Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Naanza kuamini kwamba mgogo haaminiki hata kidogo. Huyu mzee anawaaibisha sana wenzake
 
Hahahaha
Nimeanzisha mada inayolenga uchambuzi kwq mlengo mwingine lakini moderators wanaiunganisha na ya press release.

Wazeeiya hizi hasira kazini si nzuri.
 
Nimeifuatilia Press ya Ndugai leo nimeona mada zilikuwa tatu

1. Kutangaza siku ya Maombi ya Bunge tarehe 29 Jan

2. Kuanza kwa kamati za bunge ambapo tarehe 09 Jan ni kamati ya ukimwi na kamati nyingine ni tarehe 16 Jan na

3. Kumuomba radhi Rais japo wakati wa kuomba radhi yametumika maneno ambayo msamaha kaombwa Mungu tena kwa lugha ya kanisani na Watanzania sijasikia akiombwa Rais.

Swali ni Je lengo Mahsusi la Press ilikuwa nini? Msamaha au ratiba ya Bunge? Je siku za nyuma kulikuwa na Press za kutupa ratiba ya Bunge au la?

Kama ni msamaha mbona umechelewa kuombwa na kuunganishwa na matukio mengine? Kama mkutano wa Bunge ni tarehe 6 kwanini ratiba tusingepewa siku nyingine au tupewe hata press release ili msamaha usimame peke yake?
 
Wakuu
Hii press ya Job leo unaichambuaje?

Je, Ndugai & The Gang walikuwa wanaupima upepo?

Je, wananchi ama wanaharakati wangeonesha kumuunga mkono angefanya hii submission press ya leo?

Thinkers wa JF, mnaiangaliaje hii move ya Ndugai kuomba radhi hadharani leo akiwa kama mkuu wa Mhimili huru wa Bunge? Jambo hili limekaaje
Kisiasa
Kiusalama
Kidemokrasia

Pascal Mayalla
Mshana Jr
figganigga
Mzito Kabwela
Mchambuzi87
Mi ni fan wa JPM nashangaa unavyomweka Ndugai kwenye kambi ya JPM. Ndugai huyu aliyepigia debe bandari ya Bagamoyo kwa wachina atakuwaje kwenye kambi ya Magufuli?

Ndugai, Nape, na wale jamaa wote wa aina zao ni opportunists tu watakaofanya lolote ili mkono uende kinywani. Rais awe makini sana na hawa watu.
 
Japo sijaalikwa kuchangia ngoja nimwage kapumba kangu kiduchu...

Bwana Job hakuwa na nia ya kuomba msamaha. Angekuwa na nia hiyo asingechukua muda mrefu hivyo. Siamini pia kama ni ushauri wa maswahiba zake wala presha ya maadui zake....

Naamini kapigiwa simu moja kutoka mamlaka za juu (labda za ulinzi na usalama) na kumshauri afanye hivyo au aachie ngazi

CDF akimpigia simu na kumwambia sijafurahi namna unavyolumbana na bosi wangu... Amiri Jeshi Mkuu wangu.... sidhani kama Job angekuwa na namna tena.

Maana ukubwa bado anautaka na kuupenda.

Hii kwa mama imemjenga sana kisiasa. Hivi sasa anasubiria awe hai 2025 achapishiwe form yake pekee ajaze akagombee muhula wa pili.

Hamna wa kumzuia tena
CDF haingilii mambo yao ya siasa aisee hii malumbano huwa hahusiki kabisa anakaaga pembeni kama hawaoni Ila akiona wamezidi yeye hupeleka kikosi ikulu kwamba Sasa naona nchi inawashinda kuendesha wacha niwasaidie.

CDF sio kama unavyomchukulia aisee. Huyo huwa haongei siasa kabisa, muulize Nyerere aliyekumbana na CDF aliyempelekea wajeshi ikulu maana wanadai mishahara yeye alikuwa analeta siasa. Walimnyoosha akamalizana nao fasta kabla hawajalianzisha mtaani.
 
Hahahaha
Nimeanzisha mada inayolenga uchambuzi kwq mlengo mwingine lakini moderators wanaiunganisha na ya press release.

Wazeeiya hizi hasira kazini si nzuri.
Binafsi hata mimi nimeshangaa kwanini wameuunganisha
 
Mi ni fan wa JPM nashangaa unavyomweka Ndugai kwenye kambi ya JPM. Ndugai huyu aliyepigia debe bandari ya Bagamoyo kwa wachina atakuwaje kwenye kambi ya Magufuli?

Ndugai, Nape, na wale jamaa wote wa aina zao ni opportunists tu watakaofanya lolote ili mkono uende kinywani. Rais awe makini sana na hawa watu.
Je unaweza kufafanua wapi nimemtaja Ndugai kama JPM follower au team?
 
Nimesikiliza mwanzo mwisho maelezo ya Ndugai, kiukweli huyu jamaa is an idiot. Anafikiri watu wote wana akili za kitoto kama yeye. Nadhani ugonjwa wake umeingia kwenye mfumo wake wa ubongo. Kwanini hakuongelewa kuwachukulia hatua waliopotosha kauli yake. Wabunge lazima muone aibu kumuita huyu idiot , spika wenu.
 
Si mara ya kwanza leo.

Lakini nimeona niseme kidogo kufanikisha furaha yao
 
Naanza kuamini kwamba mgogo haaminiki hata kidogo. Huyu mzee anawaaibisha sana wenzake
Kweli kabisa katia aibu afadhali angebaki na msimamo wake.

Kwa maana hivyo amekitia aibu kiti cha Spika kwamba Spika ni mlopokaji mpaka anaamua kuomba msamaha kwa mhimili wenye hadhi kama wa kwake. Basi kile kiti hakimfai mpaka anaamua kukopoka bila kupima impact ya maneno yake kwenye jamii.

Njaa mbaya sana!!😆😆😆😆
 
What a cuck ending,😂😂..
Kweli hayati alikua sahihi kusema kuna muhimili mmoja umejichimbia ndani na una ukubwa kidogo kuliko mengine...Yani kiongozi wa muhimili mmoja unaomba msamaha😂😂.hii ni walk of shame...basi Rais anafaa kuburuza hii nchi,,syllabus za masomo ya uraia zirejewe...
 
Je tuamini Political Desk wamefanya yao?
Kumbe hata mimi naweza kuwa spika.
 
Nimeifuatilia Press ya Ndugai leo nimeona mada zilikuwa tatu

1. Kutangaza siku ya Maombi ya Bunge tarehe 29 Jan

2. Kuanza kwa kamati za bunge ambapo tarehe 09 Jan ni kamati ya ukimwi na kamati nyingine ni tarehe 16 Jan na

3. Kumuomba radhi Rais japo wakati wa kuomba radhi yametumika maneno ambayo msamaha kaombwa Mungu tena kwa lugha ya kanisani na Watanzania sijasikia akiombwa Rais.

Swali ni Je lengo Mahsusi la Press ilikuwa nini? Msamaha au ratiba ya Bunge? Je siku za nyuma kulikuwa na Press za kutupa ratiba ya Bunge au la?

Kama ni msamaha mbona umechelewa kuombwa na kuunganishwa na matukio mengine? Kama mkutano wa Bunge ni tarehe 6 kwanini ratiba tusingepewa siku nyingine au tupewe hata press release ili msamaha usimame peke yake?
Hata mie nimemfuatilia Ndungai, hakika hajaomba msamaha kwa rais kwa sababu radhi hiyo haipo kimaandishi tena haikufanyika ktk ofisi ya rais.

Job asiwadanganye wazanzibar bhana 😄
 
Press ya leo nikajua anakuja kumtangaza mnunuzi wa nchi[emoji1]
 
Back
Top Bottom