TANZIA SSGT Reginald Ruta wa JWTZ amejiua kwenye Kaburi la marehemu Mkewe

TANZIA SSGT Reginald Ruta wa JWTZ amejiua kwenye Kaburi la marehemu Mkewe

Watani zangu ' Wahaya ' mmeniaibisha.
Ni huyo tu mahaba yalimzidia. Kuna watu wapo hai kwa sababu pembeni yao kuna mtu anaefanya waone thamani ya maisha duniani inapotokea yule mtu akatoweka nao wanapoteza matumaini na hawaioni tena thamani ya uhai wala ya watu wanao wazunguka.
 
Nakumbuka tukiwa chuo tulikuwa tunabishana sana kati ya mtoto,mke/mume na mama yupi akifa unapata maumivu sana,,kuna lecturer ni mtu mzima sana alisema mke akifa anauma mno tena haswa mkipendana, akajitolea yeye mfano tangu mke wake afariki ni miaka 10 sasa nyumba aliiona kubwa sana ikabidi auze nyumba,akaenda kujenga sehemu nyingine anasema alipitia kipindi kigumu mno maishani mwake.
Kwa yaliyomtokea huyo askari nimemkumbuka lecturer
Pamoja na yote niseme wazi tu kuwa mlikuwa mnabishana au mnajadili kitu cha kijinga sana tena sana...samahani kama nimekuvunjia heshima.
 
Hebu nieleweshe hapa.. Maana naona ndio kilichotokea kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa mtu akijiua baadhi ya dini ikiwemo RC wanatoa hukumu kabisa, kwamba yeye ni wa motoni, hivyo hawamfanyii ibada/misa
Lakini hapa nimeona tofauti maana unasema katikista aliongea kwenye ibada. nimenukuu hapa chini

'Akizungumza katika ibada hiyo, Katekista wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Kipawa, Silivester Sadick alisema kifo hicho ni funzo kubwa kwa watu wote na kinaonyesha wazi hakuna binadamu mkubwa mbele ya Mungu.'
 
Naanza kuamin ule usemi ukiona ndoa yako imetulia na Haina migogoro ujue umeanza kuwaelewa wanawake tabia zao na hapo kifo chako hakipo mbali sana

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hahahaa hii kali jamani...ila kwann wajane wengi wakifiwa wananawiri balaa wachache sana wanapauka ...! Inatoa picha gani
 
Nakubaliana na wewe hasa kama hajajiua (i.e.ameuwawa). Kama amejiua kwa ridhaa yake na kwa sababu iliyotajwa, bila ya shaka ni mjinga.

Huwezi kuacha watoto wako yatima kwa sababu nyepesi za hivyo.
Lilo jepesi kwako, kwa wengine ni zito na huenda kuna mazito kwa wengine na kwako yakawa mepesi.
 
Back
Top Bottom