Spika Ndugai: Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, wakikaa na simu wanaperuzi tu

Sure. Watu kama Kimei, Walitakiwa wawe wametulia sasa lakini sijui wanapambania nini
 
Amekula akashiba ameendelea kula sasa Ndugai kavimbiwa. CCM imeshindwa kutatua tatizo la ajira imebaki kusimanga tu vijana. Upumbavu mtupu wanajadili uko bungeni
Ngoja waandamane..watamkimbiza huyu.
 
Halafu pool haiingizi hela, na kisha biashara ya pool kufungwa.
Na wale vijana watatafuta burudani nyingine ikiwemo madawa ya kulevya, viroba na bangi. (kwani bado mazingira ya kukiajiri yamejaa vurugu).
Baada ya muda tunapata mateja, vibaka , majambazi, maradhi na vifo vinavyotokana na ulevi haramu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wanayasoma haya matatizo kwenye vyombo vya habari lakini hayajawahi kuwapitia angalau karibu.
Nimewai kuhangaika sana na dogo mmoja anauza nguo,, akawa analazimishwa kununua mashine ya efd bila kujali ukubwa wa biashara yake. Mwisho wa siku akafunga biashara. Lakini tukaenda kupambana tena wakamfungulia na kumpa muda.( hili la kumpa muda niloona angalau lilimfanya apumue)

Rekodi zinalazimishwa kwa kuumiza wanannchi,, anayekula mshahara wa baba yake hawezi jua haya.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hivi mucheza poll sio ajira? Kuoeruzi sio ajira?
 
tatizo wamezoea kazi ni mpaka watu wote wakalime kuna kijana tuko nae kitaa ye anashinda saloon kakaa na simu yake lakni ana ml 15 kwenye sportpesa
 
Vijana wanafuatilia jinsi nchi yao inavyoporomokea shimoni kupitia kinachofanyika hapo dodoma, vinginevyo wajitahidi kubadili hali ya mambo muda huu wa majeruhi.
 
Yeye kiongozi mwenyewe anasema hajui cha kufanya.

Kwa nini asiwe sehemu ya tatizo badala ya sehemu ya ufumbuzi wa tatizo?
Mimi nashangaa kwa sasa mjadala mkubwa duniani na kwenye baadhi ya bunge ni issue ya covid hapa kwetu hizo ndiyo akili zilipoishia.

Wanajua wapiga kura wao wanateketea ila wote nahisi wanaogopa.
 
Waongeze kodi!!? Hivi hawa huwa hawasomi historia? Hiyo kauli inatofauti gani na Malkia wa Ufaransa ambaye baada ya watu kulia kuwa hawana mikate akawaambia kama hawana mikate wale keki!!?.

Mtu hana ajira halafu unamuongezea kodi?!
Marry Antoneitte
 
Nakushauri kaombe special seat bungeni
 
Huyu jamaa vipi, yeye bungeni anakaa kufanya nini? kama si kupigwa kiyoyozi cha bure tu huku analipwa mamillion.
 
Taifa halina mpango wowote ule kwa vijana wa rika la 18 - 30 ambao hawana nafasi ya formal education.

Hawa wanatakiwa wawe vyuo vya ufundi...hawa wanatakiwa wawe kwenye mashamba makubwa ya irrigation scheme.

Ndiyo maana mnaagiza Ngano, mafuta ya kupikia, sukari wakati ardhi mnayo...nguvu kazi ndiyo hiyo, maji kibao yanatiririka nchi nzima afu spika na yeye analialia eti hajui cha kufanya.

Bil 500 tu zinaweza kuigeuza Tanzania, yaani ni pesa ya Dreamliner 2 tu.
 
Unadhani wanapenda?Hebu kafanye utafiti vizuri. Hadi watu kufikia hatua ya kunywa urabu wanakuwa wamekata tamaa....
Hii nchi ya hovyo sometime wakati nataka kufungua Maabara ilinichukua mieizi 4½ tangu nimeomba kibali mpaka kufungua na duka la dawa miezi 2½...wanakatisha sana tamaa hawa watu.
 
Kutoka Dodoma.

"Tunatengeneza vijana wa kucheza Pool table, ambao wakikaa na simu wanaperuzi mitandaoni tu"...

Tunatengeneza bunge la manyani ,hawafanyi kazi zaidi ya kupiga pambio za kumsifia raisi.
 
Mwambieni Ndugai kua hua hatuperuzi Bali Tunatandika mikeka ndo ajira zetu zilikobakia huko ambako unakutana na mshahara wako kwa mujibu wa ongezeko la timu tu. Yaani kule tunajipangia wenyewe. Kama wao hawana ajira za kutupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…