Spika Tulia: Wanaopinga mkataba wa bandari wana mdomo. Msiwasikilize wanaohubiri ubaguzi

Spika wa Bunge Dkt.Tulia awashukia vikali kama mwewe wanaopinga Mkataba wa Uwekezaji Bandarini. Hayo yamejili wakati wa ziara yake jimboni Mbeya kuelezea faida za uwekezaji wa DP world katika bandari nchini

Watu wamesema sana na mimi huwa nakaa kimya nawasikiliza tu, Huwezi kuwa unabisha kila kitu, wewe kila kitu hutaki, unataka nini?

Kuna mtu aliwahi kusema, huyo anafikiri tutamchagua kwa bodaboda, bajaj anazowapa watu, mimi nikauliza wewe umewahi kutoa hata sindano ya kushona nguo ikichanika?

Sasa huku mtaani kuna watu wana mdomo sana wakati hawajawahi kuagiza hata Tshirt moja ikapita bandarini. Halafu yeye ana maneno utadhani hata pale bandarini amewahi kufika hata akajua huo mzigo unachukua muda gani, huo wizi unatokea muda gani.

Sasa kuna watu wanasema kuwa hao wezi wamewekwa na nani? Hao wezi ni kama wewe tu, ukiwekwa pale ungekuwa hivyo hivyo. Kwa hiyo lazima tutafute namna ya kupata pesa zaidi ya kujenga na kurekebisha madarasa.

Wanambeya msidanganyike, Mheshimiwa Rais ana nia njema nasi.

Wapo watu ambao ni wataalam wa kuvuta mashati nyuma wenzao, na mimi niliahidi na nirudie... Mimi siyo mtu unayeweza kushika shati nyuma halafu ukafikiri utanirudisha hatua nyuma, navua shati utabaki na shati utanikuta mbele kule.

Nchi ya Tanzania iko salama na haitagawanyika eti kwasababu eti kuna mtu kajikalisha mahali anataka kutuweka vipande, hatutagawanyia muungano huu ni wa kudumu

Na usimsikilize mtu ambaye anakuhubiria ubaguzi ukafikiri unamwelewa vizuri, leo anabagua yule, kesho atakuja kwako akakuambia wewe siyo kabila langu.
Hiki kimama nilifikiri kina uzalendo na fikra za kimapinduzi za asili kwenye chama cha mapinduzi kumbe ni kimamluki tu. Kama speaker amefeli kuliongoza bunge kama taasisi huru na mhimili huru wa dola. Badala yake amekua muoga baada ya kuona dikteta wa kike samia akimfungisha virago mtangulizi wake kimabavu huku akionyesha amehamaki kwa speaker kutofautiana naye. Tulia ameonyesha usomi wake hauna maana kwa kuunga mkono na kutetea mkataba wenye vifungu kinyume na katiba ya nchi na kwenda iweka nchi chini ya mamlaka ya kigeni.
 
Huyo kasoma sheria anaijua vizuri kuliko nyie makanjanja
Pamoja na kusoma ila elimu yake ni ya bure maana mambo madogo madogo kama kujua kuwa Dubai sio nchi yanamshinda.

Angekua nguli kweli asingekubali kuiaibisha taaluma yake kwa kupitisha mkataba wa hovyo namna ile.
 
Spika wa Bunge Dkt.Tulia awashukia vikali kama mwewe wanaopinga Mkataba wa Uwekezaji Bandarini. Hayo yamejili wakati wa ziara yake jimboni Mbeya kuelezea faida za uwekezaji wa DP world katika bandari nchini

Watu wamesema sana na mimi huwa nakaa kimya nawasikiliza tu, Huwezi kuwa unabisha kila kitu, wewe kila kitu hutaki, unataka nini?

Kuna mtu aliwahi kusema, huyo anafikiri tutamchagua kwa bodaboda, bajaj anazowapa watu, mimi nikauliza wewe umewahi kutoa hata sindano ya kushona nguo ikichanika?

Sasa huku mtaani kuna watu wana mdomo sana wakati hawajawahi kuagiza hata Tshirt moja ikapita bandarini. Halafu yeye ana maneno utadhani hata pale bandarini amewahi kufika hata akajua huo mzigo unachukua muda gani, huo wizi unatokea muda gani.

Sasa kuna watu wanasema kuwa hao wezi wamewekwa na nani? Hao wezi ni kama wewe tu, ukiwekwa pale ungekuwa hivyo hivyo. Kwa hiyo lazima tutafute namna ya kupata pesa zaidi ya kujenga na kurekebisha madarasa.

Wanambeya msidanganyike, Mheshimiwa Rais ana nia njema nasi.

Wapo watu ambao ni wataalam wa kuvuta mashati nyuma wenzao, na mimi niliahidi na nirudie... Mimi siyo mtu unayeweza kushika shati nyuma halafu ukafikiri utanirudisha hatua nyuma, navua shati utabaki na shati utanikuta mbele kule.

Nchi ya Tanzania iko salama na haitagawanyika eti kwasababu eti kuna mtu kajikalisha mahali anataka kutuweka vipande, hatutagawanyia muungano huu ni wa kudumu

Na usimsikilize mtu ambaye anakuhubiria ubaguzi ukafikiri unamwelewa vizuri, leo anabagua yule, kesho atakuja kwako akakuambia wewe siyo kabila langu.
Jinga sana huyu. Mbeya uchaguzi mwingine piga chini hii kitu.
 
Huyo kasoma sheria anaijua vizuri kuliko nyie makanjanja
sasa pale ni alitakiwa ajibu hoja kwa kuchambua vifungu walivyoelezea wanasheria wenzake ambavyo ndio utata ulipo; yeye anapiga ovyo mstuni bila shabaha. Sio kuleta siasa kwenye sheria; ni kifungu flan hakipo itakuwa hiv na hiv mwenye swali..... hivyo
 
Wale wa ''ccm mbele kwa mbele'' siwaoni; tupo pamoja
-- 'mama kanyaga twende'
-- 'kanyagia hapo hapo'
 
Nina wasiwasi kama ile kaulimbiu ya "Wanawake wakiwezeshwa wanaweza" itaweza kuwa na mashiko tena kiasi cha kuiamini tutakapo isikia tena.

Mkuu wa mhimili baada ya kuvulunda Bungeni badala ya kujikalia kimya na kungoja kunyoosha mambo kwenye kikao kijacho ameamua kukebehi watu na kujiona yeye ndie msomi wa sheria mbobezi kuliko wale anaowaongoza......

Ama kweli ""Shibe ni mwana malevya""😳
 
Eti bandarini kwenyewe hatujawahi kufika...

Spika mzima anachukua talking points kutoka kwa Maulidi Kitenge, a radio DJ
 
Spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa mbeya dk tulia akson ,amewaonya watu wanaoendeleza mjadala wa bandari na huku wakiwa hawaijui hata bandari yenyewe ! Dk tulia amesema hayo akiwa katika ziara ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake na kusisitiza kwamba Kuna watu Wana mdomo sana lakini hata kuagiza tshrt Moja ikapita bandarini hawajawahi ,dk tulia amesema Kuna wengine hata hawajui mzigo ukifika bandarini unachukua siku ngapi kutoka hivyo kuwataka watu wajikite kujadili vitu kwa kuvielewa sio kufuata Kila kinasemwa mitandaoni ,nb hayo ni maoni yake
 
Hizo dharau kwa wananchi, wao wakijibiwa wanasema wametukanwa na wanakutaka uripoti central.
 
Spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa mbeya dk tulia akson ,amewaonya watu wanaoendeleza mjadala wa bandari na huku wakiwa hawaijui hata bandari yenyewe ! Dk tulia amesema hayo akiwa katika ziara ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake na kusisitiza kwamba Kuna watu Wana mdomo sana lakini hata kuagiza tshrt Moja ikapita bandarini hawajawahi ,dk tulia amesema Kuna wengine hata hawajui mzigo ukifika bandarini unachukua siku ngapi kutoka hivyo kuwataka watu wajikite kujadili vitu kwa kuvielewa sio kufuata Kila kinasemwa mitandaoni ,nb hayo ni maoni yake
Eti ndie anaeongoza kuisimamia serikali 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom