Spika Ndugai: Lissu kwa miaka 10 ya Ubunge hakuna 'legacy' yoyote aliyoacha Jimboni kwake

DC wa CCM, DED wa CCM, RC wa CCM, Waziri wa CCM, PM Wa CCM VP wa CCM na Rais wa CCM, Kwanini hawajapeleka maji kwenye hicho kijiji?!
Unafaidika nini kutetea ujinga?
 
Ndugai ana 25 Kongwa kama mbunge lakini kongwa yenyewe haina, maji, barabara, wala madawati.
Hiki ndiyo sababu iliyomfanya Lisu asipeleke maji kijijini kwake?
 
Ndugai ana 25 Kongwa kama mbunge lakini kongwa yenyewe haina, maji, barabara, wala madawati.
Tumsamehe tu huyu bwana kwani yaelekea kila siku anakuwa na ndoto kumkumbuka mwendazake na hizo ni maongezi ya ndotoni akiwa na mwendazake.
Nakumbuka kuna wakati furani walichangisha michango pale mjengoni karibu Mil 200 kwenda kuangalia Taifa stars wakati wa mashindano ya Kombe ya mataifa, lakini cha ajabu ama cha kusikitisha baada ya wiki chache akaja kuomba msaada wa bati kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya choo jimboni kwake kutoka kwa mwendazake ambaye kipindi hicho alikuwa ziarani katika jibo hilo la bwana Job.
 
Ni aibu sana kwa nchi kuwa na viongozi aina ya Ndugai
 
Nguvu aliyotumia kutetea acacia kwa nini hakutumia kutetea wapiga kura wake?
Ccm imetawala kwa miaka 60 sasa na nchi ndivyo ilivyo hivi na unashindwa kuilaumu unawalaumu wale wahanga wake ni kuonyesha ni jinsi gani ulivyo na fikra finyu.
 
Hali halisi kongwa ikoje?
 
Sasa ndiyo mumpige RISASI??
 
Hivi huyu bwana hana kazi nyingine hapo Bungeni? anahangaika tu ooh Mbowe ooh Lema ooh Lisu , huyu jamaa vipi? kwakweli hapa tumepatikana , mambo yamaana hayaguswi hata kidogo hii ni takataka kabisa
Hawa Jamaa hawapo Bungeni lkn vivuli vyao vinamtesa Ndugai. Kuna siku huyu Ndugai ataropoka zaidi hadi kutamka kwa kinywa chake mwenyewe ni jinsi gani alivyoshiriki jaribio la Mh Lissu kupigwa risasi.
 
Ccm imetawala kwa miaka 60 sasa na nchi ndivyo ilivyo hivi na unashindwa kuilaumu unawalaumu wale wahanga wake ni kuonyesha ni jinsi gani ulivyo na fikra finyu.
Ccm kutawala kwa miaka 60 ndiyo sababu ya Lisu kuacha kutetea wapiga kura wake?
 
Ukimsikiliza huyu mzee unaweza hisi ni mtu wa maana sana jinsi anavyopanga maneno ila ukitafakari kimtokacho ni kama kusikilizia ushuzi wa dengu unavyopalia ndani ya shuka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…