Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Siyo ukomo wa ubunge tu sekita zote ziwe na ukomo Kama ilivyo kwenye uraisi kuanzia ubunge, uwaziri, ukuu wa wilaya, mkoa maana ni sekita za kuleta amsha amsha alafu watoke waingie wengine. Na serikali kuu na taasisi hivyo hivyo zile zinazozidisha miaka sitini ziangaliwe upya Ili vijana wakatumike.
Sure. Watu kama Kimei, Walitakiwa wawe wametulia sasa lakini sijui wanapambania nini
 
Leo nimejifunza kitu. Kazi ya Afisa Maendeleo ya Jamii ni kuhakikisha kila mtu anafanya kazi. Kwa vile hao Maafisa Jamii hawafanyi kazi zao kama ajira yao inavyowaelekeza, basi watu wengi wanaishia kucheza pool toka asubuhi hadi usiku. Ili kuondokana na hili tatizo, Zumbe Mkuu atawashauri na kuwaagiza Wazumbe wengine kupandisha kodi ya hizo pool. Kodi ikipanda wacheza pool wataacha kucheza mchezo huo na kuanza kufanya kazi.
Halafu pool haiingizi hela, na kisha biashara ya pool kufungwa.
Na wale vijana watatafuta burudani nyingine ikiwemo madawa ya kulevya, viroba na bangi. (kwani bado mazingira ya kukiajiri yamejaa vurugu).
Baada ya muda tunapata mateja, vibaka , majambazi, maradhi na vifo vinavyotokana na ulevi haramu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Unadhani wanapenda?Hebu kafanye utafiti vizuri. Hadi watu kufikia hatua ya kunywa urabu wanakuwa wamekata tamaa.

Kuna descouragement nyingi sana katika nchi hii. From kukamatwa mifugo hadi kukatwa kwa mazao yaliyoko shambani.

Yaani kuna ile kila unapojaribu kufanya kitu, **** mtu anajiita afisa wa serikali anakwambia umevunja sheria. Anataka ulipe faini kubwa kuliko hata thamanni ya kila kitu unachomiliki hapa duniani.

Kama hayajawahi kukukuta shukuru mungu.
Kuna watu wanayasoma haya matatizo kwenye vyombo vya habari lakini hayajawahi kuwapitia angalau karibu.
Nimewai kuhangaika sana na dogo mmoja anauza nguo,, akawa analazimishwa kununua mashine ya efd bila kujali ukubwa wa biashara yake. Mwisho wa siku akafunga biashara. Lakini tukaenda kupambana tena wakamfungulia na kumpa muda.( hili la kumpa muda niloona angalau lilimfanya apumue)

Rekodi zinalazimishwa kwa kuumiza wanannchi,, anayekula mshahara wa baba yake hawezi jua haya.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
tatizo wamezoea kazi ni mpaka watu wote wakalime kuna kijana tuko nae kitaa ye anashinda saloon kakaa na simu yake lakni ana ml 15 kwenye sportpesa
 
Dah! Maskini Tanzania yangu. Yaani haoni kabisa ajira hakuna na fao la kujitoa walilifuta. Rudisheni basi fao la kujitoa ili tujiajiri maana serikali uwezo wa kufikiri umefikia kikomo. Nilisema serikali ipo nyuma ya vifurushi vya mitandao ya simu kupanda.
Vijana wanafuatilia jinsi nchi yao inavyoporomokea shimoni kupitia kinachofanyika hapo dodoma, vinginevyo wajitahidi kubadili hali ya mambo muda huu wa majeruhi.
 
Yeye kiongozi mwenyewe anasema hajui cha kufanya.

Kwa nini asiwe sehemu ya tatizo badala ya sehemu ya ufumbuzi wa tatizo?
Mimi nashangaa kwa sasa mjadala mkubwa duniani na kwenye baadhi ya bunge ni issue ya covid hapa kwetu hizo ndiyo akili zilipoishia.

Wanajua wapiga kura wao wanateketea ila wote nahisi wanaogopa.
 
Waongeze kodi!!? Hivi hawa huwa hawasomi historia? Hiyo kauli inatofauti gani na Malkia wa Ufaransa ambaye baada ya watu kulia kuwa hawana mikate akawaambia kama hawana mikate wale keki!!?.

Mtu hana ajira halafu unamuongezea kodi?!
Marry Antoneitte
 
Watu wengi wanaofanikiwa wanatokea kwenye mazingira haya haya miaka nenda rudi wengine wanalalamika maisha magumu Vijana wengi wa kitanzania ni wavivu kuna Makundi mengi ni tegemezi hawataki kujishughulisha mfano hawa vijana wanywaji wa pombe za kienyeji ,watumiaji wa Instagram,vijana wa kubeti nk
Nakushauri kaombe special seat bungeni
 
Huyu jamaa vipi, yeye bungeni anakaa kufanya nini? kama si kupigwa kiyoyozi cha bure tu huku analipwa mamillion.
 
Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu".

"Nafikiri labda tuongeze kodi labda itapunguza hata sijui, hivi tufanye kitu gani ili tuhakikishe kila mtu anafanya kazi, maafisa maendeleo ya jamii hawafanyi kazi" -Job Ndugai.


Nini maoni yako mdau?
Taifa halina mpango wowote ule kwa vijana wa rika la 18 - 30 ambao hawana nafasi ya formal education.

Hawa wanatakiwa wawe vyuo vya ufundi...hawa wanatakiwa wawe kwenye mashamba makubwa ya irrigation scheme.

Ndiyo maana mnaagiza Ngano, mafuta ya kupikia, sukari wakati ardhi mnayo...nguvu kazi ndiyo hiyo, maji kibao yanatiririka nchi nzima afu spika na yeye analialia eti hajui cha kufanya.

Bil 500 tu zinaweza kuigeuza Tanzania, yaani ni pesa ya Dreamliner 2 tu.
 
Unadhani wanapenda?Hebu kafanye utafiti vizuri. Hadi watu kufikia hatua ya kunywa urabu wanakuwa wamekata tamaa....
Hii nchi ya hovyo sometime wakati nataka kufungua Maabara ilinichukua mieizi 4½ tangu nimeomba kibali mpaka kufungua na duka la dawa miezi 2½...wanakatisha sana tamaa hawa watu.
 
Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu"...

Tunatengeneza bunge la manyani ,hawafanyi kazi zaidi ya kupiga pambio za kumsifia raisi.
 
Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu".

"Nafikiri labda tuongeze kodi labda itapunguza hata sijui, hivi tufanye kitu gani ili tuhakikishe kila mtu anafanya kazi, maafisa maendeleo ya jamii hawafanyi kazi" -Job Ndugai.

Nini maoni yako mdau?
Mwambieni Ndugai kua hua hatuperuzi Bali Tunatandika mikeka ndo ajira zetu zilikobakia huko ambako unakutana na mshahara wako kwa mujibu wa ongezeko la timu tu. Yaani kule tunajipangia wenyewe. Kama wao hawana ajira za kutupa.
 
Back
Top Bottom