Spika Tulia Ackson anapaswa awajibike kwa kujiuzulu, kutokana na kutamka kuwa anayemsema vibaya Rais Samia, anapaswa ashughulikiwe!

Kwanza nieleze masikitiko yangu makubwa Sana kwa jinsi nilivyomsikia Spika Tulia Ackson akihamasisha machafuko, wakati akihutubia Umoja wa vijana wa CCM huko jijini Mbeya.

Kwa nchi inayoendeshwa kwa Demokrasia na yenye mfumo wa vyama vingi, ni jambo la kuskitisha Sana kwa matamko aliyoyatoa Spika wa Bunge letu Katika kikao cha UVCCM, kwa kuwataka vijana hao kuwa wasimvumilie mtu yoyote, aidha kutoka CCM au vyama vya upinzani, kuwa washughulike naye, atakayemsema vibaya Rais wetu Samia Suluhu Hassan!

Hayo maneno ni ya hatari Sana Katika nchi inayohubiri kudumisha amani kila siku.

Hivi kutoa "critical criticism" kwa kiongozi wa nchi, au kwa Spika wa Bunge, au hata kwa Mbunge yeyote, lengo likiwa kurekebisha mfumo ambao utauona siyo wa Haki, hivi kuna ubaya gani, Hadi Spika wetu atoe maneno ya vitisho vya kiasi hicho?

Katiba ya nchi yetu, ambayo ni sheria mama, Katika ibara ya 18(1) inatoa uhuru kwa kila mtanzania kutoa maoni yake.

Hivi Spika Tulia Ackson, anajaribu hata kupingana na Katiba ya nchi yetu, iliyotoa uhuru wa wananchi, kutoa maoni yao?

Hivi Spika Tulia Ackson, anajua kuwa kutokana na hayo matamko yake aliyoyatoa kwa huo Umoja wa vijana wa CCM, unaweza kuleta machafuko makubwa ya umwagaji damu nchini?🥺

Kutokana na maelezo hayo ningependa kumwomba Spika Tulia Ackson, ajiuzulu nafasi yake ya u-Spika wa Bunge Ili kuliepusha Taifa hili na machafuko ya umwagikaji damu

Mungu ibariki Tanzania

Mkiambiwa kuwa kuwa na degree au PhD sio kuelimika hamfahamu sasa huo ndio mfano wake. Mtu amefika hadi chuo halafu anatamka utumbo namna hii, hivi kweli utasema huyu mtu ameelimika? Ikiwa mtu anaetuambia kuwa amesomea sheria (sijui kama kuna ushahidi wowote kuthibitisha hayo) anasimama na kuwataka watu kunyonga wenziwao na kutia wasiwasi katika jamii, unadhani huyu mtu ana akili kweli? Hivi alikwenda chuo kusoma au alikwenda kubukua tu?
 
MNAJISUMBUA NA KUJIUMIZA VICHWA TU
MSHAWAHI ONA WAPI TANZANIA
MTU ANAJIUZULU
TANZANIA WATU HAWAJIUZULU AMA KUSTAAFU

ova
 
Ajiuzulu?labda akanyage waya kama yule andunje
Kwanza nieleze masikitiko yangu makubwa Sana kwa jinsi nilivyomsikia Spika Tulia Ackson akihamasisha machafuko, wakati akihutubia Umoja wa vijana wa CCM huko jijini Mbeya.

Kwa nchi inayoendeshwa kwa Demokrasia na yenye mfumo wa vyama vingi, ni jambo la kuskitisha Sana kwa matamko aliyoyatoa Spika wa Bunge letu Katika kikao cha UVCCM, kwa kuwataka vijana hao kuwa wasimvumilie mtu yoyote, aidha kutoka CCM au vyama vya upinzani, kuwa washughulike naye, atakayemsema vibaya Rais wetu Samia Suluhu Hassan!

Hayo maneno ni ya hatari Sana Katika nchi inayohubiri kudumisha amani kila siku.

Hivi kutoa "critical criticism" kwa kiongozi wa nchi, au kwa Spika wa Bunge, au hata kwa Mbunge yeyote, lengo likiwa kurekebisha mfumo ambao utauona siyo wa Haki, hivi kuna ubaya gani, Hadi Spika wetu atoe maneno ya vitisho vya kiasi hicho?

Katiba ya nchi yetu, ambayo ni sheria mama, Katika ibara ya 18(1) inatoa uhuru kwa kila mtanzania kutoa maoni yake.

Hivi Spika Tulia Ackson, anajaribu hata kupingana na Katiba ya nchi yetu, iliyotoa uhuru wa wananchi, kutoa maoni yao?

Hivi Spika Tulia Ackson, anajua kuwa kutokana na hayo matamko yake aliyoyatoa kwa huo Umoja wa vijana wa CCM, unaweza kuleta machafuko makubwa ya umwagaji damu nchini?[emoji3064]

Kutokana na maelezo hayo ningependa kumwomba Spika Tulia Ackson, ajiuzulu nafasi yake ya u-Spika wa Bunge Ili kuliepusha Taifa hili na machafuko ya umwagikaji damu

Mungu ibariki Tanzania
 
Huyo Spika Tulia Ackson, Leo ametoa kauli nyingine mbaya zaidi!

Eti CCM hata kama wananchi wataikataa, katika uchaguzi, watatumia nguvu za Dola kuendelea kubaki madarakani milele!😎
 
Back
Top Bottom