Spika Tulia na usomi wake wa kiwango cha PhD anataka bunge libariki kitu kama hiki?

Spika Tulia na usomi wake wa kiwango cha PhD anataka bunge libariki kitu kama hiki?

Bado niko kwenye utafiti! kuna wasomi waliohujumiwa kiakili na kihisia miaka fulani! Nimefuatilia miaka ya tulia UDSM na South Africa. Nimegundua kuna viazi fulani walizalishwa hawana hisia yoyote ya uzalendo au umakini wa kitaaluma. Wamejazwa ubinafsi kupita kiasi PHD ni makaratasi tu.
Hilo lipo wazi, elimu yetu haimwandai mtu kuwa mzalendo au mwenye kutumia taaluma yake.
Elimu yetu inaandaa watu wakufanyishwa kazi na watu wengine (kuajiriwa).
 
Kipengele kimojawapo cha mkataba wa bandari kinasema hivi

View attachment 2649785

yaani maana yake ni kwamba, haturuhusiwi kwa namna yoyote ile KUJITOA katika mkataba huo hata kama tutagundua BAYA la UKUBWA wa kiwango chochote ambao Mwekezaji atakuwa anefanya.

Yaani hata ikitokea Mwekezaji akatumika kumsaidia adui yetu ambaye tuko naye Vitani iwe ni adui wa ndani, au wa nje, tumepigwa pini kuvunja mkataba.

Hata kama tutagundua mwekezaji halipi kodi stahiki kwa makusudi, haturuhusiwi kuvunja mkataba.

Hata kama mwekezaji atahusika kufanya kitu ambacho kiko nje ya mkataba haturuhusiwi kuvunja mkataba.

Yaani TUKISHAINGIA HATUTOKI!

Je, msomi mkubwa, PhD, Dr Tulia Ackson, Mwalimu wa chuo kikuu, anataka bunge lipitishe Uwendawazimu kama huu?

Yaani Kwa Tulia, Uspika kwake una maana kuliko nchi kuuzwa mchana kweupe!

Tunakwenda wapi?
Eti tuangalie dhamira?.
Wajameni naomba ni wapi kinapatikana kipimo cha dhamira ili na sisi tuweze kukitumia!
Screenshot_20220508-210328~2.jpg
 
Tulisha waambia ccm ni janga la taifa na viongozi wake hamuelewi tu,tunatakiwa tuwaondoe kwa namna moja au nyingine,kazi kuangalia tu matumbo yao kwa sasa yaani hawaoni madhara ya baadaye kwa watoto wetu na taifa kwa ujumla
Tunawaondoaje wakati wameshika dola? Balozi tu mtaani lazima awe CCM, mkuu wa wilaya lazima awe CCM, Mkuu wa mkoa Lazima awe CCM. Tutawezaje kuiondoa?
 
Nchi hii itapona siku lile jitu la kuchekachrka likitoweka duniani
Siyo kweli,
Nchi hii itapona siku ile mimi, wewe na yule tukiamka na kuwa serious na mambo yanayohusu taifa letu. Wengi huwa tunahisi mambo ya msingi ya taifa hayatuhusu.
 
Mimi sio mwanasheria, humu wamo wenye taaluma yao.
Siyo lazima kuwa mwanasheria kujua sheria. Elimu ya sheria tujitahidini wote tuijue, itatusaidia sana kwenye kujenga taifa letu. Siyo ngumu. Naombeni mtupe mwongozo tuanze module za sheria hapahapa jamii forum kwanza baada ya hapo tuingie mtaani kutoa elimu. Taratibu tu mwisho tutafika.
 
PhD ya mwafrika isikuchanganye wewe, usomi wa mwafrika upo connected na utumbo wake.

Tulia hana IQ yoyote kwa muonekano tu wa nje.
Tatizo siyo Mwafrika, tatizo ni mfumo wa elimu usioendana na mazingira yetu. Elimu ni kwa ajili ya kutatua matatizo na kurahisisha maisha, si kwa ajili ya kujibia mitihani na kuajiriwa.
Wao wamesoma kujibia mitihani na kuajiriwa
 
Ndani ya CCM mwenye uchungu kabisa kabisa na nchi hii simuoni, labda Mpina peke yake.
 
Leta vipengele vingi ili tuupime kuliko kuchagua kipengele kinachomgombanisha Tulia na wananchi.

Hujausaidia umma kwa kuja na habari robo.
kwani wewe hujaona huo mkataba mbona umewekwa humu ndani.pitia ili uweze kutoa comments zako bila kudandia vya wengine.
 
Ni kama vile nchi nzima hakuna anayejua kusoma na kuandika.
 
Hujui sababu ya bunge kutakiwa kufanya ratification?
Unahisi kwa nini mkataba huu tu ndio umerudi bungeni kwa ajili ya ratification na sio mikataba mingine? Au unahisi Hawa ndio wawekezaji pekee tuliowapata baada ya ile sheria?
Mtu wa TPA kaeleza Hilo vizuri tu asubuhi,tofauti na unachoamini
 
Kwa sababu mmeshindwa kuendesha mambo yenu wenyewe acha tu mpigwe bei
 
Mama yako mzazi ana la ng'ombe!?
Muwe na staha basi. Sasa mama yake mzazi ameingiaje kwenye mapishano yenu. Mtakuja kupata laana msijue zimetoka wapi kwa kuwahusisha hata wasiokuwepo kwenye ugomvi wenu!
 
Shida siyo spika wakuu!

Shida ni lile jitu pale juu!
Aa wapi hicho kidude kidogo kibaya hakiwezi jivua! Tuna uzoefu na Speed and Standard Sita RIP. Huyu aliamua kusimamia alipopataka penye haki. Nakukumbuka kipindi cha richmond walimvaa waccm wenzake akawajibu "niambieni kama sera yetu ni ufisadi" yakanywea na mamvi akasepa!
Huyu mburukenge wa kike ni mwizi asiyejiamini tu!
 
Mimi ningependa kuona kipengele cha kodi,vipi Tax watalipa au ndo free ,pia maslahi ya wafanyakazi. Maana nimesoma mahali UK walipunguza wafanyakazi.
 
Tulia anatuhuma nyingi za ubadhirifu WA Mali za Uma & kutumia kauli zisizo na ethics Kwa wananchi, wadau wasiasa. since before ata hajachukua kiti we knew this, kawaida ufisadi unatabia ya kukua days come" Mwenye kisu ndo anakula nyama.
 
Hivi tukikabidhi bandari, ikatokea jeshi letu likaagiza siraha nzito je zitaingilia wapi na hawa wazandiki waarabu wasijue ?
 
Back
Top Bottom