Spika Tulia: Wanaopinga mkataba wa bandari wana mdomo. Msiwasikilize wanaohubiri ubaguzi

Lipo andiko Hilo, sijatoa kichwani,

Linaendelea kusema,

Mungu akiruhusu mtoto,au mwanamke awe kiongozi wataifa Hilo,

Huwa dhamira, ni kuliadhibu Taifa Hilo.
Aisee nisaidie hilo andiko
 
Aha,kumbe ukitaka kupinga ushoga lazima uwe uliwahi kuwa shoga!?
 
Alafu kuna watu bado wanamtetea marehemu kwa kuwaleta hawa wapumbavu, inamaana hakunaga vetting kwenye uongozi.
Poleni waTanzania kwa kupata hasara ya viongozi kila mwaka.
 
Huyu naye amelewa madaraka. Mikono yake imejaa damu za maskini. Moyo wake umejaa tamaa ya fedha na madaraka haramu kama malkia Yezebeli. Amepandishwa kilima cha madaraka asijue kuwa kesho yake ni ya majuto na hatima yake ni anguko kuu.
 
To be frank huyu mtu ameni disappoint sana...Sikutegemea kabisa kabisa...Labda I had too high expectations over her...Mungu amkumbushe kuwa kuna kesho
 
Watanganyika wakisema kuhusu utanganyika wao, na Tanganyika yao Kwa ccm wengi ni ubaguzi lakini wazanzbari wakisema juu ya uzanzbari wao siyo ubaguzi ni haki yao. Leo umekuwa ubaguzi watu kusema Ras ni mzanzbari,waziri ni mzanzbari, wakati wao wenyewe wanakiri ni wazanzbari na vitambulisho vya ukaazi wanavyo. Swala la kuligawa Taifa , tulia ujue maamuzi yeyote mabaya huligawa Taifa au jamii. Tulia usiwaone hawana akili watanzania Kwa vile wanaopinga yasiyo sawa.
 
Hajajibu hata hoja moja au kutolea ufafanuzi wa vifungu vinavyolalamikiwa zaid ya kuleta ngonjela kama kawa
 
Aliye sain mkataba Mwenyewe kastuka alicho kisaini
Ameagiza Mkataba upitiwe Tena

Sasa huyu mama PhD holder ana Bwabwaja nini
 
Hakuna mtu yeyote anayepinga huu mkataba kinachopingwa ni vile vipengere vilivyomo kwenye huo mkataba.
 
Ningekua Tulia, leo ningepanga siku 3,za kuchambua Ile document ya Dp world kifungu kwa kifungu jijini Mbeya, tena ningeruhusu maswali siku nzima nikiuchambua ule mkataba kisheria mpaka wanambeya na Nchi yangu waelemike, leo ningedifend nchi na serikali yangu, ningejibu sintofahamu zote japo by 90%. Lakini maajabu yake amenda kulopoka lopoka kama wafanyavyo wenzake. Usomi Africa mashaka mashaka, tumbo tumbo shiba lalalalaaa. Maweee!!
 
Hio phd imemfanya awe mjinga bora Hata asingekua nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…