M/city haina uzuri wowote, samaki samaki pia ni yakawaida sana. Nimekula chips samaki pale mara kadhaa na juice, bei zao ni za wastani kwangu mimi, sio ghali na wala sio rahisi kivile. Mara ya mwisho kuwa pale tulikuwa na kampani ya Lugumi na alitoa ofa kwa wadada waliokuwa pale mida ya saa kumi na moja hivi jioni. Ingawa Lugumi hakuwa na kawaida ya kunywa whisky ama beer kutoka bar, mabaunsa wake walikuwa wanashuka na vinywaji kutoka kwenye msafara wake ndio alikuwa anakunywa hivyo. Wakuu muwe mnatembea na kuingia sehemu expensive walau mara tano kwa mwaka. Sasa mkuu ukienda Moyo Kitchen ama Coral Ridge Spur si ndo utazimia kabisa wewe, Maisha mafupi wakuu tembeeni musipige mahesabu sana.