Spika Tulia ameshindwa kujibu maswali badala yake kaongea vitu ambavyo hajaulizwa kwa kupanic na mhemko

Point yako ni ya pili kwa majibu ya swali hilo la mandate, alijibu kwanza vizuri.

Dr Tulia anachukiwa kwa sababu ni spika wa bunge lililojaa CCM, hakuna kitu huu uzi utaipunguza heshima yake kimataifa.
 
Point yako ni ya pili kwa majibu ya swali hilo la mandate, alijibu kwanza vizuri.

Dr Tulia anachukiwa kwa sababu ni spika wa bunge lililojaa CCM, hakuna kitu huu uzi utaipunguza heshima yake kimataifa.
Hiyo ndio shida......kudhani rais Wa IPU ameiwakilisha CCM.
 
Hisia zake zilikuja baadae, kwanza alijibu maswali yao.
Nimeona alijibu maswali kwenye maelezo ya awali akijibu Mjumbe wa Iraq.

Sasa kama unavyojua wabunge wanataka kutest msimamo wako. Mbunge wa Lithuania akamuuliza tena swali linalofanana na la Iraq.

Ili kuonesha msimamo na Ukweli( intergrity) alitakiwa kutoa majibu yale yale na kuendelea na hoja nyingine.
 
Maswali yanaweza kufanana lakini yasihitaji majibu yenye kufanana, mantiki za maswali hutofautiana kati ya muuliza mmoja na mwingine.

Alianza kujibu kwa kuweka msingi wa majibu, kwamba barua za mialiko hutolewa kwanza kabla ya Rais wa IPU kwenda mahali fulani.

Naweza kukubaliana na hoja kwamba waulizaji wa maswali yao walimchukulia poa wakimuona ni mtoto wa kike hivyo wanaweza kumburuza wanavyojisikia, wakakutana na moto mzito.
 
Mkuu kumbe hata wewe umeona? Mtu akikosa majibu sahihi kwa maswali uliyoulizwa lazima ahemke tu ili kuwaogofya wailiza maswali. Hiyo ndiyo defensive mechanism ya madebe tupu.....lazima atike tu!
 
Mkuu kumbe hata wewe umeona? Mtu akikosa majibu sahihi kwa maswali uliyoulizwa lazima ahemke tu ili kuwaogofya wailiza maswali. Hiyo ndiyo defensive mechanism ya madebe tupu.....lazima atike tu!
Angekuwa ni debe tupu asingekuwa Rais wa bunge la CPU, kuonana ana kwa ana na Putin au kiongozi wa ngazi hiyo sio mchezo.

Wabongo katika ubora wetu wa dharau za vijiweni. Kila kitu kukichukulia kwa uzito mwepesi tu. Sio mada za Simba na Yanga kupewa nafasi ya kuongoza bunge la kidunia.
 
Waulizaji au muulizaji??
 
Nimeiona hiyo clip,nadhani kama taifa kuna sehemu moja tunakwama.
Viongozi wetu wamezoezwa kutojibu hoja,badala yake kutumia nguvu kuzima hoja.
Kitu hiki kinatudhalilisha sana,tunapokuwa sehemu ambazo huwezi kuzima hoja kwa kutumia nguvu
bali unatakiwa kuzima hoja kwa kutumia nguvu ya hoja uliyonayo.

Tunahitaji sana kujitafakari,kwa sehemu kubwa niliona alijitahidi kujibu
ila akaharibu alipoaanza kupanic,vinginevyo mimi niliona amejitahidi kujibu.
Hasa alipoulizwa kwanini ulianzia urusi na si ukraine? binafsi yale majibu nilimuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…