Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110

Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110

Kwani wanaenda kikazi au kulala hotelini? Usipoenda kaziini ina maana hauko dodoma kinachojulisha spika kuwa uko dodoma Ni.daftari la mahudhurio kazini bungeni
Per diem ni tofauti na sitting allowance. Per diem unalipwa hata kama uko hospitali. Per diem unalipwa hata siku zisizo za kazi. Daftari la mahudhurio linahusu sitting allowance. Aidha, utawadai vipi malipo ya siku ambazo hazijafika? Je wakija na barua kutoka kwa daktari ikisema kuwa ameamuru wakae karantini kwa kuhofia afya zao itakuwaje. Hili suala ni la kiutendaji na halikuwa na haja ya kulifanya la kisiasa.

Amandla....
 
Anatumia sheria/kanuni gani kukataa kuwapokea iwapo watarudi Bungeni?

Na kwanini wanawalipana in advance?

Je,ni wabunge wangapi watakuwa wamelipwa kwa style hii na baadae kutohudhuria Bungeni kwa siku za nyuma?

All in all,turudishe na yale mamilioni yaliyotumika kwa matibabu huko India.
Mtu haendi kazini unataka alipwe?dogo acha utumwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha,yaani walibugi Sana kutangaza,wangekacha kimya kimya tu,Sasa watawakomalia Hadi Basi na wasipolipa zitakatwa tu kunako pesheni,,ndo maana ilupaswa kufikiri kea mapana Sana kabla ya kuamua kutangaza kuacha kuhudhuria bungeni
 
Anatumia sheria/kanuni gani kukataa kuwapokea iwapo watarudi Bungeni?

Na kwanini wanawalipana in advance?

Je,ni wabunge wangapi watakuwa wamelipwa kwa style hii na baadae kutohudhuria Bungeni kwa siku za nyuma?

All in all,turudishe na yale mamilioni yaliyotumika kwa matibabu huko India.
Wacha wee CHADOMO Work

Mtonyeni bwana Mbowe kwamba kuna Jela na Gesti yeye na wenzie wanapendelea wapi hasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika Job Ndugai amesema wabunge wa CHADEMA ambao hawashiriki vikao vya bunge kwa madai kuwa wapo karantini wanahesabika kama watoro na wanatakiwa kurejesha fedha zote walizolipwa kwa kipindi ambacho hawatakuwepo bungeni.

Pia wamepaswa kufanya kipimo cha Covid19 kabla hawajaingia bungeni
==

TAARIFA ZAIDI
Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Mei 6, 2020 amewataka wabunge wa CHADEMA waliosusia vikao vya bunge kwa kisingizio cha Corona kurudi haraka bungeni

Spika Ndugai amesema endapo watakaidi agizo hilo la kurudi Bungeni basi itawalazimu siku watakayo rudi wawe na cheti kinachoonesha kuwa wamepima ugonjwa wa Corona na majibu yake na kurudisha pesa walizolipwa ambazo ni posho za vikao la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.

"Wabunge hawa ambao ni watoro walipokuwa wanaondoka walilipwa fedha za kuanzia Mei 1-17 Jumla ya zaidi Tsh. Milioni 110, nawaagiza kuanzia Freeman Mbowe kurudisha Tsh. Milioni 2 na elfu 40 na wenzake wote hao, huu ni utoro wa hiari kwa lugha rahisi huu ni wizi na wale wengine wamelipwa Milioni 3 warudishe" amesema Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa; "Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na tangazo hilo kwa sababu Mbowe hana mamlaka ya kuitisha utoro wa wiki mbili kwa Wabunge, anajaribu kuwa kama Prefect wa Shule ya Sekondari, japo wameambiana kubaki Dodoma lakini wanazurura nchi nzima, wabunge hao popote walipo warudi bungeni haraka sana kuendelea na kazi zao".

Inabidi warudishe hela ya bunge. Kumbe wamelipwa in advance halafu dj anawaambia waingie mitini bila kuwajibika. Kama hawarudishi cash lazima hela ya umma wakatwe kwe viinua mgongo. Na ile mijike yao inajidai mikakamavu kupigania hewa kutafuta kick za ubunge i hope hairudi hata mmoja..mungu ibariki tanzania.
 
Wapiga kura tuko njia panda huku tumeambiwa wabunge watoro waliojiweka kwenye karantini ndani ya saa ishirini na nne wawe Dodoma halafu tukaskia tena warudishe fedha na wakapimwe kama hawana virusi vya corona ndio watakanyaga bungeni!! Hatuja kaa sawa mwingine kakamatwa na na bunduki 16 na risasi mia tano !! Naona kama mzee Ndugai sasa anachanganyikiwa ashugulike na jangili au watoro?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ccm ni majangili na majiz

Its not over until its over...[emoji769]
 
Yule mbunge jangili ni kama ana kakikosi ka jeshi kabisa na zile silaha zake!
 
Kuna mtu kwa makusudi kabisa kaamua kutumia shida ya Corona kukimaliza kbs chama kife, sasa huyu ndo wa kushughulika naye...!!!
 
Duuh, Mr Speaker is absolutely under the spell of confusion....!!

Kwa nini Spika awaite wabunge wenzake "wezi" kana kwamba fedha hizo waliomba na kuishia nazo mitini?

Hivi huyu Spika amefikia hatua hii ya kiwango cha ya kukosa uvumilivu na staha kabisa hata kutumia lugha isiyo na staha kuzungumza na watu wazima, wabunge wenzake???

Hivi Spika Ndugai anadhani hao anaowakashfu hivi hawana midomo ya kumjibu kwa kutumia lugha hiyo hiyo aliyotumia yeye? Na ikifanyika hivyo, sisi tutakuwa binadamu wa namna gani eti???

Si zimelipwa kwa utaratibu halali?

Na kwanini kama anataka fedha hizo zirudishwe kwa kuwa zimelipwa kimakosa ama isivyo halali asitumie kauli ya kistaarabu tu na wakati huohuo akifuata utaratibu wa kawaida wa kiutumishi kuwaandikia barua kila mmoja kumtaka arudishe hizo fedha anazodhani si halali yao huku akikwoti na vifungu vya kanuni na sheria inayompa nguvu kuchukua uamuzi wako??

Hizi ni siasa gani za kijinga na kudhalilishana hivi zinaendelea Tanzania kwa sasa??

I really don't get it...!!

Ninavyo fahamu Mimi, mbunge ama wabunge kutoka nje ya kikao kuonesha kutoridhishwa na jambo fulani ni sehemu na haki ya kikatiba na naamini hata kwenye kanuni zao litakuwa lipo. Kwanini jambo hili limekuwa kama nongwa kwa viongozi wa serikali to the extent that wanatumia "fimbo ya fedha" kudhalilishana na kukomoana wao kwa wao??

Hata hivyo yapo maswali mengine hata;

1. Na kwanini Mhasibu wa Bunge alipe posho ya kukaa (sitting allowance) ya wiki mbili mbele kabla mtu hajafanya wala kukaa ama kufanyika kwa kikao husika??

2. Ndiyo utaratibu wa malipo ya fedha za umma unataka hivyo??

3. Mhasibu anapomlipa mtu posho ya kikao ya wiki mbili mbele kabla ya kikao chenyewe anakuwa na uhakika gani kama kikao kitafanyika na kama mtu huyo (aliyelipwa) atakuwepo na hata kuwa hai hadi tarehe 17/05/2020??

4. Kwa hiyo wale wabunge watatu waliokwisha kufa (Rwakatare, Mahiga na Ndassa) wamezikwa na pesa za posho za hadi 17/05?? Watazirudisha toka kaburini, right??

NB;
å Kumbe hawa ndugu zetu CCM wameumia sana kuachwa bungeni peke yao wakiendelea na vikao vyao....

å Nafsi yangu yanishuhudia kuwa hizi ni dalili za tukio kubwa la kihistoria linalokwenda kutokea huko mbele kubadilisha majira na nyakati katika siasa za nchi yetu...!!

å Kwa hakika kabisa pasipo chenga hii "frustration" ya viongozi wa serikali kwa mihimili yote kuanzia MAHAKAMA, EXECUTIVE na PARLIAMENT si ya kawaida hata kidogo....!!
 
Spika Job Ndugai amesema wabunge wa CHADEMA ambao hawashiriki vikao vya bunge kwa madai kuwa wapo karantini wanahesabika kama watoro na wanatakiwa kurejesha fedha zote walizolipwa kwa kipindi ambacho hawatakuwepo bungeni.

Pia wamepaswa kufanya kipimo cha Covid19 kabla hawajaingia bungeni
==

TAARIFA ZAIDI
Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Mei 6, 2020 amewataka wabunge wa CHADEMA waliosusia vikao vya bunge kwa kisingizio cha Corona kurudi haraka bungeni

Spika Ndugai amesema endapo watakaidi agizo hilo la kurudi Bungeni basi itawalazimu siku watakayo rudi wawe na cheti kinachoonesha kuwa wamepima ugonjwa wa Corona na majibu yake na kurudisha pesa walizolipwa ambazo ni posho za vikao la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.

"Wabunge hawa ambao ni watoro walipokuwa wanaondoka walilipwa fedha za kuanzia Mei 1-17 Jumla ya zaidi Tsh. Milioni 110, nawaagiza kuanzia Freeman Mbowe kurudisha Tsh. Milioni 2 na elfu 40 na wenzake wote hao, huu ni utoro wa hiari kwa lugha rahisi huu ni wizi na wale wengine wamelipwa Milioni 3 warudishe" amesema Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa; "Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na tangazo hilo kwa sababu Mbowe hana mamlaka ya kuitisha utoro wa wiki mbili kwa Wabunge, anajaribu kuwa kama Prefect wa Shule ya Sekondari, japo wameambiana kubaki Dodoma lakini wanazurura nchi nzima, wabunge hao popote walipo warudi bungeni haraka sana kuendelea na kazi zao".

Fedha ni za wananch walipa kodi na cc tumeamua wasirudishe kwa hyo

Its not over until its over...[emoji769]
 
Tutamjibu baadae, kumbe umuhimu wetu wanautambua vizuri sana pale bungeni. Haturudi ng’ooo
 
Ndugai akuza deni la matibabu nje ya nchi. Adaiwa kulamba milioni 500 ndani ya miezi mitano
 
Nimesikitika sana tena sana maana miaka yote wamekuwa wakijinasibu kuwa wanapinga ubadhirifu na matumizi mabaya ya pesa za umma.
Hivi kwa nini hawa
kuanza huu mgomo kabla ya kuchukua pesa za wapiga kula wao ambao ni wengi wao ni maskini?
Fikiria mbunge anachukua mil mbili na laki arobaini alafu anasema yupo Dodoma anaenda kujiweka karantini kumbe anaingia mjini Dar es salaam kula bata na familia yake. Huu sio uungwana kabisa.Mbaya zaidi wengine ni wachungaji sasa mchungaji gani unadanganya?
Wabunge wa Chadema na Act wazalendo mmejiabisha maana mmetuibia pesa zetu sisi wanyonge.
Hii inatupa fundisho kuwa October hamtakiwi kurudi tena bungeni.
Natoa wito wote kwa aibu ya kutuibia mjiudhuru. Maana huo ni wizi.
Naona green color mmesimamia kucha hii issue, hoja zenye akili hamuonekani kabisaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom