi tu za chupi, wasomi wengi huko wanajua kukariri lakni kwenye kupambanua mambo ya msingi ni weupe yaani unaona bora hata raia wa kawaida wa mtaani wanaweza jenga hoja na kutetea hoja tofouti na hao wanoitwa vipanga wa chuo kikuu.
Hivi unaijua First Class lakini wewe.
Unajua mpaka mtu anapata First Class atakuwa amefaulu kozi zisizopungua thelasini na sita (36) kwa kiwango cha A na B+ huku Grade A zikiwa nyingi zaidi.
Hivi unajua kozi hizo zaidi ya thelasini na sita kwa miaka mitatu mpaka mitano kutegemeana na Faculty zinafundishwa na Wakufunzi(huenda ni Madokta au maprofesa) Tofauti tofauti. Hivi unalijua jambo hilo?
Au unadhani kozi zinafundishwa na mwalimu mmoja au wawili. Kama umefika chuo ninaimani Uliona. Maprofesa na madokta tofauti wakifundisha masomo tofauti tofauti. Japo wapo wanakufundisha mwaka wa kwanza na ukamuona tena kwenye kozi ya mwaka wa tatu.
Sasa mtu mpaka anapata First Class ya chupi. Unafikiri atakuwa ametembea na Madokta wangapi.
Mkuu First Class iache iitwe First Class. Huwezi kuipata kirahisi nakuhakikishia hata uvue lichupi lako.
Sikatai kuwa hakuna wanaovua chupi kupewa marks za bure lakini sio kwa level ya First Class.
Mimi nina GPA 4.3 lakini mziki wake usipime. Wamawake waliopata GPA kuanzia 4+ hasa vyuo vikubwa kama UDSM, SUA, MZUMBE, MUHAS n.k. Usiwachukulie poa.
Alafu unasema ni degree za chupi. Na wanaume wanaozipiga nao wamevua chupi?
Au ndio kuwadhalilisha wanawake na kuwaona hawana uwezo wa kupiga First Class.
Nakuhakikishia, Huwezi pata First Class kwa kuvua chupi. Niamini mimi.
Hiyo tu Second Upper Class (SUC) Inaweza usipate.