Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimekuelewa mkuu...Sina hoja nyingine zaidi ya kukubaliana na wewe.Tupo tofauti ninaweza kuona wazo la kwako ni baya ila wewe binafsi unaliona zuri
Japo na upendo upo ila mi nadhani ni tofauti....ni ile hali ya kupata treatment Kama mtoto, upikiwe, ufuliwe yani upo kama mtoto kuna mtu anakua anakutimizia mahitaji yako (mke) akiondoka sasa unabaki kama yatima...Ndio ujue jins gan wanaume tulivyo na upendo
Kumbe nimeangalia vibaya upo ukurasa mwingine wanaodai sasa na wewe unadaiwa kila kona nikiuonyesha tu watakusumbua[emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji2815][emoji2][emoji2]hebu onesha
KWANINI iwe hivyo mkuu?Haya yatakuwa makafara
Msono wa mawazo, haya mambo acheni kabisa, acheni nasea acheni, sikia kifo tu kw mme au mke wa mwenzio, kisikukute:Kwa ambaye anamfahamu SSGT Ruta alikuwa Msata amejiua kwenye kaburi la mke wake ambaye alifariki siku ya Jumamosi huko kilakala kaacha ujumbe kuwa alikuwa anampenda mke wake.
========
Dar es Salaam. Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Reginald Ruta amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa juu ya kaburi la mkewe, Godebertha aliyezikwa katika makaburi ya Mekyuri Kipawa jeshini mkoani Dar es Salaam.
Juni 7, mwaka huu mwili wa askari huyo aliyezikwa katika makaburi hayo jana, ulikutwa katika kaburi la mkewe aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla.
Kifo cha askari huyo wa kambi ya Msata mkoani Pwani kimeacha simanzi kwa ndugu, jamaa na marafiki, kwa kuwa kilitokea siku tatu tangu mkewe afariki.
Akisoma risala kwenye ibada ya kuaga mwili wa askari huyo, iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Karakata Kipawa, diwani wa Karakata, Idary Karugendo alisema marehemu ameacha watoto wanne na wajukuu watano waliokuwa wanamtegemea.
“Mzee Ruta alikuwa tegemeo kwenye familia yake kama baba, hasa baada ya kifo cha mke wake kutokea siku chache zilizopita,” alisema Karugendo.
Akizungumza katika ibada hiyo, Katekista wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Kipawa, Silivester Sadick alisema kifo hicho ni funzo kubwa kwa watu wote na kinaonyesha wazi hakuna binadamu mkubwa mbele ya Mungu.
“Juzi tulikuwa hapa hapa, tena nawaongoza kwenye ibada ya kumuaga mke wake, hakuna aliyekuwa anajua nani anafuata lakini leo mzee Ruta anafuata, ni funzo kubwa ndio maana nawakumbusha kuzidi kumuomba Mungu wakati wote,” alisema.
Alisema kifo kinaharibu mipango yote ambayo binadamu anakuwa amejipangia kuitekeleza na ndiyo maana watu husema kifo hakina huruma, lakini ukishakufa unakwenda kwa Mwenyezi Mungu.
“Maisha ya hapa duniani yanapita, juzi tulizungumza hatujui nani anafuata, lakini mume ameenda, kama maisha yetu yako namna hii binadamu ni nani mbele ya Mungu.
Familia ipo kwenye wakati mgumu, kama ingekuwa ni mimi leo ingekuwaje, kikubwa tujitengenezee njia ya kufika mbinguni mapema na naiomba familia kuzidi kufanya maombi na kusimama katika imani kwa Mungu kwani hawezi kuwaacha,” alisema.
Kifo kilivyotokea
Kwa mujibu wa jirani mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, alidai kuwa walikuwa wote na Ruta siku ya Jumamosi ambayo yalifanyika mazishi ya mkewe aliyefariki ghafla wakati akijiandaa kwenda kazini.
Alisema baada ya mazishi Jumatatu iliyopita, vijana waliokuwa wanachunga mbuzi waliukuta mwili wake juu ya kaburi hilo.
Chanzo hicho kilieleza kwamba watoto hao baada ya kuona mwili huo wakaenda kutoa taarifa jeshini kwa sababu eneo hilo linamilikiwa na Jeshi na walipofika pale wakampekua hawakuona chochote zaidi ya kitambulisho chake.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya mazishi ya mkewe, Jumapili iliyopita Ruta alifanya vikao vya mara kwa mara na watoto wake wanne na kuwaeleza mali alizonazo na sehemu zilipo.
“Baada ya kufanya vikao virefu na watoto wake huku akiwachekesha muda wote, aliwaambia kuwa atakwenda kununua marumaru kwa ajili ya kujengea kaburi la mkewe na aliwaeleza kuwa akishafanya manunuzi atawaeleza,” zinaeleza taarifa hizo.
Habari zaidi zinaeleza kuwa alimuomba mwanaye mmoja ampe Sh50,000 kwa ajili ya kununua marumaru hizo na alipopewa fedha hizo aliondoka nyumbani hakurejea tena.
Polisi wanena
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Janeth Magomi alikiri kupokea taarifa ya kifo na kudai ililetwa na wanajeshi wenzake kutoka kituo cha Polisi Stakishari.
“Kwamba kuna mwenzao wamemkuta amefariki juu ya kaburi la mkewe, wakati wanatoa taarifa hiyo tayari mwili ulishachukuliwa na kupelekwa hospitali ya Lugalo,” alisema Janeth.
View attachment 1815077
View attachment 1815080
Amekosea tu kuzaaa watoto wengiKama ni kweli, huyo ni mjinga hasa. Not fair kabisa kwa watoto wake hasa wadogo.
Hiyo ya latekosta sio misa ni ibada fupi..kwa kifupi huyo halufanyiwa misa yoyote na kama mke nae ibada ya mzishi yake iliongozwa na katekista bas familia walikiwa hawashiriki ibada za kanisa....mawazo yanguHuwa mtu akijiua baadhi ya dini ikiwemo RC wanatoa hukumu kabisa, kwamba yeye ni wa motoni, hivyo hawamfanyii ibada/misa
Lakini hapa nimeona tofauti maana unasema katikista aliongea kwenye ibada. nimenukuu hapa chini
'Akizungumza katika ibada hiyo, Katekista wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Kipawa, Silivester Sadick alisema kifo hicho ni funzo kubwa kwa watu wote na kinaonyesha wazi hakuna binadamu mkubwa mbele ya Mungu.'
Mafunzo sahihi kuhusu nini??Hivi mna uhakika jeshi ketu kinatoa mafunzo sahihi?
Ni mwanadamu pia ana moyo anaweza kustahimili kuwa mateka lakini sio kuwa na sononaFucking coward, hivi mwanajeshi unajiuaje wakati upo uraiani? Sio kama umetekwa vitani?! How can you justfy taking ur own life?
Fucking coward, jitu lina miaka 50, linajiua! Bora ujiue kama unaumwa unahofia utawapa hasara wakikuuguza kwa muda mrefu,
This is totally shit
Poleno majiran..kuna mdai hapo juu amesema kitu hiki kuwa yawezekana huyu jamaa wakat wa uhao hakuwah muonyesha mkewe ishara yoyote kuwa anampenda....lakn kafa inataka ionekane kuwa alikuwa anampenda sana mke ...nafsi yake imelia had ikakoma..akajimaliza..huyu ni kichwa maji..Sababu ya huyu Mgambo kujiua ni Majuto. Namuita mgambo sababu mwanajeshi kamili hawezi kujiua kizembe namna hii. Kiufupi jamaa alikuwa mbali na mke wake kimahusiano. Kifo cha mke wake asilimia kubwa kimesababishwa na tabia na matendo yake yasiyokuwa mazuri. So alijiona kakosea na hakuna tena nafasi ya kumuomba msamaha mkewe. To me haya ni maamuzi yenye ubinafsi. Nafikiri kifo cha mkewe kingekuwa turning point ya yeye kuwa mtu bora zaidi kwa familia na jamii kwa ujumla kuliko kujiua. Hili tukio limetokea mtaani kwangu so hiki nilichoandika siyo story ya kutunga.
Ndiyo hivyo mamlaka husika zipo mzigonikuna shida mahala, wachunguzi wetu waliobobea waingie kazini hapa...kuanzia kifo cha mke then warudi kwenye kifo cha Mzee. Vifo hivi vinaonekana vina kisa kimoja kinachofanana....