Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Hakika.
 
Faraji katalambula,hammie rajab,na Eddie ganzer.umenikumbusha mbali sana,miaka ya 1980 ndio namalizia shule ya msingi.
 
Kumbe huu mfumo upo enzi na enzi wa kuwashughulikia wale wote wenye mawazo kinzani na maslahi yao binafsi.

Ashukriwe Mungu mkuu ambaye anatuvuna wote huku tukielekea kujibu mashitaka ya maovu yetu sote.

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema, "ukiona kiongozi wa ngazi za juu anamtaja taja sana Mungu basi tambua huyo matendo yake ndo Shetani nyuma ya pazia".
 
Huu ndiyo ulikuwa muda sahihi wa Pascal Mayalla kujitwalia tuzo ya Nobel endapo ungejikita kwenye uandishi wa habari za uchunguzi. Najua hii kazi umesomea, una weledi nayo na iko ndani ya uwezo wako. Sijui unakwama wapi Pascal Mayalla ??

Labda nikusaidie mambo ya kuyachungiuza na kuja na stori kamili.
1. Akina nani walimuua Chacha Wangwe?
2. Akina nani walimuua Alphonce Mawazo.
3. Kwann serikali ya ccm haitaki kuchunguza tukio la Lisu kupigwa risasi?
4. Kwann Makonda anazidi kupewa vyeo na serikali ya ccm ili hali watanzania wote na dunia kwa ujumla tunajua kuwa ni mtoa roho za watu? USA waliosema anadhulumu watu haki ya kuishi.
5. Nani wamiliki wa DP World?
6. Uko wapi ukoo wa babake rais Samia? Baba wadogo, mashangazi, n.k. Au tuamini tunayoyasikia?
 
Shujaa Stan Katabaro ..........Mungu aiweke roho yako patakatifu Amina!

Naikumbuka sana Kashfa ya Loliondo..................iko siku wahusika watajibu kama si mbele ya umma wa Watanzania basi mbele ya Mungu!
Ashafikishwa kwa mnyezi Mungu.

Kwa sasa anapunguziwa makali ya kaburi kisiwani.
 
Inasadikika ilikuwa ni maagizo kutoka CHADEMA
2. Akina nani walimuua Alphonce Mawazo.
Katafute taarifa polisi Geita na Mahakamani kule
3. Kwann serikali ya ccm haitaki kuchunguza tukio la Lisu kupigwa risasi?
Mazingira yale ya uhasama yaliletwa na Vyama vya Siasa. Walifikiri wakimtoa kafara mwenzao machafuko yatatokea na Serikali itaanguka.
4. Kwann Makonda anazidi kupewa vyeo na serikali ya ccm ili hali watanzania wote na dunia kwa ujumla tunajua kuwa ni mtoa roho za watu?
Wacheni wivu mtaona .
USA waliosema anadhulumu watu haki ya kuishi.
U.S.A ndio nchi peke yake Duniani inayodhulumu watu haki zao
5. Nani wamiliki wa DP World?
Waarabu na Wazungu
6. Uko wapi ukoo wa babake rais Samia? Baba wadogo, mashangazi, n.k. Au tuamini tunayoyasikia?
Nenda ikulu ukaulize. Acha Uzushi
 
Huu ndiyo ulikuwa muda sahihi wa Pascal Mayalla kujitwalia tuzo ya Nobel endapo ungejikita kwenye uandishi wa habari za uchunguzi. Najua hii kazi umesomea, una weledi nayo na iko ndani ya uwezo wako. Sijui unakwama wapi Pascal Mayalla ??
Mkuu Sexless , kwanza nikushukuru kwa imani yako kwangu, ni kweli hayo yote yako ndani ya uwezo wangu, na kiukweli sijakwama popote bali ni mipangilio tuu!.
Labda nikusaidie mambo ya kuyachungiuza na kuja na stori kamili.
1. Akina nani walimuua Chacha Wangwe?
Hili halihitaji uchunguzi, ile ilikuwa ni ajali tuu, ila eneo la Pandambili ni very notorious kwa ajali za ajabu ajabu, sio ajali ya Wangwe tuu , hata Salome Mbatia alipatia ajali eneo hilo hilo na kupoteza maisha!. Mimi mwenyewe nilipatia ajali eneo hilo hilo, nikaponea tundu la sindano!
2. Akina nani walimuua Alphonce Mawazo.
this is valid
3. Kwann serikali ya ccm haitaki kuchunguza tukio la Lisu kupigwa risasi?
this is valid but very dangerous undertaking
4. Kwann Makonda anazidi kupewa vyeo na serikali ya ccm ili hali watanzania wote na dunia kwa ujumla tunajua kuwa ni mtoa roho za watu? USA waliosema anadhulumu watu haki ya kuishi.
I knows about this, its not true.
5. Nani wamiliki wa DP World?
Ni ukoo wa kifalme wa Dubai
6. Uko wapi ukoo wa babake rais Samia? Baba wadogo, mashangazi, n.k. Au tuamini tunayoyasikia?
Hii inaingilia the right to privacy, kama hatukuuliza kwa Nyerere, Mwinyi, Ben, JK na.JPM, why Samia?.

Kuna issues kuhusu asili ya JPM niliiulizia ...

P
 
0
Sexless akili kubwa👍👍
 
RIP....Stanley Katabalo

Je mnakumbuka kile kisa cha balozi wetu wa Ufaransa.....nafikir wakti ule alikuwa Mh Anthony Nyaki................na mazungumzo ya simu na Mh. Mustapha Nyang'anyi...........dah!
Huyu Nyanganyi yuko wapi? Namkumbuka kutokana na kashfa ya kivuko cha UNIFLOAT pale ferry! Jamaa alishirikiana na marehemu colonel. Kashmir wakapiga hela kwa kununua ferry MTUMBA!’
Nyanganyi akaja fanya scandal nyingine akiwa Chairman wa ATCL akakodisha ndege hewa ya Kubeba mahujaji akiwemo mkwewe Kikwete!!
Sijui yuko wapi siku hızi?
 
Nimekumbuka mbali Sana. Antony Ngaiza Alumni, Nsumba Secondary School, 1971.
 
Nilishangaa kila mtu anasifia utawala wa Mwinyi na kusahau Loliondo
Achana nao, wengi wao ni watoto wasiojua tulikotoka na viongozi kama Ali Hasan Mwinyi aliyeigeuza Ikulu yetu Takatifu kuwa pango ya walanguzi.

Hawajui walikopotelea tausi waliotapakaa katika viwanja vya Karimjee na kuwa kivutio tosha kwa wageni waliobahatika kutembelea viwanja hivyo.

Hawajui kichowakuta wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya mafao na pensheni zao kukabidhiwa serikali ya Mwinyi iwafikishie.

Hawajui...ngoja niachie hapo kwani orodha ni ndefu sana. Kujadiliana na watoto wa aina hiyo ni heri ujadiliane na meza...
 
Sasa kama kulikuwepo changamoto kama hizo kwa waandishi wazalendo kama Katabalo kwa nini hatukuzisikia katika wasifu wa mzee wetu aliyepumzika kule mangapwani
 
Katabaro alikuwa mwandishi imara wa uchunguzi , kifo chake mama yangu alinikataza kusomea uandishi wa habari fani ambayo niliipenda sana.
 
Utawala ulikuwa dhaifu kwa Tanzania hii ,alishindwa kukusanya kodi, madawa ya kulevya ,walanguzi kujaa Ikulu huku Mke wake Siti akiwakaribisha .
 
Naikumbuka sana Kashfa ya Loliondo..................iko siku wahusika watajibu kama si mbele ya umma wa Watanzania basi mbele ya Mungu!
Usipepese macho , sema tu ukweli- mmoja wa wahusika wakuu tumemuona juzi akitembelea mkongojo, wengine kama akina Ndolanga wameshatangulia mbele za haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…