Spika wa Bunge Tulia Ackson ashitakiwa Kwa Wananchi , namba yake ya simu yawekwa hadharani

Spika wa Bunge Tulia Ackson ashitakiwa Kwa Wananchi , namba yake ya simu yawekwa hadharani

Mnyika anajua Sheria vizuri, kutoa namba ya mtu tena kwenye Public bila ridhaa yake ni kosa kisheria. Mtu anaweza kwenda lodge au gesti akafanya uhalifu kwenye kitabu Cha wageni akajaza namba ya spika. Sio Kila mnayemuona hapo ni mtu mwema.
NB: Sipo upande wa Dr. Tulia.
Akili yako iko kwenye Lodge na hujitambui.
 
Mambo ya hovyo tu, mmeshindwa kuwaondoa kisheria hizosimu ndio zitawaondoa?.

You guys are not serious at all, mnaendekeza mambo ya kipuuzi sana.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na mambo Mengine kwenye viwanja vya furahisha Mwanza Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika amewaagiza wananchi kumpigia simu Spika huyo ili kumlazimisha awaondoe Bungeni wabunge 19 maarufu kama COVID 19 , ambao amedai wamewekwa bungeni humo kinyume cha sheria

Mnyika amedai kwamba ni vema kila mwananchi akampigia simu au akamuandikia SMS Spika ili kumtaka haraka aondoe Wabunge wasio na Chama Bungeni humo , amedai kesi iliyo mahakamani haina uhusiano wowote na wao kuondolewa bungeni .

Namba ya Spika imetajwa kuwa ni 0784 763 *** ambayo baada ya kuifuatilia tumejiridhisha kwamba , imesajiliwa TCRA kwa jina la Tulia Ackson Mwansasu

Kazi kwenu wananchi , namba za simu za viongozi siyo siri , ndio maana za Ma RPC na IGP zote ziko hadharani , hawakuzitoa kama mapambo , wametupa ili tukiwa na lolote tuwapigie
Tulia ni mwanasheria.
Sidhani kama hiyo namba imesajiliwa kwa jina la Spika wa Bunge la JMT yaani simu ya ofisi.
Nina hakika imesajiliwa kwa jina la Tulia Ackson Mwansasu. Jina binafsi. Jina ambalo ni mali yake.

Mnyika ana kesi ya kujibu kwa kutoa namba ya Tulia kwa watu asio wajua ( siyo Spika) bila idhini yake.

Siungi mkono. Alotoa hiyo namba hajui kanuni
 
..Mnyika ameweka namba ya simu ya Spika wa Bunge.

..hajaweka namba simu ya Dr.Tulia Ackson.

..mawasiliano ya watumishi wa umma yanatakiwa yajulikane kwa wananchi ili waweze kuwafikia na kueleza shida zao.
Imesajiliwa kwa jina gani?
Kenge wewe
 
Duh
Yaani kama chama ndo kimeshashindwa kuwatoa
ENYI MLIOAMINI! KUWENI WASIMAMIZI (Wa kupitisha haki) KWA AJILI YA ALLAH, MUWE MKITOA SHAHADA (ushahidi) KWA UADILIFU. WALA KUCHUKIANA NA WATU KUSIKUPELEKEENI KUTOWAFANYIA UADILIFU (insafu). FANYENI UADILIFU, HUKO NDIKO KUNAKOMKURUBISHA MTU NA UCHA MUNGU NA MCHENI ALLAH, HAKIKA ALLAH ANAZO HABARI ZA (yote) MNAYOYATENDA.”[5:8]
 
Tulia ni mwanasheria.
Sidhani kama hiyo namba imesajiliwa kwa jina la Spika wa Bunge la JMT yaani simu ya ofisi.
Nina hakika imesajiliwa kwa jina la Tulia Ackson Mwansasu. Jina binafsi. Jina ambalo ni mali yake.

Mnyika ana kesi ya kujibu kwa kutoa namba ya Tulia kwa watu asio wajua ( siyo Spika) bila idhini yake.

Siungi mkono. Alotoa hiyo namba hajui kanuni
Uadilifu kwa wanadamu:

Huu unamtaka mwanadamu awe muadilifu kwa wanadamu wenziwe kwa kumpa haki kila anayeistahiki kwa mujibu wa sheria.

Katika kulitekeleza hili asiuweke mbele ya macho yake ujamaa, urafiki, rushwa, uadui na kadhalika.

Huu unahusisha pia kuwafanyia uadilifu na kuwapa haki wanazozistahiki wake kwa kila aliye na zaidi ya mke mmoja. Katika hili watoto pia hawaachwi nyuma, asiwapendelee hawa zaidi kuliko wale.
 
Hapa chadema ndio maana mnaitwa chama cha wauni…..hivi unawekaje namba ya mtu hadharani! Huu ni ushamba wa hali ya juu! Hiki ndio chama kinataka kipewe nchi kinatenda ujinga huu na wakijua ni kosa!

Hivi mnawapa namba wananchi ili wamtukane tuu halafu mpate nini?
Mnyika yuko sahihi. Tulia na namba yake ni halali ya wananchi. Sitarajii wamtukane sababu hayo si maelekezo ya Mnyika.
Wakati wa kuwajibika kwa umma umefika. Baada ya Tulia .......... na .............!
 
Mnyika anajua Sheria vizuri, kutoa namba ya mtu tena kwenye Public bila ridhaa yake ni kosa kisheria. Mtu anaweza kwenda lodge au gesti akafanya uhalifu kwenye kitabu Cha wageni akajaza namba ya spika. Sio Kila mnayemuona hapo ni mtu mwema.
NB: Sipo upande wa Dr. Tulia.
Yaani anuani ziwekwe kwenye tovuti ni sawa kisheria lakini Mnyika akizisema hadharani ni kosa kisheria?
Mbona nyie mnakuwa najuha kiadi hiki?
Screenshot_20240215-205902_Adobe%20Acrobat.jpg

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hapa chadema ndio maana mnaitwa chama cha wauni…..hivi unawekaje namba ya mtu hadharani! Huu ni ushamba wa hali ya juu! Hiki ndio chama kinataka kipewe nchi kinatenda ujinga huu na wakijua ni kosa!

Hivi mnawapa namba wananchi ili wamtukane tuu halafu mpate nini?
Spika sio "mtu tu" kama wewe uliye mtu tu..

Huyo ni mtu lakini tofauti na wewe, yeye ni "kiongozi wa umma" na ni reachable na kila mtu.

Ajabu iko wapi hapo?

Tatizo lako kubwa ni kuwa, unasumbuliwa na ushamba na ujinga tu wa kukosa ufahamu..
 
Ila nyie Chadema bhana 😂 mna vituko sana, unasema namba za simu za viongozi sio siri wakati hujaandika hiyo namba ya huyo kiongozi, sasa kama sio siri si uiandike yote
 
..Mnyika ameweka namba ya simu ya Spika wa Bunge.

..hajaweka namba simu ya Dr.Tulia Ackson.

..mawasiliano ya watumishi wa umma yanatakiwa yajulikane kwa wananchi ili waweze kuwafikia na kueleza shida zao.
Kwahy namba ya simu ya spika wa bunge ndio linasajiliwa kwa kitambulisho cha spika aliyepo.?
 
Back
Top Bottom