Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Kuna tofati kubwa kati ya kazi na shughuli, kucheza pool na kuperuzi sio dhambi. Kuto isimamia Serikali na Bunge kutunga sera nzuri za kiuchumi zitakazo tengeneza fursa nyingi za ajira ni ubinafsi na kukosa uzalendo.
 
Kama spika huu ndio upeo wake alafu eti mnategemea maendeleo, "Bunge ni dhaifu "
 
Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu".

"Nafikiri labda tuongeze kodi labda itapunguza hata sijui, hivi tufanye kitu gani ili tuhakikishe kila mtu anafanya kazi, maafisa maendeleo ya jamii hawafanyi kazi" -Job Ndugai.

Nini maoni yako mdau?
Mwambieni aturudishie viwanda walivyojiuzia pengine ajira zitapatikana.

Wakishiba wanatutaapikia.
 
Tumsome mwanafalsafa hapo
katikazaemmanuel_20210209_085223_0.jpg
 
Mwambieni aturudishie viwanda walivyojiuzia pengine ajira zitapatikana.
Wakishiba wanatutaapikia.
Mh. Job Nduga spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania sikia na soma maoni ya wananchi wako tafadhali.
 
Ndugai kasema kweli na ukweli lazima usemwe vijana wanashinda mitandaoni huku wazee wakipiga pesa huku mashambani.

Kijana hivyo vyeti vyako siyo kuku kusema vitataga mayai uuze...ajira hakuna na sio Tanzania peke yake, dunia nzima hakuna ajira za kutosha kwa kila mhitimu! jiulize hizo ATM mashine za KUWEKA PESA mbazo baadhi ya mabenki hapa nchini wameanza kuzitumia zitameza ajira za wahitimu wangapi.

hebu jiulize kiwanda cha kutengeneza hizi cassete kilifungwa? Hapata kawakufunga bali waliamua kutengeneza bidhaa nyingine, kama wewe umeamua kusubiria ajira ukiwa Mod wa group la whatapps subiri kitakachokupata maana dunia hijawahi kusimama!

download.png
 
Vijana wanashinda mitandaoni huku wazee wakipiga pesa huku mashambani.
Kweli mkuu ila sasa nasema ila sasa.

Pamoja na kuwepo aridhi ya kuweza kulima sidhani kama ni rahisi kiasi hicho kwamba kijana/vijana watoke mjini na kuelekea huko mashambani.

Mfumo wetu bado haujawa rafiki kumuwezesha huyo unayesema msomi kujikita na kilimo cha msimu au kisasa!

Kuna wakati tuangalie mfumo na mustakabali wa taifa toka alipokuwepo 'our father of nation' wewe unakumbuka vile vijiji vya ujamaa na kujitegemea? Lengo lake lilikuwa ni lipi?, Ili kujua hilo inabidi usome kitabu kinachoelezea azimio la Arusha.

Na,
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametaja uvivu na ubovu wa timu kuwa sababu za Tanzania kushindwa katika mashindano ya kimataifa.

Spika Ndugai amesema uvivu unakosesha kuendelea mbele wachezaji kwani wakifika mbele hawajitumi kama ilivyotakiwa.

 
Ngoja nipaze sauti na mabeberu nao wasikie, "fiveee agaaaaaaain!!!"
 
Sasa ikiwa ajira rasmi ni chache na za kujuana kwanini watu wasicheze pooltable, kiufupi maisha ya sasa mtu akishaona walau ameingiza hela ya chakula kwa siku inatosha muda unaobaki anautumia kwa mambo mengine.
 
Watu wanaperuzi mitandao kutafuta fursa....
kazi,biashara nk.....
huyo jamaa anaishi dunia ipi!?
 
Ni kosa kwa kiongozi alipewa dhamana ya uongozi kutumia maneno "labda", "nahisi" na "sijui tufanye nini". Lazima tofauti kati ya kiongozi na muongozwa iwe wazi!! Tatizo la Bunge letu liko kikatiba zaidi, wakati nchi zilizoendelea mipango ya fedha hupangwa na Bunge au chombo chenye madaraka ya Bunge na kuipelekea Serikali kwa utekelezaji - hapa kwetu ni kinyume. Bunge ni rubberstamp ya maamuzi ya waziri, katibu mkuu na viongozi wengine!!

Moja ya vitu vinavyoua uzalishaji ni kodi kubwa, na hapa Spika anazungumzia "kupandisha kodi" ili kuondoa tatizo la "vijana kutokuzalisha". Haishangazi tena tuko hapa tulipo!!
 
Hao wanaoshinda kwenye simu na pool table wako wangapi? maana bado wapo maelfu ya Vijana wanahangaika kutafuta na ajira au mitaji ya kujiajiri lakini hawafanikiwi....hao nao wanawasaidiaje? au wanaoonekana ni hao wa simu na pool table tu na hao wengine ni invisible.
 
Back
Top Bottom