Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu".

"Nafikiri labda tuongeze kodi labda itapunguza hata sijui, hivi tufanye kitu gani ili tuhakikishe kila mtu anafanya kazi, maafisa maendeleo ya jamii hawafanyi kazi" -Job Ndugai.

Nini maoni yako mdau?

----
NDUGAI: NCHI INAKWENDA IKIWA NA KUNDI KUBWA LA WATU WAVIVU

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kwa sasa japokuwa Nchi inakwenda na Uchumi wa Kati lakini kuna kundi kubwa la watu wavivu huku Vijana wakijikita zaidi kwenye kucheza 'Pool table'

Amefafanua kuwa, Watanzania wengi hawajitumi katika kufanya kazi na hata ubovu na uvivu wa Timu ya Taifa ndiyo sababu kubwa ya #Tanzania kushindwa katika mashindano ya Kimataifa

Ndugai ametoa wito kwa Wabunge kutafakari ikiwa Elimu inayotolewa Mashuleni inawajenga Wanafunzi kwasababu wengi wakishamaliza Kidato cha 4 wanaona kazi za kushika Jembe kuwa ni Utumwa.
 
Dah! Maskini Tanzania yangu. Yaani haoni kabisa ajira hakuna na fao la kujitoa walilifuta. Rudisheni basi fao la kujitoa ili tujiajiri maana serikali uwezo wa kufikiri umefikia kikomo. Nilisema serikali ipo nyuma ya vifurushi vya mitandao ya simu kupanda.
 
Nimeendelea kusoma mpaka chini nione alivyoishauri serikali nini cha kufanya kuondokana na hilo tatizo ajabu nilichoambulia anataka serikali iongeze kodi!

Hii inathibitisha jinsi CCM na viongozi wake walivyochoka akili zao, hawawezi tena kulipeleka mbele hili taifa.

Yaani kijana aliehitimu chuo akakosa ajira akijibana akaanzisha biashara yake ya pool table, jamaa wanawaza kumuongezea kodi, hii ni laana.
 
Ndugai ni janga la taifa. Inaonekana dhahiri hajui jinsi kanuni na falsafa za uchumi zinavyofanya kazi.

Juzi tu hapa alipendekeza walimu wafundishe masomo matatu bila kujua kwamba kinacho gomba hapa ni idadi ya vipindindi kwa siku na siyo masomo ambayo mwalimu anafundisha.

Leo anajitoa ufahamu kudhani kwamba vijana wanaoshinda vijiweni wanapenda bila kujua kwamba hakuna fursa za wao kutumika.

Hajui kwamba serikali inatakiwa ifungue fursa za watu kufanya kazi.

Amesahau kwamba serikali yake imeleata mifumo ya ajabu ajabu ambayo inaua private sector.

Amesahau kwamba kujiajiri kunahitaji mtaji, ujuzi na uzoefu ambao vijana wengi hawana.

Amesaha kwamba mfumo wa serikali kufanya biashara yenyewe kwa yenyewe inapunguza uwezo wa sekta binafsi kushamiri.

Amesahu kwamba force account ambazo wanatumia kwenye ujenzi zinaondoa makandarasi wazawa kwenye ujasiriamali.

Amesahau kwamba fao la kujitoa ilikuwa ni kichocheo cha watu kuacha kazi na kujingiza kwenye ujasiriamali kati age ya 40-54 year. Ambao waliweza kuajiri vijana.

Anajisahaulisha kwamba ubinywajinwa sekta binafsi na kubambizwa kodi kunapunguza uwezo wa sekta binafsi kuajiri.

Anajisahaulisha kwamba Taasisi zinazoitwa za udhibiti zina dhibiti uanzishwaji wa biashara mpya kwa kuweka vigezo visivyo kuwa na uhalisia kwa wajasiriamali ambao wanata kuingia kwenye biashara.

Anajisahaulisha kwamba uwezo wa bank kutoa mikopo umepungua baada ya wafanya biashara wengi kushindwa kulipa mikopo kutokana na sera mbovu.

Anajisahaulisha kwamba sera mbovu na zisizo tabirika zinawafanya wawekezaji kutoka nje kuto wekeza nchini na hivyo kutotoa ajira kwa vijana.

Amejisahaulisha kwamba watu wamehamisha mitaji yao kutokana na visasi vya serikali na hivyo kupunguza ajira.

Ongezea.
 
Ndugai ni janga la taifa. Inaonekana dhahiri hajui jinsi kanuni na falsafa za uchumi zinavyofanya kazi.

Juzi tu hapa alipendekeza walimu wafundishe masomo matatu bila kujua kwamba kinacho gomba hapa ni idadi ya vipindindi kwa siku na siyo masomo ambayo mwalimu anafundisha...
Mkuu kwa ukipofu alionao hajui hili.

Anatamani vijana wote wafe ili awe mbunge wa maisha wa kupita bila kupingwa.
 
Leo nimejifunza kitu. Kazi ya Afisa Maendeleo ya Jamii ni kuhakikisha kila mtu anafanya kazi. Kwa vile hao Maafisa Jamii hawafanyi kazi zao kama ajira yao inavyowaelekeza, basi watu wengi wanaishia kucheza pool toka asubuhi hadi usiku. Ili kuondokana na hili tatizo, Zumbe Mkuu atawashauri na kuwaagiza Wazumbe wengine kupandisha kodi ya hizo pool. Kodi ikipanda wacheza pool wataacha kucheza mchezo huo na kuanza kufanya kazi.
 
Watu wengi wanaofanikiwa wanatokea kwenye mazingira haya haya miaka nenda rudi wengine wanalalamika maisha magumu Vijana wengi wa kitanzania ni wavivu kuna Makundi mengi ni tegemezi hawataki kujishughulisha mfano hawa vijana wanywaji wa pombe za kienyeji ,watumiaji wa Instagram,vijana wa kubeti nk
 
Watu wengi wanaofanikiwa wanatokea kwenye mazingira haya haya miaka nenda rudi wengine wanalalamika maisha magumu Vijana wengi wa kitanzania ni wavivu kuna Makundi mengi ni tegemezi hawataki kujishughulisha mfano hawa vijana wanywaji wa pombe za kienyeji ,watumiaji wa Instagram,vijana wa kubeti nk
Unadhani wanapenda?Hebu kafanye utafiti vizuri. Hadi watu kufikia hatua ya kunywa urabu wanakuwa wamekata tamaa.

Kuna descouragement nyingi sana katika nchi hii. From kukamatwa mifugo hadi kukatwa kwa mazao yaliyoko shambani.

Yaani kuna ile kila unapojaribu kufanya kitu, kuna mtu anajiita afisa wa serikali anakwambia umevunja sheria. Anataka ulipe faini kubwa kuliko hata thamanni ya kila kitu unachomiliki hapa duniani.

Kama hayajawahi kukukuta shukuru mungu.
 
Atoke Bungeni aje aonyeshe mifano mtaan wakujiajiri kwann kila muhula wanapgania ubunge.
Ukomo wa ubunge unapaswa uwepo. Mbunge akitumikia miaka 10 au awamu 2 inatosha kabisa. Wapishe wengine wenye experience za mtaani kama wanao-comment.

Hii mtu anakua mbunge miaka 15 hadi 20 si sawa kabisa. Kwanza analipwa hela nyingi huku akitoa mchango wa kipuuzi kama huu wa Ndugai. Pili anabweteka yan it’s like liwalo na liwe while wanaoteseka ni raia wa chini kabisa
 
Back
Top Bottom