Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

ukiwa na kipara unapaswa kuwa makini sana unapozungumza.
 
Kuongea.na kusema vijana wajiajili ni kazi rahisi ila wanaoona rahisi ndio hao wanaokuwa wakali hadi kupiga wenzao na marungu kisa tu kugombea ubunge
 
Natanguliza samahani.ivi spika ndugai amechangia Nini katika taifa tangu awe spika wa bunge la JMT?
 
Sera mbovu za ccm ndo zimezalisha watu hao.Kama wakoloni wao waliweza kwa raslimali hizihizi wao wameshindwa nn Hali mkoloni alirudi kwao na begi tu KILA kitu aliiachia ccm kuanzia viwanda,mito, ardhi,nguvu Kazi, pesa,madini nk
 
Uvivu wetu unasababishwa na mijizi nyie mnajilipa posho lukiki na kubwa hadi kinyaa... sie tukikaa juani tunaungua na kula vumbi... kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa... kauli ya kupuuzi kabisa kuwahi kusikia maishani mwangu kutoka kwa kiongozi wa juu kabisa... Namuomba Ndugai kuthibitisha kauli yake auze kila alichonacho alafu agawe kwa masikini anaowaita wavivu kisha aanze upya maisha yake yenye khofu ya Mungu awaoneshe Watanzania na Dunia na Mungu wake kuwa yeye sio mvivu... la sivyo anyamaze na kuacha kauli mbofu mbofu... kuna watu hawana pa kuanzia wamepambana kila namna hawajafanikiwa wapo pale pale... sera za nchi haziwezi wanyanyua kufika juu afu anasema Wavivu
 
Nimepitia maneno aliyoyazungumza spika Kuna hoja ndani yake ni kweli watanzana wengi hatujitumi au kufanya kazi kwa bidii pale tunapopewa nafasi kufanya kazi katika sekta mbali mbali kwa ajili ya kukuza uchumi wa Taifa letu au hata kwenye kuiwakilisha nchi yetu kwenye mashindano mbali mbali nje ya nchi .ila juhudi zetu tumezielekeza kwenye kuikosoa serikali na kutafuta madhaifu ili lawama zote tuibebeshe serikali.
 
Kuna methari husemaga "Mwenye shibe......??
 
Watu wengi wanaofanikiwa wanatokea kwenye mazingira haya haya miaka nenda rudi wengine wanalalamika maisha magumu Vijana wengi wa kitanzania ni wavivu kuna Makundi mengi ni tegemezi hawataki kujishughulisha mfano hawa vijana wanywaji wa pombe za kienyeji ,watumiaji wa Instagram,vijana wa kubeti nk
itoe betting katika mifano yako
 
Siyo ukomo wa ubunge tu sekita zote ziwe na ukomo Kama ilivyo kwenye uraisi kuanzia ubunge, uwaziri, ukuu wa wilaya, mkoa maana ni sekita za kuleta amsha amsha alafu watoke waingie wengine. Na serikali kuu na taasisi hivyo hivyo zile zinazozidisha miaka sitini ziangaliwe upya Ili vijana wakatumike.
Kote kuwe na ukomo hadi kwenye mikataba ya kazi tu kulingana na maslahi yanayopatikana.

Wenye mishahara inayozidi 6M+ ndani ya miaka 5 wastaafishwe kwa manufaa ya umma wapishe intake nyengine. Wale wenye mishahara ya 2M-4M wapewe miaka 7!

Wenye mishahara chini ya hapo wapewe ukomo wa 10 years.

Hii itasaidia Graduates wakapate uzoefu katika taaluma zao na kujipatia mitaji katika miaka watakayokuwa kazini. Wakitoka ni aidha waunganishe mitaji waanzishe viwanda. Au kila mtu afanye uzalishaji binafsi.

Kwa mawazo yangu ndio naona ni namna pekee ya kufuta umaskini nchini na kuondosha tatizo la ajira.
 
Majibu ya hoja ya ndugai yameenza kutolewa, MB 400 kwa shilingi 1000,lazima vijana wafanye kazi
 
Kazi gani wanataka vijana wafanye wakati wao kama serikali ndio wanaua uchumi na biashara kwa sera mbovu ambazo hazizalishi Ajira kwa vijana?
Wanataka vijana wote mzunguke mitaani mmebeba mizani ya kupimimia uziko?
 
Back
Top Bottom