Spika Ndugai: Mnaogopa nini kuleta viambatanishi ili tuwavue Ubunge kwa Haki?

Hili suala limemtia doa sana Ndugai sasa anabaki kutapatapa tu ila kiukweli ndani ya nafsi yake anajua anachofanya siyo sahihi

Sisi kazi yetu kumkumbusha huu utaratibu mpya umeanza kwa suala la hawa 19 tu vipi kwa Sophia Simba, vipi kwa wale wa CUF wote walifanyiwa hivyo ha ha ha Ndugai acha kujitia wazimu bana

Kwanza ungewauliza hao wabunge uhalali wa kikao kilichowapitisha wao kuingia huko bungeni maana KM wa chama chao amekiri hakufanya hivyo na hata tume walikiri pia kuwa CDM hawakupeleka majina sasa usitake kuliacha hili ambalo ni la muhimu utake la kuwafukuza, hoji walifikaje huko kama kweli wewe ni mtenda haki, mtumia busara, mfata sheria taratibu na tamaduni

Mwishowe najua tu utakubali hili suala uliingizwa mkenge na kwa presha unayoipata mwisho utasalimu amri tu
 

Kwanza uchaguzi mnautambua kuwa ulikuwa huru na haki?
Tuanzie hapo kwanza
 
Wao wanachosema ni kuwa waliwatimua uanachama sasa uandishi wa mihtasari ni mambo ya katiba ya chama yeye inamhusu nini
Kutimua ni lazima kukidhi matakwa ya katiba ya chama na sheria ya vyama vya siasa
 
Nina Swali la kumuuliza Job:
“Condom inatumiwa baada ya mimba kuingia?”

Hizo taratibu zake anazitunga baada ya miezi 6, mimba ni pevu? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ni mambo ya KITOTO!
 
Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke.

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao.
Hata kama wamekosea, ajibu barua kwa maandishi. Haya mambo ndiyo hufanya watu kufurahia akigeuka mwendazake kwa kuitwa na Mungu
 
Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke.

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao.
Umeishia darasa la ngapi?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Wewe haya mambo yako juu ya uwezo wako,

Ulishawahi kuwaza kama kuna siku Lisu na chadema nzima watampigia makofi Lowasa, Sumaye na Nyarandu?

Kabisa. Uliyeshangaa ni wewe. Unadhani Chadema wangepata wabunge na kura walizopata kama wangemsimamisha Slaa? Kumbuka hizo kura ndizo zilizowawezesha kujenga chama. Na baadae uamuzi wao ukathibitishwa kuwa ulikuwa sahihi baada ya Slaa kuhamia CCM. Sumaye na Nyalandu walikuja wenyewe na wameondoka wenyewe. Wote walikuwa na mvuto wao ambao ulitumika kujenga chama. Wameondoka lakini wale waliowavuta bado wapo kwenye chama.

Hivi unadhani leo Mbowe au Lissu wakiomba kujiunga na CCM, CCM watawakatalia? Mbona wamewapokea vizuri tu wakina Silinde, Waitara, Lijualikali, Halima nawengine ambao walikuwa wakiwatukana hivi karibuni?

Najua najisumbua kukufahamisha maana yote haya yako juu ya uwezo wako wa kufikiri.

Amandla...
 

Spika katunga utaratibu wa kutakiwa kuambatisha Katiba na minutes za kikao husika leo, miezi mitano baada ya kupelekewa barua. Kwa kufanya hivyo, anakiri kuwa wakati anaandikiwa barua na Mnyika matakwa haya hayakuwepo. Na kama ameweza kufanya hivi, kitu gani kitamzuia kutunga utaratibu wa kiambatishi cha picha na vyeti vya kuzaliwa vya wajumbe wa Kamati Kuu iliyofanya maamuzi haya?

Mbona anatufanya wote wajinga?

Na wabunge wake wanampigia makofi.

Suzana kweli sio mtu mzuri.

Amandla...
 
Huyu mzee anazeeka vibaya, na analipeleka bunge pabaya, nje kufukuzwa na chama ,wamefoji ,hawajawahi teuliwa na chama so wamefanya ujangili, kwamba nalo hajui, why anajiondolea heshi, hakuna kupeleka nakala ya katiba Wala mhutasari anatafuta kichaka Cha kujificha , bali ni kupambana nae tu hivyohivyo ,hawezi fanya watz mil 50 WOTE ni wajinga , tumechoka sasa
 
Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke.

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao.
Acha ujinga,Sofia Simba alipofukuzwa Ndogai mbona hakumwambia mwendazake apeleke viambatanisho.
 
Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke.

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao.
Barua yenyew imepita miezi mitano hajajibu na kaita kipeperushi? Je CCM walipomfukuza Sophia Simba 2017 walipeleka vielelezo?
 
Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke.

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao.
swala la chadema waekosea wapi au akidi haijatimia sio lake hio ni issue ya MAHAKAMA . kageuza ofisi ya UMA kua ofisi binafsi anajipangia atakalo
 
Kweli wewe ni Iboya, akili za lumumba hizi ni hatari kwa nchi
 
Hivi ili bunge NDUGAI ajiona mali yake na kalijenga KWA kutoa pesa yake mfukoni, tupo na Mungu yupo, itajulikana sio mda nani mkweli Kati ya Ndugi na Chadema ,Yani mnakua wahongo mpaka shetani anawaogopa ,
 
Pelekeni sasa hivyo vielelezo sio mnakuja kupiga makelele hapa
Hakuna cha vielelezo,kweli wew mgogo.Ni kanuni au sheria ipi inayotaka hivyo vielelezo?Ujeuri wote wa hilo jamaa lenu limevimba sura km nguruwe wa kwetu unatokana na katiba anayoidharau,unafikuri tunawafundisha nin wananchi tunapodharau katiba?Hivi unajua Ndugai nje ya katiba ni mtu wa kawaida hana ujeuri na hawez kuamrisha?Askari wake na wasaidize wote wampuuze kwa kudharau katiba unafikiri itakuaje?
 
Ndugai anajiamini sana inaonekana kuna kitu anakijua na mkiendelea kumtukana kuna siku atakisema.
Ndugai kauliza swali dogo tu “wanaogopa nini kuambatanisha documents?”

Jibu pekee ni kuandika barua na kuweka hizo necessary attachments badala ya kukwepa, kupanga maandamano na kumtukana Ndugai. Ni bora kuabide ili mwisho wa siku Ndugae akose options.
 
Wapinzani wanachelewesha maendeleo, sasa hao wadada mnawakatalia wa nini?

Hawa COVID 19 WAMETOSWA TOKA DAY ONE Wala sio leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…